venance7
JF-Expert Member
- May 15, 2019
- 555
- 1,637
Mahakama kuu ya Tanzania imetoa hukumu ya kesi ya kuchafuliwa jina iliyokuwa ikimkabili mkurugenzi mkuu wa gazeti la Tanzanite na mwanaharakati huru, ndugu Musiba dhidi ya aliyekuwa Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje na mgombea Urais kupitia ACT-Wazalendo, ndugu Bernard Membe. Mahakama hiyo imemtaka Musiba kulipa kiasi hicho cha pesa.
==========
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imemuamuru mwanahabari anayejitambulisha kama mwanaharakati huru, Cyprian Musiba kumlipa fidia ya Sh6 bilioni aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje katika Serikali ya Awamu ya Nne, Bernard Membe.
Hukumu hiyo imetolewa leo Alhamisi Oktoba 28,2021 na Jaji Joacquine De Mello aliyeisikiliza kesi hiyo.
Katika hukumu hiyo Musiba ametakiwa kumlipa Membe kiasi hicho cha fedha pamoja na gharama zote za uendeshaji wa kesi kwa zaidi ya miaka miwili.
Pia imeweka zuio la kudumu kwa Musiba la kutokumkashifu Membe au kusema uongo dhidi yake.
Mwananchi
Pia, soma=> Benard Membe: Musiba hasimami tena na kujifanya yeye ni Mungu Mtu. Huko uliko naomba hela zangu