Mahari na nafasi yake katika ndoa... Je, utamaduni huu umepitwa na wakati?

mahari ni shukrani kwa wazazi tu basi na siyo hela inaweza kuwa kitu chochote ambacho wazazi watabaki nacho kama kumbukumbu.
Sema siku hizi watu wamefany mtaji eti mtu anaambiwa mahari milioni moja, ngombe wanne wanaotembea , vitenge doti ishirini hapo kuan ndoa kweli au biashara


kwetu mtoto hasa ikawa 'mweupe', ni ng'ombe 25 to 35! otherwise hujaoa....
 
kwetu mtoto hasa ikawa 'mweupe', ni ng'ombe 25 to 35! otherwise hujaoa....

...si inakubalika kulipa kidogo kidogo?

unatanguliza wawili kabla ya harusi, (kuhakikisha hujauziwa punda kwenye mfuko wa karatasi)...unamzalisha mtoto,....unaongeza mwingine mmoja maisha yanaendelea...au?
 
Kwa tamnaduni nyingi za kiafrika, hususani zile zenye mfumo dume, mwanamke hana/hakuwa na tofauti sana na bidhaa au resource nyingine. Ukoo wa mwanaume 'unanunua' mwanamke kutoka ukoo wa mwanamke kwa ajili ya kufanya kazi na kuzaa watoto ili kuongeza ukoo wa mwanaume.

Baada ya ukoo wa mwanaume kutoa mahari na ukoo wa mwanamke kuikubali na kuipokea, mwanamke anakuwa mali halali ya ukoo wa mwanaume. Ndio maana hata mwanaume akifa mwanamke alikuwa anarithiwa (kama mali nyingine!) ili kama bado kijana aendelee kuongeza ukoo pamoja na kufanya kazi. Hawezi kuolewa na mwanaume kutoka ukoo mwingine (kama ilivyo mali nyingine haziwezi kurithiwa na watu baki!).

Mambo haya kwa sehemu kubwa yamepitwa na wakati. Dhana ya mahari imebadilika sana (ingawa bado haijesha!) na kwa koo nyingi imebaki kuwa ni symbolic/gesture tu. Koo nyingi hazisisitizi tena mahari (inaweza kutajwa tu lakini ikalipwa robo tu au chini ya hapo!) kama prerequisite ya watoto wao kukaa pamoja. kuna mwanaume mmoja yeye aliambiwa apeleke senti tano (the physical brown coin!) kama mahari!

Dhana ya 'kuoa' pia inapungua na tunaelekea zaidi kwenye 'kuoana'! Lakini bado kwa sehemu kubwa mwanamke anahamia (anaolewa) ukoo wa mwanaume (wengine bado wabadilisha hata surname!). Bado mke akifa anazikwa kiumeni na si kwao.

Koo nyingi zimeacha kurithi wajane na watoto. Kwa upande mmoja hili ni zuri lakini kwa upande mwingine kwa kiasi limechangia ongezeko la watoto wa mitaani. Dhana ya collective responsibility katika ukoo inaondoka.

Kwa maoni yangu, utaratibu wa mahari utaondoka wenyewe (kwa wasio waislam!) kwa sababu itafika kipindi wahusika hawataona umuhimu tena. Uamuzi na taratibu za kuoa/kuolewa halitakuwa suala la ukoo tena bali familia na baadae mtu binafsi!

Hapa pagumu kwa kweli- mali halali ya ukoo wa mwanaume ?
 
Hapa pagumu kwa kweli- mali halali ya ukoo wa mwanaume ?

Pagumu hasa! Kwa kipindi hicho makabila yalikuwa yana-play role equivalent na dini kwa sasa (Kulikuwa na imani na miiko kadhaa!). Kwa sehemu kubwa hii ilifanya wanawake kushindwa kujitetea!

Lakini, personally, kama mwanamke unajisikiaje kutolewa mahari/kuolewa? Kama umeolewa unahisi uko affiliated na familia ya mume zaidi au kwenu zaidi?Unahisi 'kununuliwa'?
 
Pagumu hasa! Kwa kipindi hicho makabila yalikuwa yana-play role equivalent na dini kwa sasa (Kulikuwa na imani na miiko kadhaa!). Kwa sehemu kubwa hii ilifanya wanawake kushindwa kujitetea!

Lakini, personally, kama mwanamke unajisikiaje kutolewa mahari/kuolewa? Kama umeolewa unahisi uko affiliated na familia ya mume zaidi au kwenu zaidi?Unahisi 'kununuliwa'?

Mimi dada yangu alikataa kutolewa mahari wazee wakaja juu kweli wakidai hata kama hataki lazima kitolewe kitu kidogo hata kama ni shilingi 50. Na ilitolewa!! Nilishangaa.

Sasa mfano mwanamke aliolewa akatolewa mahari then wakahitilafiana na mumewe wakatengana au Mungu akamchukua mume kungali mapema then anakuja mwanaume mwingine anataka kuoa rasmi inakuwaje?
 
Mimi dada yangu alikataa kutolewa mahari wazee wakaja juu kweli wakidai hata kama hataki lazima kitolewe kitu kidogo hata kama ni shilingi 50. Na ilitolewa!! Nilishangaa.

Sasa mfano mwanamke aliolewa akatolewa mahari then wakahitilafiana na mumewe wakatengana au Mungu akamchukua mume kungali mapema then anakuja mwanaume mwingine anataka kuoa rasmi inakuwaje?

Katika unyago, mwanamke alikuwa anafundishwa 'uvumilivu'. Ni mara chache mnaweza kuhitilafiana halafu makatengana kwa mwanamke kuondoka kwa mume. Labda mwanaume amfukuze, in which case, mwanamke hawezi kurudi kwao bali atakwenda kwa wakwe zake (wazazi wa mume).

Mwanaume akifa, basi mmoja wa ndugu wa kiume wa mume 'anapaswa' kumrithi mwanamke. Sehemu nyingine mwanamke anapewa uhuru wa kuchagua mmoja kati ya shemeji zake ili amrithi.

Kule kwetu kama mwanamke akifa kabla hajazaa hata mtoto mmoja/au hata kwa mfano hazai, basi ukoo wa mwanamke walikuwa wanawajibika kutoa binti mwingine as a replacement!
 
Mtandao wa Jinsia TZ muongeze juhudin ili suala la ndoa lisitiswe kwani nihujumu masuala ya jinsia TZ,kusiwepo na dhana kwamba kuna Mtoto muhimu kuliko mwingine.
 
Katika unyago, mwanamke alikuwa anafundishwa 'uvumilivu'. Ni mara chache mnaweza kuhitilafiana halafu makatengana kwa mwanamke kuondoka kwa mume. Labda mwanaume amfukuze, in which case, mwanamke hawezi kurudi kwao bali atakwenda kwa wakwe zake (wazazi wa mume).

Mwanaume akifa, basi mmoja wa ndugu wa kiume wa mume 'anapaswa' kumrithi mwanamke. Sehemu nyingine mwanamke anapewa uhuru wa kuchagua mmoja kati ya shemeji zake ili amrithi.

Kule kwetu kama mwanamke akifa kabla hajazaa hata mtoto mmoja/au hata kwa mfano hazai, basi ukoo wa mwanamke walikuwa wanawajibika kutoa binti mwingine as a replacement!

Aha kumbe lakini hii imekaa kimila sana je katika dunia ya sasa watu wanaooana na kuishi kidaslama!! Bado mke atarithiwa iwapo mume atafariki na kumwacha akingali kijana? au ndo hatakiwi kuolewa tena? (najua wanawake mara nyingi akifiwa na mumewe huamua kubaki single ili alee watoto wake)
 
Je, Wazazi wa mwanaume nao hawastahili kupata 'shukrani' kwa matunzo mazuri ya mtoto wao kwa kuwa wamempa malezi mazuri, ana elimu nzuri, hakuwa muuza/mtumiaji unga n.k.?

Yes Wanastaili tena sawa kama wazazi wa mwanamke. Kama inawezekana wazazi wa pande mbili wawe wanatoa mahari then zinakwenda kwa wanandoa. Inapendeza sana. Kwakuwa ni moja ya tamaduni zetu, hata kama ni biased kwa upande mmoja, haina budi tuifate. Labda siku yaja ya kubadili hili swala la mahari lisiwe biased!!!


Je, kuna haya ya kuwa na kiwango maalum cha mahari maana utasikia wengine wanatakiwa watoe mpaka laki 5 au zaidi na ilhali kiwango hicho ni kikubwa mno kwa muoaji na wazazi wake?

Ingawa ni tamaduni zetu, lakini ndani yetu tuna subsets za utamaduni. Kutokana na subsets au sub-subsets unakuta mahari hutofautiana. Ukisema liwe uniformly labda tuliweke kwenye katiba, kitu ambacho kinaweza kuwa kigumu.
Nafikilia kuwa mtoa mahari anaweza akatoa zaidi kulingana na taratibu za wazazi wa mwanamke; well wengine wanaongeza kama mtoto kaenda shule, mweupe (baadhi ya makabila), n.k
 
Mahari ni kushukuru matunzo
alaaaahhh, kwani mtoto wa kiume hakutunzwa au...?? Yaani wazazi wa mtoto wa kiume wamemlea na kumsomesha na kumpa hekima ya kutochezea watoto wa watu instead aoe, then leo mseme wa kike tu ndio katunzwa..???? To me, hz ni mila za kale. Zinapelekea udhalilishaji wa watoto wa kike. And some wazazi wanazitumia vibaya, wewe mahari siku hz unakuta hadi millioni mbili, sasa hii ni shukrani au ni biashara.....!!..??

Kwa upande mwingine, mahari imefanya wazazi wengine kuwa-force mabinti zao kuacha shule ili waolewe. Hii ni kutokana na tamaa ya kutaka kupata fedha kupitia mahari. Hivyo kwa upande mwingine, imepelekea ndoa za mabinti wadogo, vijiji vingine even under 18 wanaolewa just kwa sababu ya mahari.

I believe kungekuwa hakuna return ya kuwa na mtoto wa kike in the form ya mahari, wazazi wangeswitch na kuona return pekee ni shule and hence kuolewa ni loss. But, for now, kuolewa ni profit kwa upande wao, as they focus zaidi kwenye risk ya watoto kufeli/kushindwa shule than return ya watoto kuwa na elimu. Hawaujui/wamesahau msemo wa kifedha usemao "high risk, high return".
 
Babu yangu aliniambia umhimu wa mali ni kumweka binti katika hali ya kuwaza kuwa akikosea kwa bwana yake atakuwa amewafanyia deni wazazi wake, hivyo akilipiwa mali ina kuwa ni bond ya kumfanya aheshim ndoa na kuwa mwangalifu....

Pia iliwezakana kuwa kama mzazi ana shida na hana mali, ila ana binti mdogo ambaye hajafikisha umri wa kuolewa, mzazi huyu anaweza kukopa ngómbe kwa mtu ambaye baadae atakuja kuwa bwana wa binti yake akishakuwa mkubwa! staili hiyo inaitwa "ekebhete" ukuryani.

Hapa ni swala la utamaduni kwa mtazamo wangu, pia naamini kuwa ndoa ya bila malipo huwa haina respect kama ya bwana kulipia. labda tu tuone kama pana uwezekano wa kuwa tunalipa both sides, yaani kidume alipe kwa wazaz wa binti na binti alipe kwa wazaz wa kidume, hapo ndo usawa kamili. na malipo yawe sawa.
 
Ndugu zangu naomba mnisadie mawazo.

Nimesikia mara kadhaa watu wakipeleka posa wanapochumbia na upande wa mwanamke wanataja mahari. Ninavyoelewa mpaka sasa mahari hizi zimekuwa zikitofautiana kati ya kabila moja na jingine na wakati mwingine kati ya familia na familia hata kama ni katika kabila moja. Sitaki kujadili uhalali wa kulipa au kutolipa mahari, lakini ninakwazika na kiasi kinachotozwa. Wakati kuna familia zinaweza kuamuru kuanzia vitu vichache kama msahafu au biblia na labda fedha kidogo kama courtesy tu, lakini kuna wengine wanaenda mbali kiasi cha kutoza ng'ombe 100 kwa binti mmoja. Pia wapo ambao wanatoza kiasi hicho cha ng'ombe na kukithaminisha kwa fedha ambapo huwa ni fedha kidogo labda elfu kumi kwa ng'ombe mmoja, lakini wengine wanatoza kwa bei ya soko.

Nilishtuka siku moja rafiki yangu ambaye by then tulikuwa tunafamiana vizuri sana vipato vyetu kwani ndio kwanza tulikuwa tumemaliza chuo alipotaka kuoa na aliambiwa atoe milioni 2!! ilinishtua si kidogo, kwani jamaa yangu ndio kwanza alikuwa ameanza kazi, na halafu si kwamba angetegemea mchango utoke nyumbani kwao bali mfukoni mwake, sijui iliendaje lakini baadaye tulisherehekea harusi. Ni hivi majuzi nimesikia tena kuna mtu kaambiwa mahari kiasi cha milioni sita laki tatu na nusu (6,350,000/=)fedha za kitanzania. Nikagundua kumbe sikuhitaji kushangaa milioni 2 wakati ule.

Kwa stahili hii kuoa na kuolewa ni biashara fulani yenye faida?
 
...Nilishtuka siku moja rafiki yangu ambaye by then tulikuwa tunafamiana vizuri sana vipato vyetu kwani ndio kwanza tulikuwa tumemaliza chuo alipotaka kuoa na aliambiwa atoe milioni 2!! ilinishtua si kidogo, kwani jamaa yangu ndio kwanza alikuwa ameanza kazi, na halafu si kwamba angetegemea mchango utoke nyumbani kwao bali mfukoni mwake, sijui iliendaje lakini baadaye tulisherehekea harusi. Ni hivi majuzi nimesikia tena kuna mtu kaambiwa mahari kiasi cha milioni sita laki tatu na nusu (6,350,000/=)fedha za kitanzania. Nikagundua kumbe sikuhitaji kushangaa milioni 2 wakati ule.

Kwa stahili hii kuoa na kuolewa ni biashara fulani yenye faida?
...naaam, naaam... yaani ni 'biashara' kamili ndugu yangu.

...unakuta mshenga anatumwa (tena) kwa 'wakwe' washuke 'dau',...wakwe kwa shingo upande watapunguza laki mbili u-nusu...

...mshenga atatumwa tena kulilia hali kwa 'wakwe', nao watafikia bei ya mwisho mfano; milioni moja kamili, hapo bwana harusi anapeleka laki tano na ahadi ya kumalizia 'baadae' kilichobakia!
 
hehehe..kazi kweli kweli.

Ila sasa kwa uelewa wangu nafikiri sasa hivi inakuwa kama kukomoana ingawa naona kama taratibu za kimila sasa hivi zinaishiwa nguvu hasa kwenye hili suala maana nakumbuka kuna sehemu jamaa yangu alikwenda kuoa, mwanamke (Mke mtarajiwa) ndiye aliyetaja mahari na mambo yakaenda sawa kabisa ila sasa kama ndio unakwenda kuoa halafu maamuzi yanatoka kwenye vikaoo vya ukooo mzima hapo lazima mwana uende na hela ya kutosha maana lazima utakutana na bei za Supermarket
 
Ha Ha Ha! Kwa mpango huu bado nitakuwepo sana tu na kama vp inabidi tu kukamua maziwa toka kwajirani. Kilo sita mbona si kitoto.
Wakuu mwakani ni ndo nilitaka kupeleka mahari sasa kama mambo yatakuwa hv basi nitanyoosha mikono.
 
Kamamanga haulali? Mda wote nakuona tu upo online au ndo unatafuta mahari nn?
 
Mahari muhimu bana, kama umependa msichana lazima utoe mahari. Iwe kwa gharama yeyote ile, nyie toeni tu msilalamike.
kutoa mahari hizo ni mila zetu wajemeni! Na mtu anayeacha mila yake ni mtumwa.
 
Kamamanga haulali? Mda wote nakuona tu upo online au ndo unatafuta mahari nn?
Haa haa haaa! Bila shaka na wewe pia hukulala ndio maana uliweza kumuona yeye online! Kuhusu mambo ya mahari, wee acha tu, ni maumivu!
 
Back
Top Bottom