Magufuli mtake Samwel Sitta aondoke kwenye Jumba la Spika Masaki

Wakati serikali inawavunjia wananchi wanyonge nyumba zao, viongozi wanakaa kwenye nyumba walizokuwa hawa deserve kukaa. Na ni mtu ambaye alikuwa anakiongoza chombo cha kutunga sheria. Tunategemea haki gani itendeke kutoka kwa mtu kama huyu? Uroho huu wa kujilumbikizia mali na huduma zisizo halali kweli zina kikomo?

Mkuu linapokuja swala la kuwavunjia/kuwaondoa walala hoi hakuna mjadara ila kwa makada wa chama inaku ni mchakato mreefu.mzee sita ni kauzu sana wasipo mtoa kwa nguvu hataondoka hapo milele
 
Huyo anatakiwa mahakamani aeleze Loliondo iliuzwa kwa taratibu zipi jambo ambalo haliwezi kufanyika chini ya utawala wa ccm. Ndiyo maana wengine tulipigana sana ccm iondoke madarakani lakini ndoto na matumainin yetu vikayeyushwa na fisadi mbowe na genge lake.

Ndio maana Nyerere baada ya kifo cha azimio la Arusha alikiri kabisa kulisemea jambo hili ni lazima uwe na kichwa cha mwendawazimu
Vivyo hivyo kwa hili la Loliondo
N ndio maana kumbukumbu zangu za watu waadilifu zilishia kwa Mwl Nyerere na Sokoine
 
Kuna wakati nilisikia nyumba hiyo haikuwa ya serikali bali ilipangishwa. Labda serikali ije na habari kuwa SS sasa analipa mwenyewe
 
Kapanga na analipa kodi.

Kuna wakati nilisikia nyumba hiyo haikuwa ya serikali bali ilipangishwa. Labda serikali ije na habari kuwa SS sasa analipa mwenyewe

Wakuu hivi ile serikali ya JK kuna kitu ambacho hakiwezekani ?? Inaweza ikawa Nyumba ni ya serikali ila wameamua kusema imepangishwa au wamemuuzia Sitta

Hivi lile la Prof Costa Mahalu na Jumba la ubalozi Italy ilikuaje
 
Lakini Tanzania haishi vichekesho vikao vya bunge ni Dodoma ,nyumba ya spika ipo Dar Es Salaam ambako hakuendeshwi vikao vya bunge,kwa hiyo Spika anakaa Dar kufanya kazi Dodoma,kwanini nyumba ya spika isiwe Dodoma na spika akae Dodoma ?,akija Dar aje matembezi tu ya kupunga upepo wa bahari ya Hindi?
Dar kuna ofisi ndogo ya bunge,hivyo spika anapokuwa dar hatarajiwi kulala gesti
 
Hata Dodoma pia kuna nyumba ya Spika
 
Dar kuna ofisi ndogo ya bunge,hivyo spika anapokuwa dar hatarajiwi kulala gesti
Kwanini Dar kuwe na ofisi ndogo ya spika?kwani ofisi ya spika imekuwa kama wakala wa serikali kuwa na ofisi ndogo za kikanda?hiyo ofisi haina tija bali ni ufujaji wa pesa tu na ujiulize hiyo ofisi ndogo inatumiwa mara ngapi na je shughuli zake zinazidi shughuli za ofisi kuu kule Dodoma?kama hapana basi huo ni ujinga huwezi ukawa na kasiri halafu unatumia mara 4 kwa mwaka vinginevyo utuambie spika anakaa Dar Es Salaam badala ya Dodoma
 
Hata Dodoma pia kuna nyumba ya Spika
Huo ni ufujaji wa fedha yetu spika makazi yake ni Dodoma kwanini hata Dar awe na hekalu si afadhali akija Dar akae hotelini kwa hizo siku 7 atakuwa ameokoa kodi ya hilo hekalu kwa miezi 12.
 
Asante mkuu ni kweli Huyu mzee wa busara nyingi nimemsahau
humjui au ulikuwa mdogo mzee ruksa anamiliki mtaa pale msasani karibu na kwa warioba ana ghorofa posta ,mkewe ni miongoni mwamamilionea wanawake wa nchi hii
 
Sitta anaanza kumponda magufuli bila hata heshima. Kwanini asimtafute badala ya kumuongelea ovyo kwenye vyombo vya habari? Anamdharau magufuli
 
Samuel ni uadilifu upi ulionao kama hadi leo unaishi nyumba ya spika ? Jitathmini mzee wangu .

Yaani Makinda kapiga miaka mitano ya uspika bado Sitta kushikilia nyumba?

Majembe Auction and Court Brookers wakamng'oe bila ajizi.
 
humjui au ulikuwa mdogo mzee ruksa anamiliki mtaa pale msasani karibu na kwa warioba ana ghorofa posta ,mkewe ni miongoni mwamamilionea wanawake wa nchi hii

Mkuu ni kweli unayo yasema ila kama umenielewa vizuri nimetabainisha kwamba ni mzee wa busara nyingi na kuna tofauti kati ya busara na uadilifu ,na kwa makusudi kabisa nilimjibu mdau mmoja kuwa kukumbukumbu zangu za wana ccm waadilifu zinaishia kwa Mwl Nyerere na Sokoine
Ni kweli mimi sikuwahi kushuhudia utawala wa Nyerere na Sokoine nimehadithiwa tu
 
Sitta anaanza kumponda magufuli bila hata heshima. Kwanini asimtafute badala ya kumuongelea ovyo kwenye vyombo vya habari? Anamdharau magufuli

Anatunisha misuli kama kawaida yake ngoja tuone Magufuli atafanya nini
 
Huyo aliasisi ufisadi, yaani tayari umesahau au ulikuwa hujazaliwa?
Hili genge la haya yote yanayojiita marais wastaafu kama tungekuwa na utawala wa haki yangekuwa jela, lakini tutalazimika kuyatunza mpaka yafe na mengine ndiyo hayo yana miaka zaidi ya 90 lakini bado yanadunda.
 
Kengine ndio kana miaka 59 .dadeki
 
Back
Top Bottom