Mageuzi makubwa CCM

Usanii tu Mkuu. Chama kinachotoa rushwa kwa Wabunge wake ili wapitishe muswaada uchwara kamwe hakiwezi kubadilika. Chama ambacho kinadhani bado tuko kwenye mfumo wa chama kimoja na hivyo kutoiheshimu katiba ya nchi kamwe hakiwezi kubadilika. Chama ambacho kinapora bilioni 16 za wahanga wa tetemeko kamwe hakiwezi kubadilika. Chama kinachodai kwamba mahakama ya ufisadi kutokuwa na kesi ni ishara nzuri wakati kuna mafisadi chungu nzima ambao hawaguswi na mkono wa sheria kamwe hakiwezi kubadilika.
Mara hii wivu lazima ukupeleke Akhera
 
Tarehe22/12/2016,
Asubuhi saa2, Katibu wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi Ndugu Humprey Polepole atakuwa Clouds Tv na Uhuru Fm akizungumzia mageuzi Makubwa Ndani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM).
Usikose.
Akitoka clouds anaenda nyumbani kwa Lipumba kupewa semina zaidi hiyo ndiyo ratiba yake ya leo.
 
Haka kajamaa ka polepole kameulizwa msimamo wake kuhusu serikali 3 lakini anabwabwaja tu anazunguruka Sana kashindwa kujibu
 
Nakubaliana nao tu kama katika mageuzi yao yatakuwa yanalenga yafuatayo:-
1. Kama Chama kikongwe kumshauri m/kiti kukubali na kufuata katiba iliyopo kwa kuruhusu mikutano ya vyama vyote bila masharti yoyote
2. Kujikita katika kurejea ktk katiba ya wananchi kwa maana katiba ya pendekezwa ya warioba na siyo katiba penyekezwa ya bunge maalum la katiba.
3. Kuleta mabadiliko makubwa ya watendaji wa Chama NA kukubali m/kiti kutokuwa ndiyo rais wa nchi hii itaondoa conflict of interest
4. Kukubali kuondoa au kuweka vikundi vya ulinzi kwa Chama chao na kuonyesha njia kwa vyama vingine.
5. Kumaanisha wanachokisema kwa vitendo na kuacha kumzungumzia mtu na kuxungumzia vitu vyenye maslahi kwa taifa. Na zaidi ya yote kurejea misingi ya kanuni za Chama za awali na azimio la arusha
 
Yaani jamaa Kala matamshi yake hivi hivi. Pesa mwanaharamu wallah.
 
sidhani kama anawazidi lema, tundu lissu, mbowe , halima mdee, msigwa
Sasa kama hata akili yako mwenyewe huiamini huoni kuwa humo kumukichwa kuna hitilafu kwenye fyuzi kadhaa?
Eti "sidhani"?!!!
 
Anasema hawezi kuzungumzia serikali 3,ila anadai muungano Una Challenge nyingi, hana jipya Inshort naona anamsifia jpm tu, anadai anawaachia Jpm, makamu wa rais, na katibu mkuu, ndo et watoe msimamo, yaan haeleweki kabsa leo huyu jamaa si wa kipindi kile cha katiba mpya, au alipokua analalaga channel 10
 
Usanii tu Mkuu. Chama kinachotoa rushwa kwa Wabunge wake ili wapitishe muswaada uchwara kamwe hakiwezi kubadilika. Chama ambacho kinadhani bado tuko kwenye mfumo wa chama kimoja na hivyo kutoiheshimu katiba ya nchi kamwe hakiwezi kubadilika. Chama ambacho kinapora bilioni 16 za wahanga wa tetemeko kamwe hakiwezi kubadilika. Chama kinachodai kwamba mahakama ya ufisadi kutokuwa na kesi ni ishara nzuri wakati kuna mafisadi chungu nzima ambao hawaguswi na mkono wa sheria kamwe hakiwezi kubadilika.
Kweli mkuu
 
CCM haiwezi kubadilika hata malaika akiishukia!!! Tatizo la ccm ni moja tu!!! Ukiiacha kansa iliyoanzia mkononi ikasambaa mwili mzima ni ngumu sana kupona!! Walichelewa kukata mkono sasa kansa imesambaa mwili mzima!! Magonjwa anasubiri mauti!!! Ndani ya ccm kuanzia viongozi wakubwa hadi wanachama wa kawaida wote ni wanafiki!!
 
Back
Top Bottom