Magufuli: Kuna watu walidhani nitashirikiana na majizi, wamekwama

Binafsi UKAWA damu ila mpaka hapa alipo Mh Rais Maghufuli nakubaliananae, ikiwa mwendo ni huu basi kuna siku tutapata wote keki ya mama Tanzania.
MIMI na dhani Lowassa ndio katufukisha hapa, bila yeye tungekua matajiri, Angalia Lowassa ndio huyo huyo kwney Escrow, Huyo Huyo kwnye IPtl, huyo huyo katuficha mikataba ya gesi, Lowassa huyo huo katuachia nchi ikiwa taabani ,Lowasa huyu huyu kaaweka wau wale wamitafuna nchi vilivyo , CCM wamejitahidi sana kakweli , ila Nguvu ya Lowasa ni kubw aalikau ana wazuia CCM wana shindwa kutumbua majipu mimi na dhani Ukawa hawajielewi mana Lowasa ndio pekee jipu .HIi nchi Bila Lowasa tungekua tunaishi kwa mziwa na asali .
 
Bado CDM neo maana wanapinga juhudi ,zake kwani wnajua zitawafikia walipo...

Kweli kabia hawa CHadema wameharibu nchi yani Lowassa katuhribia sana, Kil adili yumo. Lugumi, IptL,Escrow, Mikataba tusio ijua ya gezi, madini , yani kaweza watu wanao msupport badi wame itafuna nchi mbaka masikini JK ana maliza yani nchi ikiwa tabani , yani Lowasa jipu kuu, huyo ndio tatiz kubwa
 
Hivi magufuli mbali na kutumbua majipu , vision yake kwenye uchumi wetu ni nini. Mana asijisahau akawa anatumbua majipu hadi 2020 akashindwa kuijenga nchi.

Ni kujenga viwanda ili nchi ijitegemee kiuchumi....ili kufikia hapo ni lazima nchi isiwe na majizi hivyo hii tumbua tumbua ni salam kwa wezi wote wa mali za umma na yeye Rais kama msimamizi mkuu kwa niaba yetu analojukumu la kuhakikisha hizo rasilimali zinatunufaisha wote kiuchumi......kama hujamuelewa mpaka sasa hivi ni kwa sababu hujataka tu kumuelewa...
 
MIMI na dhani Lowassa ndio katufukisha hapa, bila yeye tungekua matajiri, Angalia Lowassa ndio huyo huyo kwney Escrow, Huyo Huyo kwnye IPtl, huyo huyo katuficha mikataba ya gesi, Lowassa huyo huo katuachia nchi ikiwa taabani ,Lowasa huyu huyu kaaweka wau wale wamitafuna nchi vilivyo , CCM wamejitahidi sana kakweli , ila Nguvu ya Lowasa ni kubw aalikau ana wazuia CCM wana shindwa kutumbua majipu mimi na dhani Ukawa hawajielewi mana Lowasa ndio pekee jipu .HIi nchi Bila Lowasa tungekua tunaishi kwa mziwa na asali .

Simple mind discuss Peole, Average mind discuss events and Great mind discuss Issues.

Wewe ni Simple mind= maana yake wewe akili zako ndogo sana....hebu ziongezeongeze
 
Tabaka la mrengo wa kushoto halitaki kabisa kusikia kauli hizo zinazotolewa na mheshimiwa rais
 
Simple mind discuss Peole, Average mind discuss events and Great mind discuss Issues.

Wewe ni Simple mind= maana yake wewe akili zako ndogo sana....hebu ziongezeongeze

Simple mind ndio ni nani?Huyo Sija wahi Msikia , alifanya nini kwnye ufisadi sababu mafisadi nao wajua ni LOwassa huyo Simple Mind ndio yuko kwnye gesi u Lugumi? naomba jibu tafadhali asante ?
 
Nimejuuliza sana hii issue aliyosema mweshimiwa Rais " Kuna watu walidhani nitashirikiana na majizi, wamekwama" amesema haya baada ya kutoka kwenye kikao cha chama. Inaoneka kunashinikizo alilopewa kushikiriana na wezi wanayoifathili CCM. Na hao wezi wametia ngumu kutoa hela kusaidia mkutano utakao mwenzesha kuchukua Uwenyekiti.
Naona CCM kama kweli inahitaji hela ipitishe mchango ndani ya wanachama wake wa kawaida ili JMP hapewe uwenyekiti wa CCM na tuachane na hawa wanaojiita wafathali uchawara.
 
Tanzania ilikusubiri mno ndugu yetu JPM. Sasa tumekupata. Huna mfano wako. Nchi ilikuwa ya kimadilimadili ya kupiga pesa na ufisadi wa kutisha. Kifupi, nchi imeporomoka mno. Karibu tuirudishe nchi mstarini. Ikiwezekana acha hata chama chetu kiisome namba! Ukitaka kumuua nyani usimwangalie usoni.
 
Hivi magufuli mbali na kutumbua majipu , vision yake kwenye uchumi wetu ni nini. Mana asijisahau akawa anatumbua majipu hadi 2020 akashindwa kuijenga nchi.

Nimecheka sana...unaweza kuwa na point comrade, lakini utumbuaji majibu ni sehemu ya kuijenga nchi...ameshasema mwenyewe kuwa anataka Tanzania kuwa ya viwanda, bila shaka ipo mikakati...reli ya kati iliyopangwa kujengwa ni sehemu ya ujenzi wa nchi kwani itafungua milango ya biashara kwa kasi zaidi na nchi za jirani na sisi wenyewe...lakini sisi wenyewe wananchi inabidi tuwe mstari wa mbele kuijenga nchi yetu, kwa kutekeleza wajibu wetu kila mahali tulipo...tufanye kazi kwa kudumisha nidhamu ya maisha, tubane matumizi, tufanye kazi kwa bidii mahali tulipo...kama wewe ni mfanyakazi unafanya kazi kwa bidii, kama ni mkulima unafanya kazi kwa bidii, kama ni askari unafanya kazi kwa bidii na kadhalika na kadhalika...ukiwa nje ya familia yako na umeenda kupata moja baridi na moja moto unaagiza kongoro na supu ya kuku na mchemsho wa samaki, jiulize wewe unakula hivyo je familia yako nyumbani mke/mume na watoto wako umewaachaje? je, nao wanakula hiyo supu na mchemsho? Kwa hiyo mindset yetu has to change yaani tubadilishe fikra zetu kwa maendeleo ya familia na nchi au jamii kwa ujumla.
 
Wakati akiongea na wananchi wa Jiji la Arusha kwa maelfu ambao walimsimamisha kwa nguvu ili asikilize kero zao, Rais Magufuli amesema kuna baadhi ya watu walidhani atashirikiana na majizi nchini, lakini kwa sasa wamekwama na atahakikisha anatumbua majizi yote ili nchi iwe kwa faida ya Watanzania wote na iweze kwenda mbele kwa haraka zaidi.

''Kuna majizi yalianza mpaka kuuza nyani na kama nyani wangemalizika, hata sisi tungeuzwa'' Alisema Rais Magufuli.

Aliendelea kusema, ''Uchaguzi umeisha na kinachotakiwa kwa sasa mshikamane kwa pamoja ili tuyatumbue haya majipu kwa nguvu zote. Ninasema, tutayatumbua kweli kweli''.

''Sitangalia unatoka chama gani, uwe CHADEMA, CCM, CUF au huna chama, tutakutumbua tu kama wewe ni jizi. Tunachotaka ni Tanzania yetu iende mbele zaidi'', Alisema.

Alimaliza kwa kusema, ''Haya majizi yamefaidi sana jasho la Watanzania, haitawezekana na haitawezekana waendelee kuiba''.

VIDEO:

Kazi na Dawa
 
Hivi magufuli mbali na kutumbua majipu , vision yake kwenye uchumi wetu ni nini. Mana asijisahau akawa anatumbua majipu hadi 2020 akashindwa kuijenga nchi.
kamanda kama mpaka leo hujamwelewa Magufuli basi kaa na familia yako mchape kazi. usitafute mchawi. mambo ya siasa achana nayo. kama mkulima nenda kalime kwa bidii. kama mfanyakazi chapa kazi kwa bidii na kama mfanya biashara fanya biashara halali na ulipe kodi forodhani.usikwepe kodi. timiza wajibu wako kwa uaminifu. ukifanya haya tutaelewana
 
Unachokisema hakifanani na falsafa ya CCM na wana CCM waliodai kwamba kila wanachosema wapinzani ni uongo kuwa wanaropoka na kueneza uongo usiokuwa na maana. unaposema kwamba mnakijenga chama upya unataka kuniambia ni lini mlikubali chama kilikuwa kibovu na kuwaibia wananchi? ni lini mmewahi kusema kwamba hoja za wapinzani zilikuwa sahihi walipodai kuwa CCM inashirikiana na wafanya biashara kuibia nchi..leo unapotuhumu Lissu na Msigwa kwamba wanatetea wezi hao wezi unaowaita wezi wametoka wapi wakati siku zote mlisema siyo wezi ni uongo wa wapinzani? hao wezi ni pamoja na huyo Rais wenu aliyeuza nchi kwa hao mabepari? Nakuhakikishia kama Magufuli anataka kusafisha chama na kukisuka upya basi aamini kwamba kiakwenda kupasuka ktkt au ajitoe kafara maana hao ccm siyo watu wa kawaida walishanogewa na ukatili la sivyo atarajie kunyimwa uenyekiti

Khaa wew jamaa eti kitapasuka ,lini hiyo mkuu amna tena wa kutingisha kibiriti leo hii wanasisiem wanajisikia fahaari kukupita sehem yoyote na jezi ya kijani , kama kimepita salama 2015 unategemea kwa sasa ndo kipasuke ,ccm chini ya magufuli itakuwa imara kuliko wakati mweingine wowote na hivi karibuni tutaanza kuwapokea wanachama wenu mliowaaminisha kuwa mnapigania wanyonge kumbe ni unafiki mtupu

kusubiri ccm ipasuke ni sawana kusubiri jua litokea mmagharibi kuelekeamashariki
 
Sasa ndiyo nagundua kwanini watu wanagoma kumpa uenyekiti wa chama
Ni kutapatapa kwa mfa maji! Ni woga na jambajamba nyingi, watabana sana lakini mwisho wake wataachia pwaaa! na watatumbuliwa tu.
 
Tatizo la huyu jamaa ni KUKURUPUKA tu kama alivyokurupuka kwenye issue ya sukari...vinginevyo ni mtu mzuri kwa sababu hamwonei mtu aibu. Mshaurini aachane na tabia ya kukurupuka kama digidigi aliyeona chuì mbugani.
 
naaona unaona raha kuuziwa sukari sh 2500 kilo. au wewe ni mlanaguaji wa sukari. ungeeleza kwa mifano na tafiti kidogo ungeeleweka sana. tupe data kuthibitidha usemi wako. vinginevyo tutajua una maslahi binafsi na hawa wafanyabiashara wahuni na wezi nadhani wewe ndio umekurupuka. utakuwa umeamka nazo.
 
Hivi woga Wa kutoonesha bunge unatokana na mini,wakati wananchi wanamuunga mkono Magufuli?
 
Magu ana hatari ya kupata pressure akiwa madarakani na kama teyari anayo,basi awe makini hii miaka mitano naiona ni mingi sana kwake.

Matamshi haya ya Magu yamfikie JK popote alipo iwe ni huko Kenya,Dar-es-salaam au msoga.
Unasheria,unavyombo vya usalama pressure ya nini?, ngojeni muone sinema ,namkumbuka mfalme Wa Ufaransa ambaye alidhibiti vyombo vya habari,akilala sherehe,akitamka sherehe,akionja sherehe alitumia mwanya huo kuzuia utawala bora Bali yeye tu. Watu walitumwa kila kona kufuatilia kile ambacho wananchi wanampinga ili wakamatwe na kutoswa

Stay turned
 
Wakati akiongea na wananchi wa Jiji la Arusha kwa maelfu ambao walimsimamisha kwa nguvu ili asikilize kero zao, Rais Magufuli amesema kuna baadhi ya watu walidhani atashirikiana na majizi nchini, lakini kwa sasa wamekwama na atahakikisha anatumbua majizi yote ili nchi iwe kwa faida ya Watanzania wote na iweze kwenda mbele kwa haraka zaidi.

''Kuna majizi yalianza mpaka kuuza nyani na kama nyani wangemalizika, hata sisi tungeuzwa'' Alisema Rais Magufuli.

Aliendelea kusema, ''Uchaguzi umeisha na kinachotakiwa kwa sasa mshikamane kwa pamoja ili tuyatumbue haya majipu kwa nguvu zote. Ninasema, tutayatumbua kweli kweli''.

''Sitangalia unatoka chama gani, uwe CHADEMA, CCM, CUF au huna chama, tutakutumbua tu kama wewe ni jizi. Tunachotaka ni Tanzania yetu iende mbele zaidi'', Alisema.

Alimaliza kwa kusema, ''Haya majizi yamefaidi sana jasho la Watanzania, haitawezekana na haitawezekana waendelee kuiba''.

VIDEO:
Mbona anashikiana na wakina kikwete na madabida na mkapa? Au hajui hao ni wezi? Aache usanii yupo busy kuziba pengo la kanumba badala ya kuleta mpango kazi
 
Back
Top Bottom