Mahakama kuu yapiga marufuku Mkutano mkuu wa CUF kufanyika

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
UPDATES FROM HIGH COURT-DAR ES SALAAM

DATE: 04 DECEMBER, 2018

1. MAHAKAMA KUU YAZUIA KUFANYIKA MKUTANO MKUU FEKI WA LIPUMBA.

2. SHAHIDI WA LIPUMBA AKIRI WALISIMAMISHWA UANACHAMA NA BARAZA KUU LA UONGOZI LA TAIFA NA WALIKATA RUFAA.

3. AKIRI KATIBA YA CUF HAINA KIFUNGU KINACHORUHUSU ALIYEJIUZULU KUTENGUA KUJIUZULU KWAKE.

THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF–Chama Cha Wananchi)

TAARIFA KWA UMMA:

LEO TAREHE 4/12/2018 MAHAKAMA KUU KANDA YA DAR ES SALAAM MBELE ya Mheshimiwa Jaji DKT BENHAJJ MASOUD imetoa AMRI YA KUHIFADHI HALI ILIYOPO SASA [Maintenance of Status Quo] KWA MAANA YA KUZUIA KUFANYIKA KWA MKUTANO MKUU ‘FEKI’ ULIOPANGWA KUITISHWA NA LIPUMBA NA GENGE LAKE mpaka hapo shauri la Msingi Namba 23/2016 litakapotolewa Uamuzi.
Uamuzi huo umetolewa mbele ya Wasomi Mawakili wote waliohudhuria Mahakamani hapo Mhe. Juma Nassoro, Mpare Kabe Mpoki, Daimu Halfani, Rehema Mtulia(AG), Mashaka Ngole, Majura Magafu na Samwel Mutabazi(RITA).

Uamuzi huo umetolewa kutokana na Mhe. Joran Lwehabura Bashange [NAIBU KATIBU MKUU TANZANIA BARA] na Mhe. Nassoro Ahmed Mazrui [NAIBU KATIBU MKUU ZANZIBAR] kufungua shauri dogo [Miscelleneous Civil Application No. 40/2018 arising from Civil Cause No. 23/2016] lililoiomba Mahakama kuzuia kufanyika Mkutano Mkuu huo mpaka pale shauri la Msingi linalohoji UHALALI WA LIPUMBA NDANI YA CUF litakapotolewa uamuzi, ambapo tayari Mahakama Kuu ilishapanga kutolewa uamuzi shauri Namba 23/2016 mwakani January 15, 2019.

Leo shauri Na. 40/2018 lilikuja kwa ajili ya kutolewa uamuzi wa jumla, Hata hivyo Mahakama Kuu imeahirisha kutoa Uamuzi huo na kujielekeza katika kutoa AMRI/ORDER ya kuhifadhi hali iliyopo na kwamba kusifanyike chochote mpaka pale Mahakama itakapotoa Uamuzi katika mashauri ya msingi Namba 23/2016 linalohoji uhalali wa msajili Mutungi kumtambua Lipumba na shauri Namba 13/2017 linalohoji uhalali wa RITA kusajili Bodi ya Wadhamini mpya ya CUF.

Mbali na shauri hili dogo pia Lipo shauri Namba 248/2018 ambalo ni Makhsusi lililofunguliwa kwa ajili ya Kupinga UCHAGUZI FEKI WA LIPUMBA NA GENGE LAKE mbele ya Jaji Stephen Murimi Magoiga.

Akizungumza na Wanachama wa CUF waliohudhuria mahakamani hapo Naibu Katibu Mkuu TZ-Bara Mhe. Joran Bashange-amewataka wanaCUF Tanzania nzima kutembea kifua mbele na kwamba wasiwe na wasiwasi wowote juu ya hatma ya Chama chao.

“…Leo Mahakama imetoa Amri ya kuziua kufanyika Mkutano Mkuu FEKI uliopangwa kufanywa na Lipumba kwa lengo la kutaka kumfukuza Katibu Mkuu Maalim Seif na Viongozi wengine ili wapate uhalali wa kuendeleza hujuma zao dhidi ya CUF. Tumefanikiwa kuwazuia. Hawatafanikiwa. Tembeeni kifua mbele na wala msiwe na wasiwasi wowote. Chaguzi zote FEKI zilizofanyika TUTAZIFUTA na kuanza upya. Viongozi wenu tupo Imara na Tunaamini HAKI ITASIMAMA NA TUTASHINDA MAPAMBANO HAYA.” Alisema Bashange.

Shauri la RITA No.13/2018;

SHAURI LA RITA limeendelea leo kwa upande wa Lipumba kuleta shahidi wake Thomas Malima. Amehojiwa na kufunga ushahidi wake ambapo kesho saa 3 asubuhi ataletwa Shahidi wa Mwisho kwa upande wa Lipumba ikiwa ni hatua za mwisho kabisa za kusikilizwa kwa shauri hili na baadae kutolewa Uamuzi.

Tangu saa 3:30 Asubuhi mpaka saa 12 jioni Thomas aliwekwa kiti moto na Wasomi Mawakili Daimu Halfani, Juma Nassoro na Mpare Kabe Mpoki kiasi ambacho kwa jinsi alivyobanwa alilazimika kukiri kuwa;

1. Katiba ya CUF haina Ibara inayoruhusu kiongozi aliyejiuzulu kutengua kujiuzulu kwake.

2. Akiri kuwa Walisimamishwa Uanachama na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa yeye( Malima), Abdul Kambaya, Lipumba, Sakaya, Kapasha, Shashu Lugeye na Masoud Muhina lakini Msajili Jaji Mutungi ndiye aliyewarejesha.

3. Akiri kuwa baada ya kusimamishwa na wengine kufukuzwa uanachama wote waliandika barua za KUKATA RUFAA kwenda kwa Mkutano Mkuu wa Taifa na kuzikabidhi kwa Katibu Mkuu Maalim Seif.

4. Akiri kuwa Rufaa zao mpaka sasa hazijasikilizwa.

5. Akiri kuwa Msajili hana mamlaka kwa mujibu wa Katiba ya CUF kuingilia masuala ya ndani ya CUF na wao hawaruhusiwi/hakuna kifungu kinachowaruhusu kupeleka Malalamiko yao kwa Msajili.

6. Fomu ya Usajili wa Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ilikosewa badala ya wajumbe 9 wao walijaza Wajumbe 11.

7. Adai nusu ya kolamu ya Wajumbe wa Baraza Kuu ni Wajumbe 8 tu badala ya 32.

8. Kikao chao cha Baraza Kuu kilihudhuriwa na Wajumbe 15. Haifahamiki Wajumbe wapya walithibitishwa na nani wakati kolamu ya kikao haijatimia.

9. Adai Lipumba hajawahi Kujiuzulu. Bali aliandika barua ya kusudio la kujiuzulu.

10. Ashindwa kuthibitisha kwa mujibu wa Katiba ya CUF wapi Kiongozi aliyejiuzulu anaweza kutoa KUSUDIO na akawa bado hajajiuzulu? Kwa mujibu wa Ibara ya 117(1) ya Katiba ya CUF.

11. Kama Lipumba hajajiuzulu! ALITENGUA NINI?

12. Marehemu nao waorodheshwa katika mukhtasari/taarifa ya kikao chao.

13. Akiri kuwa Kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa kinaweza kuongozwa na mjumbe wake kama Mwenyeikiti na Makamu Mwenyekiti hawakuhudhuria au hawapo kwa sababu yeyote ile.

14. Mukhtasari wa Kikao na Saini ya Maalim Seif iliyogushiwa yazua kizazaa kingine.

15. Atoa ushahidi wa uwepo wa makundi mawili na kila moja likiwa na Baraza Kuu moja la Lipumba lenye wajumbe 15 na lingine la Maalim Seif lenye wajumbe 42. Exhibit zatolewa kuthibitisha idadi hiyo.

16. Ashindwa kujibu ilikuwaje lipumba aliteua wakurugenzi bila kushauriana na makamu Mwenyekiti kwa mujibu wa katiba ya CUF?

17. Ashindwa kujibu kwa nini wameshindwa kuwasilisha muhtasari MAHAKAMANI kuthibitisha kufanyika kikao cha BARAZA KUU LA UONGOZI LA TAIFA ‘FEKI’ la Lipumba la kuteua wajumbe feki wa Bodi ya Wadhamini.

18. Akiri msajili hana mamlaka ya kuteua viongozi wa CUF kwa mujibu wa Katiba ya CUF Toleo la mwaka 2014.
Haya ni baadhi tu ya masuala yaliyoulizwa katika Cross Examination iliyofanywa na Wasomi Mawakili wa CUF kwa Thomas Malima.

TUKUTANE KESHO TAREHE 5/12/2018 SAA 3 ASUBUHI TUMALIZE KAZI.

HAKI SAWA KWA WOTE

Imetolewa na kurugenzi ya Habari CUF-Taifa;

SALIM BIMANI
MKURUGENZI HABARI.
 
Msaliti na Mkuu nyuma msaliti kuua democrasia tuwazomee
 
UCHAGUZI FEKI WA LIPUMBA NA GENGE LAKE
kJZWYia.gif

Hahahahaaa!!..Nchi hii kwa Chaguzi feki na mimi nilifikiri ni zile za CCM tu....mbavu zangu jamani.
 
Aluta Continua
 
Mzee Lipumba hebu acha uhuni uhuni; hivi vyama vinaongozwa kwa misingi ya kisheria, huoni sasa unajiaibisha mbele ya wajukuu zako; watajifunza nini toka kwako?? aaa Mzee mwenzangu hebu acha mambo hayo!!
 
Uamuzi huo umetolewa mbele ya Wasomi Mawakili wote waliohudhuria Mahakamani hapo

Nimezoea kuona Mawakili Wasomi na siyo wasomi mawakili

Je tofauti yake ni nini, naomba kujua ndugu wabobezi wa sheria
 
Hiyo mipango ilikuwa ikamilike 2019 so muda wa kujipanga na uchaguzi kwa CUF unakuwa tayari haupo tena na ushirikiano kivyama utakuwa umeshapigwa chini January 2019 kutoka kwenye Bunge Hovyo linaloongozwa na yule mtu wa Dodoma aliyempiga mgombea mwenzake fimbo wakati wa kura ya maoni.
Mipango yote hiyo inasimamiwa na kiongozi ambaye anaomba kuombea kila uchwao wa Muumba
 
Back
Top Bottom