Mahakama Kuu imetoa siku 14 Mwanasheria Mkuu atoe ufafanuzi kuhusu mapingamizi ya CyberLaw

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Cyber-Crime-.jpg


MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, leo imempa siku 14 Mwanasheria Mkuu wa Serikali kueleza kama ana maelezo yoyote au pingamizi juu ya kesi iliyofunguliwa na jopo la mawakili 7 wanaopinga baadhi ya vipengele vya Sheria ya Makosa ya Mtandaoni ya mwaka 2015 iliyoanza kutumika Septemba 1, 2015 wakati haijafanyiwa marekebisho yaliyowasilishwa na wadau mbalimbali katika mamlaka husika.

Upande wa Jamhuri uliwakilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) wakati upande wa utetezi uliongozwa na wakili Benedict Ishabakaki. Kesi hiyo ya kikatiba ilikuwa imepangwa kupangiwa majaji leo Septemba 15, 2015.

Kesi hiyo itasikilizwa na majaji watatu chini ya Mwenyekiti wake Prof. Jaji John Ruhangisa, Jaji Lugano Mwandamo na Jaji Winfrida Korosso.

Mahakama imempa AG siku 14 awe amewasilisha kwa maandishi maelezo kama ana pingamizi lolote juu ya kesi hiyo ya kikatiba au awe amejibu malalamishi ya mlalamishi ambaye ni wakili wa kujitegemea, Jebra Kambole.

Mara baada ya AG kuwasilisha maelezo yake, walalamishi watapewa siku saba au kabla ya Oktoba 7, 2015 wawe wamejibu mambo ambayo yatakuwa yameainishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Kesi hiyo inasimamiwa na jopo la mawakili saba (7) wa kujitegemea na kesi hiyo itatajwa Oktoba 22, 2015.

Akizungumza mara baada ya kutajwa kwa kesi hiyo wakili Kambole, amekariwa na FikraPevu akisema kitendo cha serikali kupuuza maoni ya wadau wa habari na haki za binadamu juu ya baadhi ya vipengele vya sheria hiyo ni mwendelezo wa ukandamizaji wa kuzuia kuwapa uhuru wananchi kujieleza pamoja na sekta ya habari nchini.

Mawakili hao wanaiomba Mahakama kutengua baadhi ya vifungu vya sheria hiyo ikiwemo kifungu cha 4,5, na 45 (4) cha sheria ya makosa ya mitandao amabcho kinazuia haki ya kutafuta, kupata na kutoa taarifa na hivyo kukinzana na ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania.

Kifungu cha 6,7,8,10,11,14,19,21 na 22 vya Sheria hiyo ambavyo vinaelezwa kuwa na maneno yasiyo na tafsiri na hivyo kuhofiwa kuwa vinaweza kupekeleka taafsiri mbaya kwa watekeleza sheria na hivyo kupelekea uvunjifu wa haki za binadamu na kukiuka ibara ya 17 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Vipengele vingine kifungu cha 31,33,34,35 na 37 vya sheria hiyo vinatoa maamlaka kwa Polisi kufanya upekuzi na kuchukua kompyuta bila idhini ya mahakama hivyo kukinzana na ibara ya 16 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano. Na kifungu 38 cha sheria hiyo kinachonyima haki ya mtu kusikilizwa na mahakama hivyo kupingana na ibara ya 13(6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Baadhi ya mawakili katika kesi hiyo ni pamoja na Harold Sungusia, Flugence Massawe, Jeremiah Mtobesya, Benedict Alex, Boka Melkisedeckm Neema Ndemno na Jebra Kambole.


Chanzo
: Mahakama Kuu imempa AG siku 14 kutoa maelezo yaliyowasilishwa kupinga sheria ya makosa ya Mtandao
 
Well done!

Haya mambo ndo watu tunataka tuyaone kwa wasomi wetu sio kuwa mazuzu bila kuonyesha michango yao katk jamii.

Nasema tena well done pambaneni mpaka kieleweke
 
serikali ina rekodi mbaya za kushindwa kesi,,,,sitashangaa........
 
It is a commendable attempt but a bit late move.

This was supposed to begin during the Katiba mpya's sessions that ended into raping of wananchis' opinion on the engagement of corpses' votes. Samwel Sitta and Samia Suluhu, Im telling you, you have a lot to explain before ALAH's cort for what you did. You can pretend to be adamant now but before God you are as soft as Vaseline Jelly!

I will never ever forget and forgive for the kind of rudeness that you inflicted to the people of the republican of Tanzania for the interest of a meager and greedy group of people.

Sooner or later you will be before the supreme court of law of Almighty God. You will look at me for seek of testimony, but my friend, there will be no mercy!
 
Hapo sasa ndio tutafaidi matunda ya tasnia ya sheria na tukiuchagua ukawa itakuwa ni heri kwa watanzania
 
Nakumbuka Tundu lisu na mnyika walipambana bungen na hawa wabunge wa ndiyooooo!! Tena hasa askar kupekua bila ridhaa ya mahakama!!
Wakaona wameshinda!!
Haya wakishinda hawa mawakili!!
Hovyoo sana ccm
 
Mwalimu alisema serikali inayozuia uhuru wa kujieleza na ku kusanyika haitufai. Lazima wananchi kuuliza kwa nini mnatuzuia kujieleza na ku kusanyika?Serikali aina hii haitufai haitufai kabisa.
 
Naona wanashetia sasa wameamka nakufanya kazi zinazowapasa. Big up you have done justice to your professional.
 
Itafutwa coz inakinzana na haki za binadamu imejaa uonevu na walio itunga walikurupuka kisiasa tu
 
Back
Top Bottom