Magufuli augua ghafla, alazwa

Status
Not open for further replies.
Apone haraka awahi changuzi zingine kutoa ahadi za kujenga madaraja!
 
Habari tulizozipata punde zinadai kuwa Waziri wa Ujenzi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli amezidiwa ghafla na kukimbizwa hospitalini huku Dodoma ambapo bunge la tisa linaendelea.

Kwa mujibu wa Naibu Spika, Job Ndugai Dk. Magufuli alikumbwa na homa ya ghafla ambapo baada ya kukimbizwa General Hospital, Dodoma, ilibainika kuwa presha yake ilikuwa juu na ana kichomi upande wa kushoto wa mbavu zake.

Mpekuzi blog
 
Ofisi ya Bunge inafanya taratibu za kumpeleka Apolo India kwa uchunguzi zaidi! ooooops!Sorry
 
Get well soon Hon.
Hivi wale anti-corruption kwenye weight bridge zote wameshaanza kazi?
Nilisikia wangeanza wiki hii..
 
R.I.D
means Rest In DODOMA,
HOPE WAKAZ WENG WA KANDOKANDO MWA BARABARA HASA WALIO NDANI YA ROAD RESERVE WANAIFATILIA AFYA YAKO KWA UKARIBU.
 
Tunamwombea apone haraka na aendelee na kazi asihofu chochote kwani kila kitu kwake kinawezekana. Lakini ni muhimu kujua/kuwa na taarifa ;Wengi wanapenda kuwafutilia watu hata pale ambapo haina umuhimu wowote
Je kuna nini kwa yeye kuugua? Je ni punda asiyeugua?
Kama mpenzi wako bora useme sioni ulazima wa wewe kumfuatilia kiasi hicho
Na nadharia mmoja imezoeleka na mnaona kila anayeugua basi kuna mtu/watu wamemzuru kwa kumziba je hali hii itaisha lini? Maana watu sasa wanapenda kuoanisha kila kitu na uchafu unaoendelea nchini
Kila kitu mafisadi hata wawe mafisadi mtapata dhambi bure kuwazania kila mara ni wao wamesababisha kuumwa
Hata mtu akila chakula cha hovyo mtaani na akawa anaharisha mtasema mafisadi!
Angalia sana maswali unayouliza na kupelekea watu kuendeleza dhana na kisha kudumaza mawazo ya wanajamii na kisha kukwaza maendeleo yao na kujenga woga katika maamuzi ya maendeleo
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom