Magufuli msikilize huyu Mzungu!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,786
Ningemshauri Raisi Magufuli kwa kuwa ameonyesha nia ya dhati ya kuinua Uchumi wetu kwa kuongeza uzalishaji amsikilize huyu Mzungu kwenye hiyo video ambaye anamiliki shamba la maua Arusha, ameajiri WatanZania mia nane (800 ) kwa hesabu ya haraka haraka kama kila mwajiriwa anahudumia familia ya watu 4 ina maana WatanZania 3200 wanategema kufanikiwa kwa hili shamba, hivyo msikilize malalamiko yake ikiwezekana muite Ikulu muongee ana kwa ana ili muangalie ni jinsi gani mnaweza kumuondolea vikwazo ambavyo vinapunguza uzalishaji wa maua!

Kwani kulingana na maelezo yake kama vikwazo vikiondolewa au kupunguza ana uwezo wa kuzalisha zaidi na kuajiri Watu wetu wengi zaidi na hiyo ni win win situation kwani itaongeza mapato serikali kwa kuuza kuingiza fedha za kigeni kutokana na export!

Last edited by a moderator:
Hiyo hesabu siyo mkuu ..siku hizi watu wako irresponsible hakuna tena na usishangae kuambiwa hao wote ni familyless ..yaani wapo wapo tu, familia isikie tu.
 
Mzungu anataka fursa sijui magufuli wataelewana katika lugha.

swissme
 
Hawa watu wa maua wanawalipa wafanyakazi sh laki moja.

Mazingira ya kazi ni sumu tupu.

Kama ni hizi kampuni hapa arusha muulizeni kwa nini maua yanapitia Nairobi kuwekwa label ya kenya?
 
mkuu huwafahamu tu hao wazungu wa maua, wafanyakazi wanafanya kazi katika mazingira hatarishi sana na mshahara ni kidogo mno, usipumbazwe na maneno yao matupu nenda mwenyewe kaone hali ya wafanyakazi wa maua Arusha inatisha mkuu, hao si wa kuwahurumia ni wanyonyaji.
 
Hawa watu wa maua wanawalipa wafanyakazi sh laki moja.

Mazingira ya kazi ni sumu tupu.

Kama ni hizi kampuni hapa arusha muulizeni kwa nini maua yanapitia Nairobi kuwekwa label ya kenya?
kama utapata watu wa kwenda pokea hiyo laki 1 ujue wanaihitaji.... ni juu ya serikali sasa kuhakikisha watu wake wanafanya kazi kwenye mazingira mazuri na salama, wanalipwa angalau si chini ya kima cha chini na wafanyakazi kuunda vyama vyao, mwekezaji angependa hata hiyo laki 1 asilipe...
 
Ingawa mazingira ya ufanyaji kazi katika mashamba haya ya maua ni hatarishi, ni kweli yanaajiri watu wengi sana, mishahara midogo ni kweli lakini kuna watu wanatafuta hizo nafasi hawazioni.. hii inamaanisha kuwa kuna tatizo kubwa la ajira katika nchi yetu.. serikali iweke mazingira rafiki kwa kila mtu, mfanyakazi na muwekezaji (win win situation). Pia tupunguze kodi za viwanja vya ndege ili maua yasiendelee kupitia Nairobi maana landing fee zetu zinatisha sana ni vigumu sana ndege nyingi kuja kutua KIA. Its all about mipango mizuri i hope JPM na serikali yake watalifanyia kazi na hili!
 
Yaani, kwa vile ni Mzungu ndio lazima akutane na Rais; haya mambo yanahusiana na Wizara ya Kilimo au chombo cha kulobby kuhusu masuala ya kilimo ndio kiwakilishe. Kama kila mtu mwenye matatizo na mawazo akitaka kwenda Ikulu kukutana na RAis ili matatizo yake yatatuliwe tutaanza kurudi kule kule kwa kwenda kupokea baskeli Ikulu!
 
Si swala la kusikilizwa mzungu tuu ni kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji na kuondoa ukiritimba serikalini kwa wawekezaji wazawa pia..hao wazungu hawaji na mitaji hapa ila wanafanikiwa katika biashara zao wazawa wenye mitaji wanafeli kwa kuwa na ukiritimba mkubwa..
 
Watu wanakufwa polipoli shauri ya chemicali hatarishi. wanapewa mshahara wa house gili au bamaide.Kilimo kinakausha maji bonde la Pangani - surface and underground water huko tunakosa umeme. JPM ni mtaalam analijua.
 
Yaani, kwa vile ni Mzungu ndio lazima akutane na Rais; haya mambo yanahusiana na Wizara ya Kilimo au chombo cha kulobby kuhusu masuala ya kilimo ndio kiwakilishe. Kama kila mtu mwenye matatizo na mawazo akitaka kwenda Ikulu kukutana na RAis ili matatizo yake yatatuliwe tutaanza kurudi kule kule kwa kwenda kupokea baskeli Ikulu!

Sisi Waafrika tuna safari ndefu sana kuendelea na tatizo kubwa ni kwamba hatuelewi jinsi capitalist economic system inavyofanya kazi na cha kusikitisha na kukatisha tamaa zaidi unakuta watu ambao hawaelewi capitalist economic system wanaishi Ulaya, Marekani au Japani kwa zaidi ya miaka 20!

Wewe unabeza kwamba hili jambo siyo muhimu na halipaswi kushughulikiwa na Raisi wa nchi, nchi kama Marekani kama kuna kiwanda kinafilisika na watu hamsini (50) tu wanapoteza kazi Raisi wa Marekani huwa anaongea na hawa ni watu 50 TU kwenye nchi ambayo unemployment rate iko chini ya 10% sasa ni ajabu sana kwenye nchi kama TanZania ambayo unemployment rate ni zaidi ya 80% nikimaanisha watu ambao wameajiriwa na kulipa Kodi (PAYE) na NSSF unaona kwamba mtu aliyeajiri watu 800 hana umuhimu wa kukutana na Raisi nchi? Hakuna kaya ambayo kuna mtu hatafuti TanZania!

Tanzania ina trade deficit kubwa sana yaani tunachoexport ni kidogo sana kulinganisha na import kwa kifupi hakuna tunacho export ukiachia chai na kahawa na hii nchi yenye watu zaidi ya milioni 40 leo kuna mtu mwenye soko la Uhakika kuexport Maua Ulaya ana matatizo ambayo yanaweza kutatulika unaona hakuna haja ya yeye kukutana na Raisi wa nchi?

Nchi yetu ina export kwa mwaka 5.5 bilion US dollars tuna IMPORT 11.5 bilion dollars hiyo trade deficit ni kubwa sana yaani tuna import mara mbili zaid ya tunavyo export halafu kuna Mtu ambaye anaajiri watu 800 ana soko la uhakika Ulaya unampuuzia kwamba anaweza tu kukutana Waziri kilimo sasa Waziri wa kilimo anahusika nini na upatikanaji wa umeme au tax system ya nchi?
Halafu tunalalamika kwamba hata tooth picks zinatoka Uchina unafikiri ni kwa nini Uchina wanaweza kuexport toothpicks TanZania?

Siasa haziwezi kututoa hapa mambo ya kudakia sijui katiba bill of rights na upuuzi mwingine wa Marekani hauwezi kuendeleza Afrika hata kwa miaka 500 ijayo, hata mkichukuwa Katiba ya Marekani kama ilivyo hakuna kitu kitafanyika na bado miaka 50 baadaye tutakuwa hapa hapa kama siyo nyuma zaidi, kwa maana tatizo letu Afrika ni sisi Waafrika na siyo Mfumo tunaoutumia!
 
Salute
 
Yaani, kwa vile ni Mzungu ndio lazima akutane na Rais; haya mambo yanahusiana na Wizara ya Kilimo au chombo cha kulobby kuhusu masuala ya kilimo ndio kiwakilishe. Kama kila mtu mwenye matatizo na mawazo akitaka kwenda Ikulu kukutana na RAis ili matatizo yake yatatuliwe tutaanza kurudi kule kule kwa kwenda kupokea baskeli Ikulu!

Si ndiyo Mfumo wa Chama ?
Unashangaa nini ?
 
Huyo mpigaji tu! Akalipe Kodi hayutaki tena misaada tunajitegemea. Kulalamika tu lskini biashara hawaachi
 
Kama ni mwekezaji asiyetuibia na anaetoa ajira,ni vema ukiritimba ukaondolewa kwa wawekezaji.

Ajaira ya Mshahra 100,000/= kwa mwezi huku watuw etu wakifa kwa sumu?

Jamaa nazungumzia Foreign Currency, sijuhi ni mimi au ndivyo ulivyo, mfano huyu ni muolanzi maua anauzia uholanzi huku ataleta rwa material na hela chacche za kuendesha shamba, faida yote itaishia hukohuko, hakuna dola inayokuja huku tusiongopeane.
 
Yaani, kwa vile ni Mzungu ndio lazima akutane na Rais; haya mambo yanahusiana na Wizara ya Kilimo au chombo cha kulobby kuhusu masuala ya kilimo ndio kiwakilishe. Kama kila mtu mwenye matatizo na mawazo akitaka kwenda Ikulu kukutana na RAis ili matatizo yake yatatuliwe tutaanza kurudi kule kule kwa kwenda kupokea baskeli Ikulu!

Mimi huwa nashindwa kuelewa hivi Marekani nako huwa yanaishi mataahira? Nani aliyaruhusu haya mataahira kuingia nchi za watu? Wakati wa JK mlikuwa mkishangilia yakienda yale mazungu yenye kuficha jicho moja, sasa huyu anataka afikishe Ujumbe moja kwa moja kwa rais mnaanza kubeza!
 
Yaani, kwa vile ni Mzungu ndio lazima akutane na Rais; haya mambo yanahusiana na Wizara ya Kilimo au chombo cha kulobby kuhusu masuala ya kilimo ndio kiwakilishe. Kama kila mtu mwenye matatizo na mawazo akitaka kwenda Ikulu kukutana na RAis ili matatizo yake yatatuliwe tutaanza kurudi kule kule kwa kwenda kupokea baskeli Ikulu!

Naona wanakimbilia kilimo cha maua, wakati kuna vilimo vingi ambavyo vinalisha Nchi na kukimu wakulima wetu... Watu wanataka Mzungu asikilizwe! Tena anayeua watu kwa sumu na kukausha maji ya bonde la mto...
 
Back
Top Bottom