Mahiga asema Tanzania haitambui Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel, baada ya Ndugai kunukuliwa akisema anautambua

Vyombo vya Habari vya Kimataifa vimemnukuu Spika wa Bunge, Job Ndugai akisema anaunga mkono tamko la Rais wa Marekani Donald Trump la kuutambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel

African states may follow Trump Jerusalem embassy move: Tanzania's speaker

Tanzania imekana kuwa inaunga mkono tamko hilo

Aiongea na Gazeti la The Citizen, waziri wa mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk Augustino Mahiga alisema Tanzania kama ilivyo kwa jamii yote ya kimataifa bado inaitambua Tel Aviv kama mji mkuu wa Israel

Ubalozi wetu upo Tel Aviv na utaendelea kubaki hapo. Kuna nchi zimetushawishi ila tutabaki Tel Aviv

Jana Rais Donald Trump alitangaza kuutambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel na kusema Marekani itahamishia ubalozi wake mji huo jambo ambalo limekosolewa duniani kote

=============================================================

International media outlets have quoted National Assembly Speaker Job Ndugai saying Tanzania was supporting announcement made by US President Donald Trump.

Dar es Salaam. Tanzania has distanced itself from international media reports that the East African nation was supporting the US recognition of Jerusalem as the capital of Israel.

International media outlets have quoted National Assembly Speaker Job Ndugai saying Tanzania was supporting announcement made by US President Donald Trump.

Speaking to The Citizen on Thursday, December 7, the minister for Foreign Affairs and East African Cooperation, Dr Augustine Mahiga, said Tanzania, just like the international community, continues to recognize Tel Aviv as the Israeli capital city.

“Our embassy is in Tel Aviv and we’ll remain there. Some countries have tried to convince us. We will remain in Tel Aviv,” though he declined to give detailed comments over the issue.

Yesterday, US president Donald Trump announced that the US now recognise Jerusalem as the capital of the Israel State, promising that his country will shift its embassy from Tel Aviv to Jerusalem, the announcement was received with criticism from various parties around the world.

Source: The Citizen
Tanzania kwa Israeli ni sawa na mbuzi mbele ya Tembo.
 
Kwa mimi, familia na ukoo wangu tunatambua mji mkuu wa israel ni jerusalem!.Na aibarikie israel nae hubarikiwa na ailaanie naye hulaaniwa.Tatizo watz wengi wazan kuna udin hapa apana.Israel ina madhehebu yote kama ilivyo hapa Tz kuna waislam,wakristu,wayahud,wapagan nk.lkn tutambue ya kwamba ni tayari Mungu alishaliteua ni Taifa lake teule.Na angalia Nchi zotes zilizo kiri na kuibariki israel zilivyo na nguvu kuanzia ya kiuchumi na mambo mengine.then angalia Nchi ambazo hazikuibarik hali yao ilivyo mfano mzur ni Tz nk.Hatutafanikiwa kwa chochote kama tusipo kiri Israel ni Taifa teule la Mungu na kufungua ubaloz wa Israel hapa Tz.Kenya,Ruanda,Ghana nk wanatuacha nyuma kwa kila nyanja ishu ni moja tuu tangu awali walikiri Israel ni Taifa teule la mungu.Na ata Nnchi za Arabu emiret wanakuwa na nguvu ya kiuchumi kwa ishu moja tu ni walishaikir na wanaendelea kuikubali Israel.Saaa siye tuzidi kuungana na hao wanao uza waafrika wenzetu huko libya tuangalie kama tutapumua hadi masia anarudi.
acha upuuzi wewe Israel yenyewe ni Taifa masikini linaishi kwa kutegemea misaada kutoka Marekani.....Hivi unajua bajeti karibia yote ya Israel inategemea pesa kutoka Marekani........Taifa gani teule wanatumia bunduki na vifaru kujilinda......kwa nini Mungu asiwalinde wateule wake?.....
 
Ndugai anautambua.

Mahiga hautambui.

Siku pogba akizungumza atasema hata kwenye biblia kunazungumza jerusalem ndio mji mkuu wa israel.

kwahyo kutakuwa na misimamo mitatu kwenye serikali moja. lakini jambo hilo ni lakawaida kwenye serikali hii.

Mimi pia natambua jerusalem kuwa ni mji mkuu wa israeli. Over.
 
Tusiingilie huu ujinga hata kidogo, Marekani inaweza kudeal na mataifa ya waislamu sio Tanzania, tusijaribu kabisa kuingilia vita vya wapalestina na waisraeli, sehemu zote mbili ziko backed up na mataifa powerful, tukiingilia tunajiweka kwenye black list ya mataifa ya waislamu mapema sana, soon utaanza kusikia ISIS Tanzania.

Hawajaambiwa watoe tamko kama wanaunga mkono au la, wasijipendekeze. Huyu spika hua anatamka bila kufikiria, sio kitu cha kwanza anasema ovyo, hakuna faida yoyote ile kuliongelea hili swala.

Kwani speaker ameongea kwa niaba ya serikali? Mbona unaogopa sana haya mataifa ya kiislamu? Hivi unamjuaa aliyeanzisha ISIS?
 
Mimi, raia mwema na mzalendo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nautambua Yerusalem kuwa Mji Mkuu usiogawanyika wa Taifa la Kiyahudi la Israel.
 
Hii inafahamika waziwazi Jerusalem ndio mji mkuu wa Israel, hii Tel Aviv ni mbwembwe tu.
 
acha upuuzi wewe Israel yenyewe ni Taifa masikini linaishi kwa kutegemea misaada kutoka Marekani.....Hivi unajua bajeti karibia yote ya Israel inategemea pesa kutoka Marekani........Taifa gani teule wanatumia bunduki na vifaru kujilinda......kwa nini Mungu asiwalinde wateule wake?.....
Na hujiulizi ni kwann huyo mmarekan anamsaidia kwa kila kitu!?. kwa nn asisaidie Taifa lingine ang'ang'anie tu pale jangwani!?.Jiongeze mkuu ndiyo maana ànazid kuwa na nguvu za kila kitu na kuitawa dunia
 
Mwanaume ni Trump Tu,wengine hata mseme vipi alichosema mwanaume ndiyo hicho hamuwezi kubadili kitu ni sawa na kelele za chura ambazo haziwezi kumuzuia Tembo kunywa maji.
 
Na hujiulizi ni kwann huyo mmarekan anamsaidia kwa kila kitu!?. kwa nn asisaidie Taifa lingine ang'ang'anie tu pale jangwani!?.Jiongeze mkuu ndiyo maana ànazid kuwa na nguvu za kila kitu na kuitawa dunia
Taifa la Israel lilianzishwa mwaka 1947 na Marekani ili kuzidhoofisha nchi za kiarabu zinazoizunguka .......kiufupi Israel ni kama kituo cha kijeshi cha Marekani chenye lengo la kuleta machafuko na vurugu middle east.....kabla waisrael hawajaivamia palestina middle east kulikuwa na amani baada ya israel kuingia amani ikatoweka....sasa wateule gani wa Mungu wanaosababisha vurugu na mauaji kila siku....?
 
Tusiingilie huu ujinga hata kidogo, Marekani inaweza kudeal na mataifa ya waislamu sio Tanzania, tusijaribu kabisa kuingilia vita vya wapalestina na waisraeli, sehemu zote mbili ziko backed up na mataifa powerful, tukiingilia tunajiweka kwenye black list ya mataifa ya waislamu mapema sana, soon utaanza kusikia ISIS Tanzania.

Hawajaambiwa watoe tamko kama wanaunga mkono au la, wasijipendekeze. Huyu spika hua anatamka bila kufikiria, sio kitu cha kwanza anasema ovyo, hakuna faida yoyote ile kuliongelea hili swala.
Kongole Mkulu umenena vyema
 
Kuna Mmoja kazungumza kwa niaba ya Serikal na Mwingine kazungumza kwa niaba ya Imani yake Hakuna Tatizo
Utawala uliofikitinika utauona tu. Mmoja kwa niaba ya BUNGE la Tanzania; "Tunaitambua Jerusalem". Mwingine kwa niaba ya SERIKALI ya Tanzania; " Hatutambui Jerusalem.
 
Kwani speaker ameongea kwa niaba ya serikali? Mbona unaogopa sana haya mataifa ya kiislamu? Hivi unamjuaa aliyeanzisha ISIS?
Speaker wa bunge ni mtu mkubwa serikalini haijalishi anaongea kivyake au la, statement yake hadi kuwekwa kwenye gazeti maana yake wamemsikia, mataifa ya waislamu yanapaswa kuogopwa ndiyo, doesn't matter aliyeanzisha ISIS ni nani, the fact kwamba ipo iko palepale.
 
Kuna Mmoja kazungumza kwa niaba ya Serikal na Mwingine kazungumza kwa niaba ya Imani yake Hakuna Tatizo
CCM ndugai anapingana na msimamo wenu msipanic yule ni mgonjwa akili zake aliziacha India kwenye matibabu
 
Back
Top Bottom