Mahakama ya Rufani Nigeria yamruhusu Peter Obi kupinga matokeo ya Uchuguzi

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,400
Mahakama ya Rufani nchini Nigeria imetoa ruhusa kwa mgombea wa chama kiloshindwa cha Labour bwana Peter Obi kupinga matokeo ya uchaguzi ambapo ulimpa ushindi mgombea wa chama cha APC bwana Bola Tinubu.

Mapema mwezi huu mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini Nigeria bwana Mahmood Yakubu alitangaza ushindi kwa bwana Tinubu kwa kura milioni 8.8.

Bwana Obi ambae ni wa chama cha Labour, alitangazwa kuwa mshindi wa tatu katika uchaguzi huo aliwasilisha madai ya kupinga matokeo hayo tume ya malalamiko ya uchaguzi mjini Abuja tarehe 20 March kutaka kupinga matokeo hayo na kubatikisha ushindi wa bwana Tinubu.

Kwa mujibu wa mwanasheria wa bwana Obi maombi ya kupinga matokeo yamezingatia vipengele vya katiba ya Nigeria, sheria ya uchaguzi ya mwaka 2022 na sheria za mahakama ya Rufaa.

Katika pingamizi hilo bwana Obi anataka ama yeye ndiye atangazwe mshindi na raisi wa Nigeria au kutangazwe uchaguzi mpya wa raisi ambao bwana Tinubu hataruhusiwa kushiriki.

Katika uchaguzi huo bwana Obi alipata kuta milioni 6,101,553 ambazo ni asilimia 25 ya majimbo yote 16 yalopigiwa kura.

Peter Obi ni mgombea ambae aliitwa ni "hurricane" yaani kimbunga kwa mtindo wa siasa zake ambazo zilikonga nyoyo za vijana wa nchi ya Nigeria ambao wamekuwa wakihangaka kwa kukosa ajira.

Katika majimbo hayo 16, Obi alishinda majimbo 12 na kukosa majimbo kama la Lagos ambalo ndilo lilokuwa na utata wa kutoa matokeo yaloridhisha.

Peter Obi alijiunga na chama cha Labour mwaka 2022 akitokea chama tawala cha PDP ambacho ni moja ya vyama vkuuu vya siasa nchini Nigeria. Vyama vingine ni cha APC ambacho kama vilivyo vyama vingine barani Afrika ndo chama kinoshika dola nchini Nigeria.

Chama cha PDP ndicho kilichoshika madaraka katika miaka ya 2000 chini ya maraisi kama Olusegun Obasanjo na waziri wake wa fedha mama mchumi Ngozi Okonjo- Iweala na baadae akaja bwana Goodluck Jonathan ambae alikuja kushindwa katika uchaguzi wa mwaka 2015 na jenerali Muhammadu Buhari wa chama cha APC.

Kabla ua uchaguzi wa mwaka huu bwana Peter Obi alikuwa ni gavana wa jimbo la Anambra lililoko kusini mashariki mwa Nigeria. Jimbpo hili ni maarufu kwa shughuli za kilimo na biashara na ni moja ya majimbo maarufu barani Afrika kwa kuwa na kiwanda cha vifaa vya magari na uundaji wa magari kiitwacho Innoson.

Kwa wale ambao hawajafika Anambra ni jimbo ambalo lina maendeleo makubwa kutokana na kutumia uzuri rasilimali zake kama mafuta na gesi. Mapato ya maliasili hizi ndo yamefanikisha kujengwa kwa vyuo vikuu, miundiombinu kama barabara na madaraja kama lile daraja kubwa linopita juu ya mto Niger kuelekea mji mkuu wa jimbo wa Onitsha.

Kwenye elimu jimbo la Anambra laongoza kwa ubunifu na sayansi na teknolojia na ndipo kilipo vyuo vikuu vya Nnandi Azikiwe, Chukuemeka Ojwuku (zamani chuo kikuu cha Anambra), chuo kikuu cha masuala ya elimu, na vyuo vikuu vitatu vya ufindi vya Oko, Nwafo Orizu na Umunze na chuo kikuu cha kilimo cha Anambra Polytechnic.

Hivi vyote ni vyuo vya serikali na vipo vyuo vikuu binafsi vipatavyo 12.

Nigeria ni nchi ya tatu kwa ukubwa barani Afrika lakini bado yaaminishwa kuwa nchi hiyo ni moja ya nchi maskini sana.

Chinua Achebe mmoja wa waandishi mahiri wa fasihi andishi atokea katika jimbo hili la Anambra. Huyu ndie mtunzi wa kitabu maarufu ambachi ni lazima kila mwanafunzi wa sekondari wa lugha akisome kiitwacho "Things Fall Apart" na harakati za bwana Obi Okonkwo.

Things Fall Apart, No longer at Ease, na Arrow of God ni vitabu vizuri ambavyo vyatoa mwekeleo wa mwafrika na safari yake ya kujikomboa kifikra.
 
Inakuwaje Taifa la watu 200mil wapiga kura wasifike milioni 50?

Marekani wako 330mil, wapiga kura 2020 walikuwa 150mil

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Inakuwaje Taifa la watu 200mil wapiga kura wasifike milioni 50?

Marekani wako 330mil, wapiga kura 2020 walikuwa 150mil

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Ndivyo mambo yalivyo.

Ukiishatambua kuwa kuna siasa za kilaghai huwa wakosa msukumo.

Wanigeria khasa vijana wamekata tamaa ya kuona mabadiliko yakitokea ya hali zao ukizingatia uchaguzi kabla ya huu ulijawa na vitimbi vya polisi na vikosi kazi vilokuwa vikitesa wananchi.

Hivyo katika uchaguzi wa mwaka huu wapiga kura wengi waliamua kukaa pembeni.

Nigeria nchi maarufu barani Afrika na duniani na ikiwa imekalia ukwasi mkubwa wa maliasili nchi hiyo yaishindwa kuboresha maisha ya wananchi wake ambao wengi wakiribia asilimia 60 ni vijana.

Ofisi ya takwimu bila aibu imesema watu waso na ajira ni asilimia 33 (kwa 2020) na sasa yasemwa ni 42% na kipato cha chini ni dola 65!
 
Back
Top Bottom