Magaidi wa IS watishia kumuua Papa, Papa Francis azungumzia tishio hilo

Status
Not open for further replies.

leiya

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
648
1,546
Watu wanne wanaosadikika kuwa ni magaidi wamekamatwa nchini Italia na Kosovo kwa tuhuma za kupanga njama na kutishia kumuua kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis.

Watu hao ambao wamebainika kuwa na uhusiano na magaidi wa kundi linalojiita Islamic States, walikamatwa na kikosi maalum cha kupambana na ugaidi nchini humo kilichokuwa kikiwafuatilia walipopanga njama hizo na kuweka vitisho kwenye mitandao ya kijamii.

Polisi nchini Italia wamesema kuwa watu hao waliweka vitisho kwenye mitandao ya kijamii na kueleza kuwa ‘Papa Francis anaweza kuwa Papa wa mwisho'.

Aidha, Papa Francis alifanya mahojiano na Carcova News na kuelezea vitisho hivyo, na hivi ndivyo alivyoeleza;

"Maisha yako mikononi kwa Mungu. Nimeshamwambia Bwana, ‘yaangalie maisha yangu'. Lakini kama ni mapenzi yako kwamba nife au kitu kingine chochote kinitokee, nakuomba kitu kimoja tu.. kwamba kisinipe maumivu. Kwa sababu mimi ni binadamu mwenye hisia kali hasa linapokuja suala la maumivu ya mwili'."

Chanzo: Dar24
 
Maneno ya huyo Papa ndo maneno kuntu kabisa. Maisha yetu yapo mikononi mwa Mungu ambaye ni mkuu kuliko hayo magaidi.
Wanaweza panga vyema, njia na nanmna ya kumuua Papa, wakafa wao sekunde moja kabla tena wala si kwa kuuawa na mlinzi bali malaika wa Mungu
 
Yaani Habari nzito kama Hiyo isitangazwe na corporate media kama aljazeera, CCN, BBC n.k Hapana.
 
--------- Khomein alitangulia kabla ya Salman Rushdie mwandishi wa kitabu cha aya za shetani{satanic verses]
 
ISIS kuna ile adhabu ya kubana makende, kama ni wanaume hiyo ndio adhabu kali hadi wanajutia... kisha kuwaua...!
 
Watu wanne wanaosadikika kuwa ni magaidi wamekamatwa nchini Italia na Kosovo kwa tuhuma za kupanga njama na kutishia kumuua kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis.

Watu hao ambao wamebainika kuwa na uhusiano na magaidi wa kundi linalojiita Islamic States, walikamatwa na kikosi maalum cha kupambana na ugaidi nchini humo kilichokuwa kikiwafuatilia walipopanga njama hizo na kuweka vitisho kwenye mitandao ya kijamii.

Polisi nchini Italia wamesema kuwa watu hao waliweka vitisho kwenye mitandao ya kijamii na kueleza kuwa ?Papa Francis anaweza kuwa Papa wa mwisho?.

Aidha, Papa Francis alifanya mahojiano na Carcova News na kuelezea vitisho hivyo, na hivi ndivyo alivyoeleza;

?Maisha yako mikononi kwa Mungu. Nimeshamwambia Bwana, ?yaangalie maisha yangu?. Lakini kama ni mapenzi yako kwamba nife au kitu kingine chochote kinitokee, nakuomba kitu kimoja tu.. kwamba kisinipe maumivu. Kwa sababu mimi ni binadamu mwenye hisia kali hasa linapokuja suala la maumivu ya mwili?.?

Chanzo: Dar24

Kama ni kweli basi kundi hilo linataka kufutika katika ramani ya dunia.
 
Huyu PAPA mbona mwoga sana?! MASIHA MWANA WA MUNGU alipigwa mijeledi na ile miyahudi, akabebeshwa msalaba mzito, kuchomwa mkuki wa ubavuni, kugongelewa misumari, kuvishwa taji ya miba na kunyweshwa SIFONGO lakini bado hakulia wala kuteteleka.... tena akawaambia akina mama walokuwa wakimlilia "oyaaa niondoleeni makelele yenu hapa na msinililie mimi bali lilieni nafsi zenu"
Sasa PAPA analialiaaa kabla hata hajaguswa wala kuchubuliwa na hivi vimjamaa vya ISIS!
Tell Him to be a Gentleman like JESUS!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom