Jogoo Mstaafu
New Member
- Jan 15, 2009
- 3
- 0
Anolds kijana wangu!amani kwenu wana JF..
hivi umewah kutafakari hili suala zima la ulipaji mahari origin yake ni nn?!..na ni vigezo gain vinavyotumika ku evaluate thamani ya huyu mwanamke?. Embu fikiria, kitendo cha mwanaume kulipa mahari kina ulazima gani?, ukiangalia kwa makini ni kama mwanamke ananunuliwa vile!, na mtu akinunua kitu huwa anakitumia atakavyo,simply coz ameingia gharama!..jamani huu utamaduni (hii biashara) si unadhalilisha wanawake?
Suala la mahari ni la kimila, kidini na kimpenzi! Kwa mimi muumini wa dini ya Kiislamu mahari ni muhimu kwani ni zawadi kwa nayeolewa. Kiislamu kutokana na maandiko ya Kitabu chetu kitukufu anayeolewa ndiye hupewa mahari sio mzazi! Na mahari mara nyingi bi harusi huangalia uwezo wa mwenzi wake. Utashangaa mwanamme au anayeoa anaweza akaambiwa alipe hata kuku na kumsomea sura fulani kutoka kitabu kitakatifu. Au bi harusi anaweza kulipa kidogo kidogo katika maisha ya ndio yao. Kwa mila za Wasukuma kabila la mama yangu rangi ya bi harusi ndio ongezeko la wingi wa ng'ombe kwa mzazi! Naomba nisahihishwe pale nilipo kosea wana Jamii.