Mafuta ya Ubuyu salama

Hawa TFDA wana lao jambo.naona walishindwa kuelewana kuhusu 10% na wale wajasiriamali waliokuwa wanauza mafuta hayo pale sabasaba!watatangazaje issue nyeti kama hiyo kwenye maonyesho?walikuwa wapi siku zote? NIMR ni Taasisi inayoshughulika na utafiti wa dawa zote(za kisasa na dawa mbadala).wako right kuhusu suala hili na ndo wahusika wakuu.TFDA wasituletee usanii kwa suala nyeti kama hili linalohusu maisha ya Watanzania.
 
Tuwekeen basi facts kabla ya opinion zetu, wengine hatujaziona zote. NIMR wanasemaje, na TFDA wanasemaje?
 
kuna upotoshaji mkubwa ,TFDA walisema ukitumia kwa kiwango kikubwa sana ndio ni hatari lakin watu wameamua kupotosha na kusema ni hatari kutumia
 
Akili kichwan mwako,,....coz kila mmoja anasema lake,,....pambanua mwenyewe
 
Wakuu tusipende kucheza sandakarawe na maisha yetu..., tunajua kabisa kwamba vitu vingi ni sumu ila vikifanyiwa treatment vinakuwa salama mfano
Maharage yana sumu (ukila mabichi) lakini yakipikwa ile sumu inatoka
Mihogo vilevile ina sumu ila ikifanyiwa treatment inakuwa salama
Kisamvu kina sumu ila ukikipika sana kinakuwa salama
Mwarobaini ukitumia sana inaweza ikaleta infertility

Sasa wakuu umeshaambiwa mafuta ya ubuyu yana sumu (kwahio usiyanywe) ila unaweza kutumia externally, au kama unaweza kuyafanyia process kuondoa hizo sumu basi ni salama..., sasa cha maana badala ya kulalama ni kuchukua opportunity ya kuweza kuondoa hizo sumu ili iwe salama.

Kumbuka pia kuna vitu hapo zamani tulidhani ni salama kumbe baadae tukafahamu kwamba sio salama
 
Hawa TFDA wana lao jambo.naona walishindwa kuelewana kuhusu 10% na wale wajasiriamali waliokuwa wanauza mafuta hayo pale sabasaba!watatangazaje issue nyeti kama hiyo kwenye maonyesho?walikuwa wapi siku zote? NIMR ni Taasisi inayoshughulika na utafiti wa dawa zote(za kisasa na dawa mbadala).wako right kuhusu suala hili na ndo wahusika wakuu.TFDA wasituletee usanii kwa suala nyeti kama hili linalohusu maisha ya Watanzania.

continue to play politics kwenye swala nyeti kama hilo majibu yake utayapata!
 
Back
Top Bottom