Mahakama Kuu Kanda ya Tabora yatupilia mbali pingamizi la Wakili Husna dhidi ya Kafulila

Dotto Mnzava

R I P
Mar 6, 2014
865
427
Mahakama Kuu Kanda ya Tabora inayosikiliza kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi jimbo la Kigoma Kusini ilofunguliwa na David Kafulila dhidi ya washtakiwa; Husna Mwilima, Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya uvinza kama msimamizi wa uchaguzi na Mwanasheria mkuu wa Serikali ilipokea pingamizi toka kwa wakili wa Husna Mwilima kutaka Mahakama Kuu isiendelee na kesi hiyo kwakuwa Mhe Kafulila hakufuata taratibu katika ufunguzi wa kesi hiyo.

Katika utetezi wa wakili wa Kafulila Daniel Lumenyera, Tundu Lissu waliomba mahakama itupilie mbali pingamizi hilo la wakili maarufu Fungamtama kwa hoja kuwa ni usumbufu kwa mteja wao na halina mana yoyote kwa kesi ya Msingi.

Leo Jaji anaesikiliza kesi hiyo Bi Leila amezingatia ombi la Fungamtama na utetezi Lumenyela na kuamua kutupilia mbali pingamizi hilo la wakili wa Husna na kumtaka Husna Mwilima kumlipa Kafulila gharama za usumbufu kwa kuweka mapingamizi yenye sura ya kupoteza muda na usumbufu.

leo Mahakama imendelea na hoja ya kutathimini gharama ya dhamana ambayo Mhe Kafulila atapaswa kuweka kama dhamana ya kesi ili kesi ya msingi iweze kuanza.

Uamuzi kuhusu kiasi gani Mhe Kafulila atalipa kama dhamana utatolewa kesho na Mahakama.
 
tumbili ushindi ni wako. Tunakuhitaji bungen ukashirikiane na tingatinga kuibua maovu
 
.. tuendelee kumuombea Kafulila. Tunamhitaji sana bungeni
 
Mahakama Kuu Kanda ya Tabora inayosikiliza kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi jimbo la Kigoma Kusini ilofunguliwa na David Kafulila dhidi ya washtakiwa; Husna Mwilima, Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya uvinza kama msimamizi wa uchaguzi na Mwanasheria mkuu wa Serikali ilipokea pingamizi toka kwa wakili wa Husna Mwilima kutaka Mahakama Kuu isiendelee na kesi hiyo kwakuwa Mhe Kafulila hakufuata taratibu katika ufunguzi wa kesi hiyo.

Katika utetezi wa wakili wa Kafulila Daniel Lumenyera, Tundu Lissu waliomba mahakama itupilie mbali pingamizi hilo la wakili maarufu Fungamtama kwa hoja kuwa ni usumbufu kwa mteja wao na halina mana yoyote kwa kesi ya Msingi.

Leo Jaji anaesikiliza kesi hiyo Bi Leila amezingatia ombi la Fungamtama na utetezi Lumenyela na kuamua kutupilia mbali pingamizi hilo la wakili wa Husna na kumtaka Husna Mwilima kumlipa Kafulila gharama za usumbufu kwa kuweka mapingamizi yenye sura ya kupoteza muda na usumbufu.

leo Mahakama imendelea na hoja ya kutathimini gharama ya dhamana ambayo Mhe Kafulila atapaswa kuweka kama dhamana ya kesi ili kesi ya msingi iweze kuanza.

Uamuzi kuhusu kiasi gani Mhe Kafulila atalipa kama dhamana utatolewa kesho na Mahakama.

Tunamuombea mh kafurila aweze kufanikiwa
 
huyu Fungamtama ndio alikuwa wakili kuitetea IPTL katika sajata la ESCROW..
 
Back
Top Bottom