Kitambi toroli
New Member
- Mar 29, 2013
- 2
- 5
Mbunge wa Mwanga Jumanne Magembe ambaye pia ni Waziri wa maji ni miongoni mwa waziri ambao wamekwishawahi kukabidhiwa wizara mbalimbali lakini Jimbo lake ni Miongoni mwa majimbo yaliyopo nyuma kimaendelea Mkoani Kilimnjaro na kero nyingi kwa wananchi.
Sina maana kuwa apendelee jimboni kwake la hasha bali atambue wajibu wake wa kuwatumikia wananchi,Juzi katika pitapita zangu nilikutaka na wananchi wakijadili kijana mmoja Henry Kileo wa CHADEMA ambaye kwa sasa anamuumiza sana kichwa Magembe kuwa huenda akamtoa kwenye kiti hicho cha Ubunge kutokana na harakati zake.
Nilikuwa napita maeneo ya Kata ya Kigonigoni ndipo nilipokuta gunzo hilo,huku wazungumzaji wakiwa hawajui ni nani na nimetokea wapi,nilikuwa nimenyeshewa na mvua na nguo zangu zikawa zimechafuka hivyo walinihisi na mimi nimvuvi mwenzao kwenye ziwa Jipe.
kwenye Kata ya Kigoni goni yalitokea maafa ya mvua mwezi uliopita na wananchi wakaharibiwa nyumba zao,kwa kuezuliwa mabati,ila na nyingine kubomoka,lakini viongozi waliokuja kuwatembelea waadhirika hao hadi leo hawajegeuka tena.
Lakini Kileo alifika kwenye eneo hilo na kuwafariji waadhirika wa majanga hayo kwa kuwasaidia mabati ya nyumba mbili,ambapo kilichonifurahisha zaidi mmoja wa waliobomokewa na nyumba ni Katibu wa UWT Kata Shaina ally ambaye hata CCM imeshidnwa kumsaidai lakini kamanda huyo amewasaidia bila ubaguzi,huku watu wanasema Chaadema wanaubaguzi.
Kwa kweli kwa taarifa nilizongumza na wananchi wa eneo la Kata ya Kigonigoni kijana Kileo amefanya kazi kubwa na akiendelea na moto huo kwa kuwa karibu na wananchi maana wananchi wengine wanasema tangu wamemchangua hajawahi kumuona.
ndo hilo tu waungwana...