Maharage Chande: Tuache kupeana maneno tamutamu; bei ya Tsh 27,000/= haitoshi kuunganisha umeme

RWANDES

JF-Expert Member
Jun 12, 2019
1,615
3,909
Leo tarehe 23.02.2022 mkurugenzi wa TANESCO, MAHARAGE CHANDE ameongea na vyombo vya habari kwa kueleza umma kuwa hakuna umeme wa tsh 27, 000/= tuache kupeana maneno matamu matamu katika kuendesha shirika hilo. Amesema ni vigumu sana kutofautisha mjini na vijijini kwani wote wanahitaji huduma hiyo kitu ambacho inasababisha shirika hilo kujiendesha kwa hasara kubwa!

Aidha kwa maoni yangu waziri wa nishati na Naibu wake je wakati wakiwasilisha taarifa mbalimbali za utendaji wa shirika hilo hawakai na wataalamu wakaambiwa kuhusu bei hizo za kuunganishiwa umeme?

Kutokana na kauli hizo kati ya waziri na mkurugenzi wa Tanesco ni kauli zipi ambazo umma utakuja kuziamini kutokana na mkanga'nyiko huo ambao hauleweki wa umeme wa tsh 27,000/=?

Ni hatari sana kwa mkurugenzi wa Tanesco kuambia umma kuwa unawezaje kununua tv ya sh 1,000,000/= halafu uhitaji umeme wa tsh 27000/= akumbuke kuwa hii nchi ni ya kwetu sote hata hivyo kutokana na nyakati tulizopo tulihitaji umeme wa gharama ya chini na siyo kukatisha tamaa umma kuwa hakuna umeme wa tsh 27,000/=.

Kwa hali hiyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ana kila sababu kufatilia kwa karibu utendaji wa shiraka hilo na Wizara ya Nishati kwa ujumla kwani tayari wananchi wameshaanza kutokuwa na imani na watendaji wa Tanesco na wizara husika.
 
Naomba majibu haya :-

Nguzo ni mali ya nani?
Luku / Mita ni mali ya nani?
Tanesco ni Profit au Business oriented?

Je hawajui kwamba pesa watakusanya zaidi wakiwa na wateja wengi zaidi ?. Umeme sio kama mchele unachota kadri unavyotaka ukiwa na megawatts za kutosha (unazalisha inabidi zitumike) unless otherwise hakuna sababu ya kuongeza ma-Megawatt ya kutosha iwapo mahitaji sio makubwa hivyo.

Tukimaliza Bwawa la Nyerere (if ever....) hizo Megawatt tutazitumia wapi?
 
Back
Top Bottom