Mahakama yaiamuru Serikali kurekebisha kifungu Sheria ya Mtandao

Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ameondolewa mamlaka ya kutoa adhabu isiyokatiwa rufaa kwa mshtakiwa anayekiri makosa ya kimtandao.

Uamuzi huo umetolewa na Mahakama Kuu,umeipa Serikali miezi 12 kukifanyia marekebisho kifungu cha 50 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao kilichobatilishwa.

Hata hivyo, mahakama hiyo imehalalisha vifungu vingine vyote vya sheria hiyo, ambavyo pia vimekuwa vikilalamikiwa na wadau wa matumizi ya mitandao na teknolojia ya habari.

Uamuzi huo umetokana na kesi ya kikatiba, iliyofunguliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)na mashirika mengine.

Katika hukumu iliyotolewa na majaji Profesa John Ruhangisa, Winfrida Korosso na Lugano Mwandambo, Mahakama ilibatilisha Kifungu cha 50 cha sheria hiyo, lakini ikaridhia vingine kuwa ni halali.

C1JSpqvWQAAp1u1.jpg
 
tubandikie nakala ya uamuzi tujisomee. section 50............compounding of offences. powers of dpp to fix penalties....revoked

Sababu za kuhalalisha vifungu vinginevyo ni vyema zikajulikana
 
Wanakurupuka kutunga SHERIA ili kukomoa kundi flani matokeo yake wanakiuka mpka KATIBA.. mfano kukurupuka kuanzisha Mahakama ya Mafisadi wakidhani watamkomoa Lowasa matokeo yake aibu Mahakama haina kesi kwani mafisadi wote wanatoka cccm
 
Mahakama yaiamuru Serikali!!!!! Ni Tanzania hii ya CCM au ni nyingine!!! Kama ni hivyo kweli, basi ngamia amepenya kwenye tundu la sindano.
 
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ameondolewa mamlaka ya kutoa adhabu isiyokatiwa rufaa kwa mshtakiwa anayekiri makosa ya kimtandao.

Uamuzi huo umetolewa na Mahakama Kuu,umeipa Serikali miezi 12 kukifanyia marekebisho kifungu cha 50 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao kilichobatilishwa.

Hata hivyo, mahakama hiyo imehalalisha vifungu vingine vyote vya sheria hiyo, ambavyo pia vimekuwa vikilalamikiwa na wadau wa matumizi ya mitandao na teknolojia ya habari.

Uamuzi huo umetokana na kesi ya kikatiba, iliyofunguliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)na mashirika mengine.

Katika hukumu iliyotolewa na majaji Profesa John Ruhangisa, Winfrida Korosso na Lugano Mwandambo, Mahakama ilibatilisha Kifungu cha 50 cha sheria hiyo, lakini ikaridhia vingine kuwa ni halali.
 
Baada ya mahakama kuamuru kurekebishwa kwa kifungu cha 50 cha sheria ya makosa ya mtandao (The Cyber Crime Act 201), sasa huenda sheria hiyo ikafumuliwa zaidi baada ya wanaharakati kupata matumaini ya ushindi katika shauri la kupinga kifungu kingine.

sheria.jpg

Kifungu ambacho sasa kinapingwa kwa nguvu kupitia kesi ya kikatiba, iliyofunguliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), na mashirika mengine ni kifungu cha 16, ambapo mmoja kati ya mawakili wa shauri hilo Jebra Kambole anadai kuwa kifungu hicho hakifai kwa kuwa kinaweza kumuingiza kila mtanzania matatani.

Amesema kifungu hicho kinahusu mtu anayeweka taarifa za uongo mitandaoni, na kwamba ndicho ambacho kimewakamatisha watu wengi wenye kesi mahakamani kwa hivi sasa.

Kifungu hicho cha 16 kinasema:-

"Mtu atakayechapisha taarifa au data katika picha, maandishi, alama au katika namna nyingine yoyote katika mfumo wa kompyuta, akijua kwamba taarifa au data ni za uongo, zinapotosha, zisizo sahihi, na kwa lengo la kudhalilisha, kutishia, kutusi au kwa naamna nyingine kudanganya umma au kuchochea utendaji wa kosa, atakuwa ametenda kosa, na akipatikana na hatia atalipa faini isiyopungua shilingi milioni tano au kutumikia kif

ungo kisichopungua miaka mitatu au vyote kwa pamoja".

Katika shauri hilo upande wa Jamhuri uliweka pingamizi la awali la kutosikilizwa kwake, na kinachosubiriwa ni maamuzi ya mahakama juu ya shauri hilo.

Wakili Jebra anasema ana matumaini makubwa kuwa kifungu hicho kitabatilishwa huku akishangilia maamuzi yaliyofanywa na mahakama katika shauri lingine ya kuiamuru serikali kukifanyia marekebisho kifungu cha 50 cha sheria hiyo.

Jebra1.JPG

Wakili Jebra Kambole

Katika shauri hilo ambalo mahakama ilitoa maamuzi mwishoni mwa mwezi Desemba , 2016 Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ameondolewa mamlaka ya kutoa adhabu isiyokatiwa rufaa kwa mshtakiwa anayekiri makosa ya kimtandao.

Uamuzi huo ulitolewa na Mahakama Kuu na kuipa Serikali miezi 12 kukifanyia marekebisho kifungu hicho ambacho kinasema

Kifungu.JPG

Kubatilishwa kwa kifungu hicho, kinamfanya wakili Jebra Kambole kupata usingizi mzito, ambapo amesema hatua hiyo ni ya kihistoria, kwani haijawahi kutokea sheria ikatungwa halafu ndani ya mwaka mmoja ikaonekana kuwa na mapungufu na kutakiwa kufumuliwa.

"Uzuri katika vipengele ambavyo mahakama imehalalisha hakuna kipengele cha 16 ambacho ndio mwiba, tunafanyia kazi na huenda tukakata rufaa, cha hamsini kwetu ni usingizi mkubwa sana" Amesema Wakili Jebra

Chanzo: EATV
 
Wewe Wakili unapinga kifungu cha ccm wanachotumia kuwafunga watu wanawakosoa wakati wao ni malaika
 
tubandikie nakala ya uamuzi tujisomee. section 50............compounding of offences. powers of dpp to fix penalties....revoked

Sababu za kuhalalisha vifungu vinginevyo ni vyema zikajulikana
Nimeomba mwenye kopi ya hukumu atuwekee!
 
Adhabu isiyokatiwa rufaa????!!!!!
Waliotunga walikuwa wana matatizo ya akili
 
Back
Top Bottom