Magazeti Yetu na JamiiForums

Mchambuzi

JF-Expert Member
Aug 24, 2007
4,850
9,405
Imekuwa jadi kwa baadhi ya magazeti yanayotoka Jumatano na Jumapili kuchapisha content nyingi sana kutoka humu JF. Binafsi nimeona content zangu lifted kama zilivyo, neno kwa neno, kwenye matoleo na magazeti kama manne tofauti. Wakishindwa kubadili angalau maneno ili yaendane na mawazo yao, na badala yake kuamua to lift neno kwa neno, ingekuwa jambo la busara sana kama waandishi hawa angalau wangetoa credit kwa jamiiforums, kwani huko ni kujengana kama media platforms. Hawana haja ya kutaja majina ya wachangiaji au watoa mada humu kwani wengi wetu tuna majina ya uongo, lakini angalau watoe credit kwa jamiiforums. Huo ni mtazamo wangu binafsi.
 
Mkuu Mchambuzi ebu weka link za makala zako na makala za hayo magazeti yanayofyonza habari JF.

Imekuwa jadi kwa baadhi ya magazeti yanayotoka Jumatano na Jumapili kuchapisha content nyingi sana kutoka humu JF. Binafsi nimeona content zangu lifted kama zilivyo, neno kwa neno, kwenye matoleo na magazeti kama manne tofauti. Wakishindwa kubadili angalau maneno ili yaendane na mawazo yao, na badala yake kuamua to lift neno kwa neno, ingekuwa jambo la busara sana kama waandishi hawa angalau wangetoa credit kwa jamiiforums, kwani huko ni kujengana kama media platforms. Hawana haja ya kutaja majina ya wachangiaji au watoa mada humu kwani wengi wetu tuna majina ya uongo, lakini angalau watoe credit kwa jamiiforums. Huo ni mtazamo wangu binafsi.
 
some they show credits, i remember zamani nilikuwa naona Jf ikitajwa huko nje, that is why nikajiunga pia ili niwe naziwahi kabla hawajazitoa huko nje, it is better kama wakashukuru na kuonyesha kutambua mchango wa mhusika
 
Siku hizi waandishi wa habari wanarelax hawasumbui bongo zao wanasubiri wapate habari kutoka jf, HONGERENI WANA JF.
 
kwenye kifo cha mh.regia (R.I.P) magazeti mengi yalitaja simanzi ya kwenye mitandao ya kijamii hasa facebook na michuzi, JF haikutajwa katu, wana wivu wa kijinga, but JF nimeona ikitajwa sana na raia mwema na mwanahalisi.
mkuu mchambuzi si kosa sana km wali'quote' coz lengo nikutoa habari na uchambuzi wako pia ulikusudua kutoa habari, sioni kosa.
 
Lakini na sisi humu tunahamisha mengi toka kwenye hayo magazeti. Magazeti hayatoi tu shukrani kwa JF kama wanaJF wafanyavyo wanapoyanukuu. Nyumba tunajenga ni moja. Tusigombee fito.
 
kutoa habari humu wako sahii sana kwa kuwa mtandao huu umesambaa kidunia zaidi hivyo ni kama wako shule ya technoama ya kuwasiliana papo kwa papo na kupata picha ya hali halisi. Kweli ni vizuri wakakubali lakini kwa kuwa hatuna majina halis watatoa pongezi kimoyo moyo kwa kuwaraishia kazi.
 
Mkuu wa Uchambuzi JF kuwa a giant media chini kwa chini haijaanza leo .Muulize hata Mwakyembe na mambo yake ya ufisadi alikuwa anashinda hapa na wengine tulimpa msaada mwingi kuupata ukweli kule US.JF ni kigingi mkuu na ukiona kuna habari za magazetini ina maana yanaletwa kwa mijadala pekee ila kwa kuibua issue JF ndiyo penyewe kama unabisha muulize Salva .
 
Labda kwa vile mwenzetu umejikita kwenye masuala ya magazeti, lakini tukwambie, kuna:
-watu wameoa na kuolewa kutokana na JF,
-wengine wamejipatia marafiki wa kudumu,
-WENGINE wamepata ajira zinazowalipa sana,
-wengine wameuza na kuuziwa vitu vya thamani kama magari, majumba na viwanja
-na wengine wameambulia umaarufu mkubwa sana , kiasi wakipita mahala wakatambuliwa, basi wanaweza hata kunywa Konyagi za bure kwenye pubs!..(Ngongo bado nakumbuka ahadi ya kukutana pale Twiga Sekei kwa Konyagi moja ama mbili)

Kwahiyo, si wa magazeti tu wanaowiwa na JF, huenda hata wewe Mchambuzi unastahiki sana kuihishimu JF kwa nyanja fulani!...huh!
 
Mkuu Mchambuzi ebu weka link za makala zako na makala za hayo magazeti yanayofyonza habari JF.

ukisoma gazeti la raia mwema, makala za johnson mbwambo kama mbili hivi utaona namna ambavyo ameitumia JF kupata taarifa..na inayodhihirihsa ni ile ya last week aliokuwa anazungumzia ukimya wa serikali kuhusu uginjwa wa naibu waziri mwakyembe huku flow yake ikirandana na ile ya jason bourne wa JF,kuhusu litvinenko vs polonium....
Mwanahalisi nao, walinukuu kauli ya ZZK kuhusu ushindi wa maalim seif kule zanzibar........so JF lazima ipewe credits.

ONA HAPA KAMA ANAVYOSEMA MBWAMBO,

Kama, kwa mfano, (narudia maneno ‘kwa mfano’ ) kilichomsibu ni kuwekewa sumu ya polonium 210 kama ile iliyotumika kumuua kachero wa Urusi, mjini London, Alexander Litvinenko, basi umma uambiwe; maana katika u-Mafia ambao tumeufikia hivi sasa hapa nchini kwetu, hilo nalo halitatushangaza sana.
 
Naunga mkono kauli ya bwana Ngongo! Please atupe hizo Link ya makala zake.
 
Mi naona iko poa tu,
Same way na sisi tunavyoingia kwenye Web zao na ku-copy then Paste hapa halafu mtu anajiita nae ana Thread.
Labda tofauti tu ni kua sisi tunaweka source kua ni wao, sina hakika kama nao wanatutaja kama source zao.
 
Ni jambo la kweli cheki gazeti la dimba jmosi au j2 niliikuta habari inayomhusu mhindi,mpare na mchaga ya kutoa mshiko
 
Mkuu Mchambuzi ebu weka link za makala zako na makala za hayo magazeti yanayofyonza habari JF.

Nitawarudia juu ya makala hizi, zipo on hard copy, mfano mmoja ni ile ya last wednesday nadhani kwenye TZ Daima: Nape anaijua katiba.....? mwandishi alichota vitu kama vilivyo, hata pale niliposema nape alitumia 60% ya muda kuji defend na 40% ku attack, mwandishi akabeba hivyo hivyo wakati pengine takwimu zangu hazikuwa sahihi sana, kwani zilikuwa subjective, and based on how i observed the debate...
 
hata TBC husema habari zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii wakati issue ipo hapa pekee! Waseme tu source Jamii Forums!
 
Back
Top Bottom