Magari ya kifahari ya Japan yakamatwa Dar

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,148
Magari ya kifahari ya Japan yasakwa Dar
broken-heart.jpg
Exuper Kachenje
POLISI wa Kimataifa (Interpol) kwa kushirikiana na Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai na ubalozi wa Japan nchini wanaendesha zoezi la ukamataji magari ya kifahari yanayodaiwa kuibwa nchini Japan.

Taarifa zilizoifikia Mwananchi jana zinasema kuwa zoezi hilo la ukamataji limeshaanza na tayari magari zaidi ya 24 ya kifahari kutoka Japan yamekamatwa.

Hali hiyo imeelezwa kuwaweka matumbo joto watu wanaomiliki magari hayo hapa nchini wasijue hatma yao na magari yao huku wengine wakiyaegesha nyumbani bila kuendesha kuhofia kukamatwa.

Kuendeshwa kwa zoezi hilo kunafuatia taarifa za kuwepo wimbi kubwa la wizi wa magari hayo nchini Japan ambayo imedaiwa kuwa huuzwa katika nchi za Kiarabu na Afrika, ikiwemo Tanzania.

Habari zaidi zinasema kuwa magari hayo ya kifahari yakiwemo Toyota Land Cruiser Prado, VX, GX, Lexus pamoja na Toyota Rav4 yamekuwa yakiibwa katika harakati za kupelekwa sokoni mara baada ya kuundwa na mengine yakiwa katika maeneo ya kuuzia magari.

Habari zinadai kuwa zaidi ya magari 350,000 yameshaibwa nchini Japan hadi sasa, yakiwemo magari ambayo wamiliki wake waliyauza na baadaye kusingizia yameibwa ili walipwe bima.

Mwananchi ilishuhudia magari hayo ya kifahari zaidi ya 24 yakiwa yameegeshwa katika kituo cha polisi Oysterbay, huku taarifa za kipolisi zikithibitisha kuendeshwa kwa zozi hilo.

"Ni kweli magari yapo, zoezi hilo linaendeshwa na Interpol na ubalozi wa Japan nchini. Mimi si msemaji lakini ukitaka kujua zaidi, mtafute DCI au Interpol wenyewe. Hapa wameyaegesha tu kwa kuwa ni eneo la polisi lakini hakuna taarifa zaidi," alisema mpashaji habari wetu.

Mwananchi ilishuhudia pia gari la ubalozi wa Japan nchini likiwa kwenye kituo hicho kabla ya kuondoka saa 10:33 jana jioni.

Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba alipoulizwa, alikiri akisema: "Taarifa kuhusu hilo mtapewa, mtapewa baadaye, usiwe na haraka taarifa mtapewa tu."
Tuma maoni kwa Mhariri
 
waanze na magari ya madeshee wa mujini kwani kunatetesi kuna mmoja wa wagombea uraisi mwaka 2005 alipewa gari kwa ajili ya kampeni na pedeshee mmoja(JAMBAZI WA MAGARI) kwa ajili ya kampeni Interpol wakalikamata
 
waanze na magari ya madeshee wa mujini kwani kunatetesi kuna mmoja wa wagombea uraisi mwaka 2005 alipewa gari kwa ajili ya kampeni na pedeshee mmoja(JAMBAZI WA MAGARI) kwa ajili ya kampeni Interpol wakalikamata

Kama wewe si muongo mtaje, vinginevyo wewe ni muongo na mfitinishi.
 
Kama wewe si muongo mtaje, vinginevyo wewe ni muongo na mfitinishi. __________________
AKIWA SHOGA YAKO......UKAMWAMBIE ALIFICHE..WAPE WATU UHURU WA KUANDIKA....
 
hiyo tetesi tulisikia kwani hao wanaojiita mapedeshee wengi wao si wezi wa magari na kuuza madawa ya kulevya na kuuza gold feki kwa wazungu?ila wanakifadhili chama cha mapinduzi ndio kama kinga kwao,kwani tarime CCM kiti cha udiwani walikosa si kwa sababu walimsiamamisha Jambazi maarufu musoma na Mwanza najulikana(anamiliki mabasi ya Z..............ri..bus service
 
Back
Top Bottom