Magari, pikipiki yang'olewa matairi. Ni katika kutekeleza agizo la Rais Magufuli

Kuna kauli mkuu aliitoa ile siku ya uzinduzi haikuwa kauli ya kutolewa na mkuu wa nchi ambaye amewekwa pale kwa mujibu wa sheria!

Yote kwa yote me niliamini hiyo ni kauli tu ya kuwatisha wanaofanya huo mchezo kumbe haikuwa hivyo!
 
20170201_201033.jpg
 
Baada ya agizo la Rais Magufuli kwa watu wanaotumia barabara ya mwendo kasi magari na piki piki zao kung'olewa matairi.

Agizo hilo limeanza kutekelezwa kwa pikipiki na magari kung'olewa matairi.

Nimeshudia pikipiki na magari yaliyong'olewa matairi kwa macho yangu.

Kamanda Mpinga kasema watu hao watafikishwa mahakamani. Hukumu kabla ya kesi, kama polisi akikuchukia kwa visa binafsi na kukuchomekea umetumia barabara ya mwendo kasi imekula kwako.

Bado natafakari!

Chanzo: ITV habari
Yaani Umeshuhudia wewe Mwenyewe and then Chanzo: ITV? Ambiguous
 
Wakati haya mabasi yanaanza kulikua na ajali nyingi sana. Mara pikipiki zimegongwa au magari na wakati ule mlikua mnalalamikia sana serikali na kuwaponda bodaboda leo mnawatetea wanaovunja sheria na kujitakia ajali?

Umeshaambiwa hii njia ni kwa ajili ya mabasi ya mwendo kasi tu. wewe ni nani kuvunja sheria na mimi na support yatolewe mataili tu


Kipindi hiki tutaheshimiana. Kama huwezi jiongoza mwenyewe ukajua hiki ni kibaya ngoja uongozwe tu.

HAPA KAZI TU
 
Ifike wakati waafrica tujifunze namna ya kufuata sheria, umeambiwa ni barabara special ya mabasi maalum, we mbio na Vits yako au tukutuku yako..... iking'olewa tairi usilalamike, fools learn in a hard way!!
Sahivi tutaheshimiana tu mkuu
 
Mwezi wa12 nilibahatika kuokoa maisha ya mke wangu baada ya kwenda muhimbili wakazingua nikaamua kuhamsha subaru kwenda kwa dr kahiruki hospital. Niliingia mwendo kasi fire mpaka Morocco. Na nadhani nilitumia si zaidi ya dakika 10 toka muhimbili mrembo wangu alishaingizwa theatre mikocheni. Nawashukuru waliojenga mwendokasi. Nawashukuru mikocheni hospital kwa kurudisha maisha yaliyokuwa yanapotea ghafla. Kauli ya mrembo wangu pale muhimbili "nisipoweza kuishi tena just know I love u" aya maneno sitasahau na nilikuwa tayari polisi watoe matairi!!
 
nafikiri haitakua sawa wachomoe matairi na bado wakupeleke mahakamani... ni muhimu kuzingatia sheria! wanasahau sheria no msumeno ipo siku utawaka na wao:mad:
 
Back
Top Bottom