Magufuli afanya ziara ya kushtukiza Mtwara

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
Maghufuli%286%29.jpg

Waziri wa Ujenzi, Dk. John Pombe Magufuli


Waziri wa Ujenzi, Dk. John Pombe Magufuli pamoja na Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia, wamefanya ziara ya kushtukiza kwa ajili ya kujionea ujenzi wa kivuko kinachounganisha Mtwara mjini na Msanga, kinachojengwa na kampuni ya M/S Sheepsbouw Noord Netherland B.V.

Akitoa taarifa ya mradi huo jana, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa), Marcellin Magesa, alisema mkataba kwa ajili ya ujenzi wa kivuko hicho ulisainiwa Juni mwaka 2010 kwa Sh. 2.8 bilioni.

“Mkandarasi huyo alipaswa kuanza kazi ndani ya kipindi cha miezi 10 kuanzia hapo, lakini kazi hiyo haikuweza kufanyika kutokana na kutokamilika kwa baadhi ya vipengele vya mkataba ambavyo vilisababisha kuchelewesha usafirishaji wa vifaa muhimu kwa ujenzi,” ilieleza sehemu ya taarifa ya Wizara ya Ujenzi wa vyombo vya habari jana.

Taarifa hiyo ilimshtua Waziri Magufuli na alihitaji kupata taarifa kamili kuhusiana na ucheleweshaji huo na kuagiza kuwa mkandarasi huyo sasa ahakikishe anaongeza nguvu na kukamilisha kazi hizo hata kabla ya muda huo aliopewa.

“Tumekwisha subiri zaidi ya miezi nane kwa kazi hii kuanza, hatuwezi kuvumilia ucheleweshaji wa aina hii,” alisema Dk. Magufuli.

Mwakilishi wa Mkandarasi, Peter Van Brugger, alimhakikishia Waziri Magufuli kuwa kampuni yake imejipanga vyema kuona kwamba kazi hiyo inakamilika kwa viwango na ndani ya muda uliokusudiwa hasa baada ya vikwazo vilivyokuwa vimejitokeza awali kuwa vimefanyiwa kazi kikamilifu.

Naye Waziri Ghasia ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mtwara Vijijini ambako kivuko hicho kitafanya kazi, alielezea kufurahishwa kwake kuona hatimaye ujenzi wa kivuko hicho sasa umeanza na unaendelea vizuri ingawa aliwataka Watendaji wa Temesa kumsimamia vyema Mkandarasi huyo ili kuhakikisha kuwa kivuko hicho kinakamilishwa katika viwango vilivyokusudiwa.



CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom