Magufuli: Watumishi hewa wamefikia 10,295. Ashusha kiwango cha kodi katika mishahara

anajutia kuwa rais, ww jamaa... sio kwel mengine umechapia nilikuwa makin kwa kideo
 
Usipotoshe watu wewe. Naona huelewi dhana nzima ya uwekezaji katika mifuko ya hifadhi ya jamii. Uwekezaji wowote unatakiwa kuzingatia vigezo vifuatavyo "safety, liquidity, yield, diversification and socio-economic utility".

Hivyo basi kuwekeza kwenye daraja je kunakidhi hivyo vigezo???

Unapowekeza kwenye viwanda basi hizo principles zote zinapatikana na nyongeza kama ifuatavyo:-
1. Ajira zinaongezeka
2. Wanachama wanaongezeka
3. Uchumi unakua kutoka uchumi wa chini kwenda uchumi wa kati
4. Uwekezaji wa aina hii unaweza kufanyika pia katika mfumo wa PPP
5. Kukua kwa soko la mitaji
6. Utafaidisha jamii yote kwa ujumla
7. Standard of living itaongezeka
8. Pengo la umasikini litazidi kupungua
9. Soko la nje kupatikana na hivyo kuleta stability ya shilingi yetu
10. Nk
Kwa kifupi unaweza kuona hayo mambo yote niliyoyataja yanaleta maana ktk dhana nzima ya kazi za Hifadhi ya Jamii ktk nchi yoyote kwa uchache wake.

Kuhusu hilo la mishahara kwanza ulitakiwa ufanye analysis ya kitu kinaitwa "pay gap".

Ulizia hao wakurugenzi wanaolipwa mil 30 au zaidi mfanyakazi wake wa chini analipwa shs ngapi? Wote Wenye mishahara above 15 mil na bado marupurupu ya kufa mtu (mafuta, air time, kulipiwa simu ya TTCL, ada social clubs, ada za watoto shule, magari mapya, yenye kulipiwa ushuru, simu ya bei ghali ya mkononi, outfit allowance, entertainment allowance, maposho ya vikao, magari ya kuhudumia familia, furniture allowance, house allowance, bonus, safari kibao nje na ndani ya nchi nk kutegemea shirika husika).

Ukimaliza hapo fanya analysis ya WAGE GAP kati ya wa juu na wa chini halafu ndio uje kubisha. Mhe Rais ana taarifa zinazojitosheleza kabla ya kufanya maamuzi.

Na kwa taarifa yako wafanyakazi wengi wa kati na chini ambao ni wengi na wale wa Serikali kuu wamefurahia sana uamuzi huo.

Queen Esther

Sioni akiisadia hii nchi
Kushusha mishahara ya maDG wlaiojitoa kwenye mashirika makubwa na kuifanyia nchi kazi, hapo ni kuwatoa kwenye point

Kuwaambia haya mashirika ya mifuko ya jamii kutojenga majengo na kuwekeza kwenye viwanda anaua mifuko bila kujua

Kushusha paye bila kuwaongezea mishahara au kuset kima cha chini ni kosa
 
Mishahara mikubwa ya maofisa ilikuwa "unsustainable" kwa level ya viwango vya uchumi wa Tanzania. Vigezo vilivyokuwa vinatumika kuwazawadia baadhi ya watu mishahara ambayo haiendani na kiwango cha GDP ya Tanzania ukiangalia hali halisi ya utendaji serikalini ni wale waliokuwa wakitokea kwenye sector binafsi. Wapo waliokuwa wakiletwa kutoka nje ya nchi (mfano wa huyo boss wa TIC ambaye aliukataa mshahara na kuishia kujilipa posho kubwa kubwa). Katika mazingira kama haya, ukifanya analysis nzuri ya mambo ya mishahara utaona kuwa kulikuwa na upendeleo ambao kama ungeendelea huko mbele ulikuwa unatupeleka kubaya. Mfano; taasisi A bosi wake kavutwa kutoka nje; kapewa mshahara unaofanana na aliokuwa akilipwa huko nje. Taasisi B bosi wake ni mbongo wa kawaida na mshahara wake ni ule wa kawaida wa kitanzania. Ungewezaje kufanya "justification" ya malipo ya boss huyu wa taasisi A na bosi huyu wa taasisi B kwa kuangalia vigezo vya utendaji? Yaani mtu, kwa kuwa katolewa kwenye ajira Ulaya, unamleta Tanzania na kumlipa mshahara unaolingana na aliokuwa akilipwa kule Ulaya; Je na wasaidizi wake wote utawapandisha walipwe kwa viwango vinavyolingana na nafasi zao kwa huko Ulaya? Hapa tulikuwa tunaiingiza nchi kwenye mgogoro mkubwa sana. Hatimaye yule bosi wa taasisi B naye kesho angedai kulipwa kama bosi wa taasisi A; hivyo viwango tungeweza kuvihimili kwa uchumi wetu?

Watu wanaotetea hii wengi huwa nasikia maneno wanayotumia ni yale yale ya kihisia - utakuwa umemuonea mtu kumpunguzia mshahara. Hoja nyingine huwa ni hawa ni wataalam. Perfomance za taasisi hizo ambazo zinaongozwa na wataalam waliokuwa wakilipwa mishahara ya viwango vya Ulaya mbona haifanani na viwango vya Ulaya? Ukipanga mishahara kwa kutumia hisia matokeo yake ni mabaya mno. Kila nchi mishahara yake inaendana na hali halisi na mfumo wa nchi ile. Ni ngumu sana kumchukua mtu kwenye Private Sector South Africa halafu ukamleta Tanzania kwenye Public sector ukatarajia huyu mtu a "perform kama alivyokuwa aki perform kule". Ikiwa performance yake haiwezi kulingana kumlipa mshahara kama ule aliokuwa akilipwa kule ni kumzawadia fedha ya walipa kodi maskini.
 
"Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, ameutangazia umma wa watanzania kuwa ameshusha kiwango cha kodi inayotozwa kwenye mshahara wa wafanyakazi wa ngazi ya chini (lower bracket) kutoka 11% mpaka 9%. Hili ni punguzo la kihistoria. Najua malengo ya kufanya hivi ni kukidhi haja ya watumishi ya muda mrefu kuwa kiwango cha kodi kishuke kiwe 'single digit', pia kupunguza mzigo wa kodi kwa watumishi na hivyo kuwaongezea kipato chao. Pia ameweka msisitizo kwenye azma yake ya kushusha kiwango cha mshahara wa waliokuwa wanalipwa mishahara mikubwa na kuhakikisha haizidi 15mn - lengo likiwa ni kupunguza 'gap' kati ya walionacho na wasionacho kwenye nchi.



Ukimsikia Rais Magufuli anazungumzia mambo ya kuleta usawa nchini utajua wazi kabisa kuwa 'maneno yake yanatoka kwenye special corner ya moyo wake', maana anayazungumza kwa 'passion' ya hali ya juu sana kiukweli. Kwenye hili, ninamuahidi, kwa dhati kabisa, kumsaidia kutimiza hayo malengo yake kwa nguvu zangu zote, na kwa 'passion' na kasi kama ya kwake. Maana ni katika mambo ninayoyaamini na yaliyonifanya niingie Bungeni kwenye utumishi kwa wananchi, na 'passion' hiyo inatoka moyoni mwangu kabisa. Wakati natangaza nia ya kuomba nipewe ticket ya CCM kuwa mgombea wake wa uRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania niliwahi kusema kuwa 'kizazi chetu cha viongozi kisikubali tuwe na matabaka ya aina mbaya kabisa kwenye nchi yetu: kwamba, tuna kundi moja la watu wengi wanaoamka kila siku asubuhi na kutembea maili 10 kusaka mlo wa siku hiyo, huku tuna kundi lingine linalotafuta walau muda wa kutembea maili 10 ili kukata vitambi vyao!'



Somo kubwa la kujifunza hapa ni kwamba, mfanyakazi hana namna ya kukwepa kodi ya serikali ya PAYE, maana serikali anachukua kodi yake kwanza kabla mfanyakazi hajalipwa mshahara. Tofauti na wafanyabiashara, ambao wanazalisha, kisha wanaanza mambo ya makadirio ya kodi ya serikali. Niliwahi kusoma kitabu cha Robert Kiyosaki, Rich Dad - Poor Dad, anayesema kuwa 'watu wajanja hawawezi kukubali kuajiriwa, maana hawawezi kuwa tayari kukubali kukatwa kiasi kikubwa cha pesa kama kodi, wajanja hujiajiri wenyewe kwa kuwekeza na kuzungusha mitaji kutafuta faida kisha kutafuta kila namna ya kukwepa kodi ya serikali, na hivyo kundi hili la pili huishi maisha ya raha kwa kuwa lina uhakika wa kutajirika.'



Kwa vijana wa nchi yetu wanaohangaika kutafuta ajira siku hata siku wana la kujifunza hapa. Kama wanataka mali, watayapata shambani."
 
Ametaja wafanyakazi hewa ni wa makundi yafuatayo:-
1. Wastaafu ambao wameondoka kabisa kazini lakini bado wako kwenye payroll
2. Wafanyakazi walioajiriwa na Serikali na wakaacha kazi kwa kupata kazi nyingine na wanaendelea kupata mishahara kule walikotoka (double payment)
3. Wafanyakazi walioenda masomoni na wamepitiliza ruhusa ya muda wa masomo kutokana na kozi wanazofanya hasa za muda mrefu. Wamemaliza masomo muda mrefu na hadi sasa hawajarudi vituoni na bado wanachukua mishahara. Kuna wengine wana mpaka miaka 20 nje ya kazi. Hiyo ni shule gani??
4. Kuna wengine ni marehemu na wako kwenye payroll
5. Kuna wengine wako kwenye payroll na hawajawahi kukanyaga hiyo ofisi inayowalipa mshahara
6. Nk

Queen Esther

Hivi hewa ni nini?
 
Nikiangalia mmchanganua wa mwaka uliopita, siku zote hili jambo linawahusu wale wanaopata mshahara chini ya 360,000/ hawa wengine nidanganya toto tu. ukiangalia salary slip unaweza pata ugonjwa wa moyo. nibora salary slip wabakigi nazo tu, nisheeeda
 

Attachments

  • IMG-20160501-WA0004.jpg
    IMG-20160501-WA0004.jpg
    40.6 KB · Views: 99
kigwangala aache unafiki...kigwangala ndio aliomba muongozo wa spika bunge lililopita kupinga wabunge kupunguziwa mafao yao mwaka jana,,,hana uzalendo wowote ni mbinafsi sana...angeanza kwa kukataa posho kama alivyofanya zitto ndio tungemuamini...anachofanya sasa hivi ni kujipendekeza tu...mwanasiasa pekee mzalendo wa nchi hii ni MAGUFULI NA ZITTO KABWE TU
 
Nataka kujua hiyo punguzo la 2% ni kihasi gani? Mwaka Jana walipopunguza kwa 1% mshahara wangu ulipanda kwa Tsh 2000.
 
Back
Top Bottom