Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 14,939
- 20,399
Habari zinazotoka katika shirika la habari la Italia ANSA zinasema kwamba waziri mkuu wa Italia Silvio Berlusconi ameondolewa kinga dhidi ya mashataka au "immunity law" yoyote yale dhidi yake na sasa ataweza kushtakiwa.
Majaji wamesema kwamba "immunity law" inawabagua wananchi dhidi ya viongozi kwamba wote ni sawa na pia inapingana na katiba ya nchi.
Hivyo basi baada ya hatua hii itabidi bwana Berlusconi ajiuzuru na kusimama kizimbani kujibu mashtaka mbalimbali likiwemo la kuhusu rushwa.
Mahakama hiyo ya katiba imefikia uamuzi huo baada ya upande wa mashtaka kuwa na uzito wa madai dhidi ya bwana Berlusconi na hivyo kumtaka ajiuzuru na hatimae kusimama kizimbani.
Kitakachofuata kinasubiriwa kwa hamu, patamu hapo!
Immunity Law au kinga dhidi ya mashtaka kwa viongozi wa juu wa serikali imekuwa ikitumiwa katika nchi nyingi duniani hasa Afrika na imekuwa ikitumiwa vibaya.
Fuatilia habari zaidi kutoka ANSA katika link ifuatayo ambayo ni kwa lugha ya Kiingereza:
http://wwww.ansa.it/site/notizie/awnplus/english/english.html
Mahakama ya Italy yaamuru Berlusconi aende jela miaka 4.
Mahakama mjini Milan nchini Italy leo imemtia hatiani tajiri waziri mkuu wa zamani Silvio Berlusconi kwa makosa ya wizi wa kalamu ambao ulipekea kutokulipa kodi inavyopaswa.
Berlusconi ameamuriwa kulipa gharama za kesi kiasi cha euro milioni 10
Berlusconi na wenzake kumi, walikuwa wakituhumiwa kwa kosa la kufanya malipo hewa kwa kampuni ya haki miliki ya kimarekani kupitia benki za nje ya Italy na baadae kujirudishia kiasi kikubwa cha pesa hizo.
Pamoja na kifungo hicho, pia Berlusconi amefungiwa kugombea nafasi yoyote ya uongozi nchini humo ingawa ni jana tu alitangaza kutogombea nafasi ya waziri mkuu kwenye chaguzi zijazo.
Berlusconi ambae ana umri wa miaka 76 atatumikia kifungo cha mwaka mmoja jela kutokana na uratatibu wa kukata rufaa ambao unaweza kuchukua hata miaka mitatu na pia kwasababu jela za nchini humo zimejaa wafungwa.
Berlusconi pia bado anakabiliwa na kesi ya kufanya malipo kwa ajili ya kuhudumiwa vitendo vya ngono na msichana wa miaka 17. Mzee huyo ni mtu mashuhuri katika hafla za ngono, maarufu nchini Italy kwa jina la "bunga bunga"
Jaji Edoardo d'Avossa akisoma hukumu kwa Berlusconi.