Magufuli amewaumiza watumishi wa umma!

Naendelea kusisitiza kwamba hiki kimbunga cha 'HAPA KAZI TU' kitapeleka maafa makubwa kwa watumishi mumiani na wazembe.Hiki kimbunga licha ya kuvuma kwa kasi kubwa ya kung'oa magugu,pia kina joto kali linalochoma vibaya,kwa hiyo kimbunga kisipong'oa basi kitachoma.
 
Huo ni uongo walim walivyo na shida ....kama wangekuwa wana neemeka na dawa wasingekuwa hivyo
 
We unadhani hata sitting allowance ikifutwa wabunge watafurahi?

Magufuli ana kazi sana@huo ndo uhalisia wa mambo,mwanadamu anaangalia kwanza interest zake rais anataka kubadili mambo ili watu kwa ujumla wanufaike ni kaazi sana

Kazi anayo Mr Prezo but amechaguliwa kufanya kazi muache afanye kazi.
 
Kuna mzungu aliwahi kunitania akisema Tanzania kwa posho ni kiboko. kuna:

Sitting allowance,
Sleeping allowance
Standing allowance
Running allowance
Walking allowance
Travelling allowance
Meeting allowance
Night allowance,
Disturbance allowance,
Leave allowance,
Maternity leave allowance, etc
 
Sijawahi kuona kujikomba kwa kiwango hiki cha unafiki na uzandiki kwa hiyo unawashtaki watumishi wa umma kwa wananchi huku ni kujikomba kwa kiwango cha degree ya kwanza!@#@^$*&*!
 
Kuna mzungu aliwahi kunitania akisema Tanzania kwa posho ni kiboko. kuna:

Sitting allowance,
Sleeping allowance
Standing allowance
Running allowance
Walking allowance
Travelling allowance
Meeting allowance
Sio uongo mkuu. zipo hizo allowance.
Kuna wafanyakazi serikalini kutwa kuchwa ni kwenye mikutano na wanalipwa allowance.
Kama hakuna allowance hawaendi.
Na hapo zinatoka allowance za wapiga picha, waandishi wa habari, vitafunio,kukodi ukumbi, mtoa mada(na allowance yake), muwezeshaji-you name it.
Nchi hii inabidi Magufuli afanye kama alivyofanya Mkapa, punguza wafanyakazi wawe wale barely minimum , ili waliobaki walipwe vizuri na wafanye kazi.
 
Pombe ajue kuwa wanaotekeleza maagizo yake wakiwa na njaa watamuhujumu tu, ni vema akawatengenezea maslahi bora yaliyo halali, la sivyo watamuangusha.
 
Wakuu, niko Rachel bar Moshibar .- Ukonga. Pembeni yangu kuna watu watano wanapata bia. Katika hali ya kustaajabisha namsikia jamaa mmoja akilaani kitendo cha mh. rais kufuta sherehe za uhuru. Anaelezea jinsi gani rais anavyojijengea chuki na watumishi wa umma. Jamaa anahitimisha kwa kutolea mfano yeye akiwa daktari kwenye sherehe za uhuru hutoka na shilingi laki tatu. Anajiapiza kuwa Magufuli atarogwa kwa sababu hii ya kuwanyima ulaji.

Baada ya kuyasikia haya nasema moyoni mwangu, bado safari ni ndefu sana kufikia mageuzi ya kweli. Juzi nilimsikia mama mmoja akilalamika kuwa mwalimu mkuu (shule hakutaja ) alimwambia wazi wazi kwamba kitendo cha kuondoa michango na tuition mashuleni hakikubaliki. Kwamba walimu hawajafurahi hata kidogo, kisha akamwahidi mama huyo kuwa baada ya miezi sita mtakuja kutupigia magoti mkiomba tuition.

Hivi watanzania tumekuwaje hasa!? Unataka nini? Mbona inavyoonekana "wasomi" ndio wanageuka kikwazo kwa mabadiliko chanya? Kundi la wasomi limegeuka kuwa wapigania maslahi binafsi. Tutafika kweli!!?

Mungu mtie nguvu rais wetu, tuko pamoja naye. Amina

Wasomi gani hao wanaopinga mabadiliko? Hebu mwaga majina yao hapa tuwajue.
 
We unadhani hata sitting allowance ikifutwa wabunge watafurahi?

Magufuli ana kazi sana@huo ndo uhalisia wa mambo,mwanadamu anaangalia kwanza interest zake rais anataka kubadili mambo ili watu kwa ujumla wanufaike ni kaazi sana

Well said! Human resources ndo kila kitu hata km wagonjwa wote watalala vitandani lakini daktari hana moyo wa kuwatibu watakufa tu, lakini hata wakilala chini na daktari ana moyo wa kuwaponya watatibiwa na watapona tu
 
Huu ujinga ulijengwa na marais waliopita kasoro Nyerere. Inabidi sharia ichukuliwe haraka ya kuwakamata kina Mwinyi, Mkapa, JK kabla hawajafa ili wachukuliwe hatua ya kuzorotesha taifa na uchumi wake. Nchi ilipoteza dira kabisa mpaka na wananchi wake karibia ya wengi hawana matumaini ya kesho. Wasomi ndiyo wamekuwa wasanii na hawapendi maendeleo bali njia za mkato.
 
Afute kwanza posho za wabunge, inakuwaje anakomalia wafanyakazi tu?

Mkuu Posho za wabunge ziko kisheria sio Hisani hivyo hawezi kuzifuta labda kupunguza.

Dodoma sio eneo la kazi kwa wabunge bali ni kwenye majimbo yao. Huwezi kumtoa mbunge kule mtwara aje Dodoma usimpe pesa ya accomodation pamoja na kujikimu

Posho hii haiko tu kwa wabunge bali kwa wafanyakazi wote wa umma na makampuni binafsi wakiwa nje ya eneo lao la kazi.
 
Hao ni watu wa kunyongwa tu.

Umeposti saa tisa na nusu hivyo hao watu wanakunywa wakati wa kazi!

Huo ndo mfano wa watu wanaojifanya wanafanya kazi kumbe ni mizigo.

daktari akiwa night shift ana pingamizi kujiburudisha mchana? ukiwa ukanda wa pwani mchana kutwa utakuta watu vijiweni wakinywa kahawa na kupiga soga. ukichunguza utagundua kuwa wengi wao kama sio wote wako kazini baharini usiku kucha. usipende kujumuisha katika hoja zako
 
Wakuu, niko Rachel bar Moshibar .- Ukonga. Pembeni yangu kuna watu watano wanapata bia. Katika hali ya kustaajabisha namsikia jamaa mmoja akilaani kitendo cha mh. rais kufuta sherehe za uhuru. Anaelezea jinsi gani rais anavyojijengea chuki na watumishi wa umma. Jamaa anahitimisha kwa kutolea mfano yeye akiwa daktari kwenye sherehe za uhuru hutoka na shilingi laki tatu. Anajiapiza kuwa Magufuli atarogwa kwa sababu hii ya kuwanyima ulaji.

Baada ya kuyasikia haya nasema moyoni mwangu, bado safari ni ndefu sana kufikia mageuzi ya kweli. Juzi nilimsikia mama mmoja akilalamika kuwa mwalimu mkuu (shule hakutaja ) alimwambia wazi wazi kwamba kitendo cha kuondoa michango na tuition mashuleni hakikubaliki. Kwamba walimu hawajafurahi hata kidogo, kisha akamwahidi mama huyo kuwa baada ya miezi sita mtakuja kutupigia magoti mkiomba tuition.

Hivi watanzania tumekuwaje hasa!? Unataka nini? Mbona inavyoonekana "wasomi" ndio wanageuka kikwazo kwa mabadiliko chanya? Kundi la wasomi limegeuka kuwa wapigania maslahi binafsi. Tutafika kweli!!?

Mungu mtie nguvu rais wetu, tuko pamoja naye. Amina

Watashindwa na kulegea tu
 
Sio uongo mkuu. zipo hizo allowance.
Kuna wafanyakazi serikalini kutwa kuchwa ni kwenye mikutano na wanalipwa allowance.
Kama hakuna allowance hawaendi.
Na hapo zinatoka allowance za wapiga picha, waandishi wa habari, vitafunio,kukodi ukumbi, mtoa mada(na allowance yake), muwezeshaji-you name it.
Nchi hii inabidi Magufuli afanye kama alivyofanya Mkapa, punguza wafanyakazi wawe wale barely minimum , ili waliobaki walipwe vizuri na wafanye kazi.
sasa inabidi semina ,warsha etc wafanyie kwenye madarasa,hakuna hela ya mchezo
 
Wakuu, niko Rachel bar Moshibar .- Ukonga. Pembeni yangu kuna watu watano wanapata bia. Katika hali ya kustaajabisha namsikia jamaa mmoja akilaani kitendo cha mh. rais kufuta sherehe za uhuru. Anaelezea jinsi gani rais anavyojijengea chuki na watumishi wa umma. Jamaa anahitimisha kwa kutolea mfano yeye akiwa daktari kwenye sherehe za uhuru hutoka na shilingi laki tatu. Anajiapiza kuwa Magufuli atarogwa kwa sababu hii ya kuwanyima ulaji.

Baada ya kuyasikia haya nasema moyoni mwangu, bado safari ni ndefu sana kufikia mageuzi ya kweli. Juzi nilimsikia mama mmoja akilalamika kuwa mwalimu mkuu (shule hakutaja ) alimwambia wazi wazi kwamba kitendo cha kuondoa michango na tuition mashuleni hakikubaliki. Kwamba walimu hawajafurahi hata kidogo, kisha akamwahidi mama huyo kuwa baada ya miezi sita mtakuja kutupigia magoti mkiomba tuition.

Hivi watanzania tumekuwaje hasa!? Unataka nini? Mbona inavyoonekana "wasomi" ndio wanageuka kikwazo kwa mabadiliko chanya? Kundi la wasomi limegeuka kuwa wapigania maslahi binafsi. Tutafika kweli!!?

Mungu mtie nguvu rais wetu, tuko pamoja naye. Amina

Ulivyoandika nadhani wewe ndio muhusika wa kibano hiki ila tu umeamua kujiweka nafsi ya Tatu. Ila mi nachoamini hili sekeseke litachukuwa muda mfupi tu na watanzania wataelewa nia safi ya magufuli na serikali ya awamu ya nne. Nchi hii wananchi wa kawaida wameteseka sana, watanzania wachache ni walafi wanafikiria kupiga tuuuuu...........
 
Unambana mwalimu huku analipa kodi na kupata net salary ya laki mbili halafu na mtu kama wewe unasupport ujinga wakati gas na mikataba mingine ya wakubwa haizungumzi. Ni upuuzi
Kila jambo Lina mahali pa kuanzia. Na huu ni mwanzo, yote yatawekwa sawa. Au kipi kianze? Wajibu Au haki? Tufanye kazi ili tupate maslahi bora au tupate maslahi bora ili tufanye kazi?

Hii ni awamu mpya na mtazamo mpya, elewa hilo. Tusiwe na mawazo mgando, twende na wakati. Tubadilike Na wakati kuliko kusubiri wakati utubadilishe, itakuwa ni kilio na kusaga meno!! Na hii ndio hekimanyingi
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom