Magufuli: Wapinzani wanawaza Ipo Siku Watatawala, Wasahau

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,840
Rais magufuli akihutubia kwenye maadhimisho ya miaka 39 ya CCM amesema "Kama kuna chama kina ndoto ya kutawala nchi hii wafute ndoto hiyo''.

Maana hakuna mtawala anayependa kutawaliwa,ameenda mbali na kusema. Hawa wenzetu wapinzani wanawaza ipo siku watatawala nchi hii wasahau hilo.

Dah nimejiuliza ina maana hata hao wapinzani wakishinda kwenye box waendelee kusahau? Nimeanza kupata picha ya kule visiwani,Pole sana Maalim.

Kuitamka demokrasia ni jambo moja,Kuitekeleza ni jambo jingine-Kagame

Very true na asante sana JPM kwa kuueleza 'ukweli' huu.
Hii ni kwa sababu hiyo NEC hata ikiwa bila Jaji Lubuva daima itaendelea 'kutangaza matokeo kadri inavyoletewa'!
 
Unajua kitu nawashangaa waTz nipale wanapotaka kumtenganisha Magufuli...na CCM ukichukulia Mkutano anaoutumia kusemea hayo mlitegemea angesemaje
 
Kama kila rais atakuwa kama Magufuli
Kweli upinzani hii nchi wataisikilizia tu radioni.
Na hasa kwa wapinzani aina ya kina Kubenea wanaokwenda kuchungulia shanga badala ya kujadili matatizo ya waliowatuma
 
Rais magufuli akihutubia kwenye maadhimisho ya miaka 39 ya CCM amesema "Kama kuna chama kina ndoto ya kutawala nchi hii wafute ndoto hiyo''.

Maana hakuna mtawala anayependa kutawaliwa,ameenda mbali na kusema. Hawa wenzetu wapinzani wanawaza ipo siku watatawala nchi hii wasahau hilo.

Dah nimejiuliza ina maana hata hao wapinzani wakishinda kwenye box waendelee kusahau? Nimeanza kupata picha ya kule visiwani,Pole sana Maalim.
Kuitamka demokrasia ni jambo moja,Kuitekeleza ni jambo jingine-Kagame
 
Sasa si mfute tu vyama vingi mbaki wenyewe?
Kule zanzibar mmeachiwa nchi na cuf na bado mnalia lia badala ya kufurahia ushindi wa mezani.

Hapana, haujaelewa, vyama haviwezi kufutwa kwa sababu vyama vipo kwa ajili ya kuikumbusha Serikali kama ikijisahau, kama ilivyotokea kipindi hiki na sasa Serikali imeamka na matokeo yanaanza kuonekana, hivyo hivi vyama ni lazima viwepo kwa ajili hiyo na hilo hata wenye vyama kama akina Mbowe, Mtei & Co. wanalijua, wanaweza wakashika Miji wakaongoza baadhi ya Halmashauri hapo sawa lkn

Siyo Kuongoza TanZania, hilo ni NOPE!
 
Mtoa mada huna tofauti na wale wanaotafsili lile fungu la biblia ya kwamba kila kiingiacho tumbon si najisi bali kitokacho huku wakitaka kuhalalisha vyakula vyote bila kusahau mbele kuna ujumbe gani...

Kwan ungesikiliza hadi mwisho au mwanzo wa hiyo sentence na ukaleta ujumbe ulivyo ungepungukiwa na nini?!
 
Back
Top Bottom