SoC01 Maendeleo ya kijamii: Changamoto na mapendekezo yake

Stories of Change - 2021 Competition

mzee_kijana

New Member
Jul 15, 2021
4
2
Uhali gani mwanafamilia wa JF

Karibu katika makara maalumu leo naomba nikuelekeze katika Maendeleo ya kijamii na kwa kuanza makara hii naomba nitangulize shukurani kwa mda wako wewe msomaji.

Kabula ya yote ni vyema tujue maendeleo ya kijamii ni nini? kwa ufupi tu maendeleo ya kijamii ni hali ya watu kukusanyika pamoja kwa ajili ya kutafuta utatuzi au ufumbuzi wa changamoto zinazo wakabili.

Katika kukuandalia Makara hii nimechunguza changamoto katika sekta ya elimu, Miundombinu, Afya, Utawala bora na kilimo hivyo kwa muhtasari kabisa nimekuletea uchambuzi wa changamoto na mapendekezo ya nini kifanyike.

Elimu

Kwa upande wa Elimu Jamii ya kitanzania kwa sasa imekuwa na muamuko na naweza kusema kuwa tumepiga hatua kubwa sana, tofauti na kipindi cha nyuma kwa sasa Elimu inatazamwa na watanzania wengi kama sekta muhimu na hivyo kuipa kipaombele katika mijadala mingi ya maendeleo lakini bado kuna changamoto nyingi zinazohitaji jitihada za serikali lakini pia kuna changamoto ambazo sio lazima serikali kuhusika ambapo kila mmoja kwa nafasi yake akitimiza wajibu wake changamoto izo zinaweza kupungua ama kuisha kabisa.

Changamoto izo ni pamoja na tatizo la Mimba kwa wanafunzi wa kike,Utoro, Miundombinu midogo kama Vyoo,Madawa,maji, huduma ya chakula na hata madarasa.
Kwenye shule zenye changamoto za namna hiyo wanajamii tukiunganisha nguvu tunaweza kubolesha Elimu ya msingi na kuongeza ufaulu.

Lakini pia ni wazi bado watu wenye ulemavu wa viungo katika shule nyingi kwenye jamii zetu hawana nafasi kwani miundombinu ya shule nyingi haina mazingira rafiki kwa watoto wenye ulemavu hasa wa viungo na kutokana na uchache wa Shule maalumu kwa ajili ya watoto wenye ulemavu inakuwa ni vigumu watoto kupata haki yao ya msingi ya kupata elimu hivyo basi ni muhimu serikali kutilia mkazo katika kuwatafuta watoto wa aina hiyo ili kuwapeke katika shule maalum kwa ajili ya watoto wenye ulemavu au Jamii kuliona hilo na kujenga au kuhimiza ujenzi wa miundombinu inayowawezesha walemavu kupata elimu kama watoto wengine.

Pia Elimu ya kutosha inahitajika ili kuhakikisha wazazi wengi hasa katika maeneo ya vijijini kutowaficha ndani watoto wenye ulemavu kwani watoto hao wana haki ya kuelimika kama walivyo watoto wengine wasio na ulemavu.

Lakini pia ni jambo lililo wazi kwamba kwa sasa tatizo la Ajira ni pasua kichwa katika jamii zetu hapa nchini mimi na tatizo hili linahitaji ufumbuzi wa haraka ili lisiendelee kutatiza harakati za maendeleo ya kitaifa.

Cha kufanya pamoja na kukaribisha uwekezaji wa sekta binafsi ili kutengeneza Ajira mpya pia ni muhimu zaidi kuandaa mazingira ya kudhibiti ukubwa wa tatizo katika miaka mingi ijayo na ili kutekeleza ili yapo mengi ya kufanya ila kubwa zaidi naona kuna haja ya kufanya mabadiliko makubwa katika mitaala ya kufundishia ili ijikite katika kutoa Elimu ujuzi ili kuwapatia ujuzi utakaowawezesha vijana kujiajiri baada ya kuhitimu na kupunguza changamoto ya ajira kwa wahitimu wa vyuo na wale ngazi ya Elimu ya msingi, pia njia nyingine inayoweza kupunguza changamoto ya ajira ni serikali kutilia mkazo katika masomo ya Tehama kwani kwa sasa kupitia teknolojia vijana wanaweza kujiajiri na kuendesha maisha yao.

Kilimo

Tukiachana na elimu kuna suala zima la kilimo na kama mnavyojua 65% ya watanzania ni wakulima lakini 63% kati yao wanatumia kilimo cha jembe la mkono.

Hivyo katika sela ya kilimo serikali inatakiwa kuzingatia kundi hili la wakulima wadogo ili kuwawezesha kufanya kilimo chenye tija.

Pamoja na mambo mengine ni vizuri serikali iwapatie wakulima hao elimu ya kilimo bora kupitia serikali za vijiji au mitaa aidha kwa makundi au kwa mtu mmoja mmoja ili walime kisasa kuliko kufanya kilimo cha mazoea ambacho matokeo yake huwa ya kubahatisha na hatua hiyo iambatane na utoaji wa pembejeo na kuwatafutia masoko ya uhakika na bei isiyowaumiza wakulima hili kuongeza uzalishaji na kupunguza kiwango cha Umasikini.

Lakini karibia jamii zote za wakulima nchini hulalamikia mamlaka kutowatendea haki wakulima kwa kutumia vyama vya ushirika kuwanyonya, hasa katika mazao ya biashara na hii husababisha wakulima kulima na kuzalisha kwa wingi ila faida kutoendana na jitihada zao husika hivyo kufanya wakulima wengi kukosa mwamko katika kilimo na kushusha thamani ya shughuli hii ambayo ndio uti wa mgongo wa taifa letu. Sababu kubwa katika changamoto hii ni viongozi kutokuwa wawajibikaji au waaminifu katika nafasi zao na pia kutunga sheria kandamizi kusimamia kilimo bila kujali adhari kwa wakulima wenyewe.

Kupitia Makara hii nitoe ombi kwa waliopewa dhamana ya kushughulikia ukuaji wa sekta hii kuwa waaminifu na kuzingatia masilahi ya wakulima ili kuimalisha kilimo nchini.
Kumbukeni utawala bora ni pamoja na kuwatengenezea mazingira rafiki watu wako katika sekta mbalimbali ili waweze kuchangia uchumi wa nchi.

Afya

Baada ya kutazama kilimo sasa tugeukie upande wa Afya
Ni wazi Hatuwezi kuhitimisha makala hii bila kujadili Afya na Sote tunajua Afya ni muhimu sana kwani yote tuliyoyajadili hapo awali hayawezekani kama hatutakuwa na Afya njema ivyo kwa kuliona ilo naomba japo kwa ufupi tuliangalia swala hili.

Katika jamii nyingi za kitanzania hasa katika ngazi za vijiji na mitaa tuna utaratibu wa kuchangishana sisi wenyewe kugharamia ujenzi wa zahanati na vituo vya afya lakini jitihada hizo mara nyingi huingia dosari pale serikali inaposhindwa kutimiza wajibu wake licha ya wananchi kujitolea.

Ili kukabiliana na changamoto hizi ni vyema viongozi tunaowachagua kutuwakilisha vyema na kuhakikisha vifaa tiba,madawa na wataalamu wanaletwa katika vituo husika ili kutatua changamoto za kiafya kwa wananchi wa eneo husika.

Kwa kufanya hivyo tutapunguza idadi ya vifo vya akina mama wajawazito wanaopoteza maisha kutokana na kukosa huduma katika maeneo ya karibu wakati wa kujifungua.

Mwisho kabisa niwaombe watanzania tuendelee kuhamasishana na kupeana elimu ya ulipaji kodi ili kuwezesha serikali kutekeleza miradi ya maendeleo hasa miundombinu ya barabara ambayo ni tatizo katika maeneo mengi nchini bila kusahau uwajibikaji binafsi kwani bila kufanya kazi kwa bidii Tanzania ya uchumi wa kati itakuwa kwenye makaratasi tu.

Bila shaka kwa kufanya hivyo jamii ya kitanzania itaimalika kiuchumi na kauli mbiu ya serikali ya Kazi iendelee itakuwa na matokeo Chanya.

Kwa pamoja tunaweza kufikia malengo kila mmoja akitimiza wajibu wake.

Asanteni
 
Mkuu kwa kurejea kauli mbiu hiyo je, hauoni kama ni kauli kandamizi?
Yaani kazi iendelee wakati tunapandishiwa hadi kodi za tozo kwenye makato ya simu.

Kazi iendelee ina maana pana sana, Kauli mbiu hii inaweza kuihusu serikali au kukuhusu wewe moja kwa moja kwani wajibu wa kufanya kazi ni wa kila mmoja wetu.

Kaka Ni vizuri kauli hii tusiitafisr kisiasa ili tupate maana yake halisi
 
Shukran Sana kwa maelezo mazuri lakini kutokana na maelezo yako mwanzo ukipata kutaja Mambo matano lakini umeweza kuelezea matatu,
Hivyo na maswali Kama mawili
1: je ni kivipi utawala Bora na miundombinu inaweza kuwa chachu ya kimaendeleo katika jamii?
2: changamoto gani zinaikumba sekta hizi kuendelea hasa kwa nchi yetu? Na nini kifanyike ili kuondoa changamoto izo na kufanya sekta endelevu katika ukuaji wa uchumi wa nchi?
 
Bonyeza hapa
shukurani mkuu kwa maelezo Hayo nakutakia ushindi mwema
 
Shukran Sana kwa maelezo mazuri lakini kutokana na maelezo yako mwanzo ukipata kutaja Mambo matano lakini umeweza kuelezea matatu,
Hivyo na maswali Kama mawili
1: je ni kivipi utawala Bora na miundombinu inaweza kuwa chachu ya kimaendeleo katika jamii?
2: changamoto gani zinaikumba sekta hizi kuendelea hasa kwa nchi yetu? Na nini kifanyike ili kuondoa changamoto izo na kufanya sekta endelevu katika ukuaji wa uchumi wa nchi?
Asante kaka

Asante kaka Katika utangulizi wangu nimetaja Afya,Elimu,Kilimo,Utawala bora na miundombinu.

Katika ufafanuzi nimegusia kila sekta iliyotajwa hapo awali ila kwa ajili ya kufupisha chapisho chapisho, Utawala bora bora nimeuzungumzia moja kwa moja kwenye sekta ya kilimo na miundombinu nimeigusia kwa ufupi katika hitimisho kwenye ushauli wangu kuhusu kuhamasishana kulipa kodi ili kusaidia serikali kutekeleza miradi ya maendeleo.

Sababu za kufanya hivyo ni kujaribu kupunguza maneno katika chapisho husika ili lisikiuke vigezo na masharti ya JF.

Majibu ya maswali yako;

1.Utawala bora ni Matumizi ya uwezo(Mamraka) wa kiserikali katika jitihada za kuongeza na kutumia rasilimali ili kuboresha maisha ya wananchi.
Pia neno hili hutumika kuelezea taasisi za umma zinavyofanya mambo yake kwa umma na kusimamia raslimali zao.

Kwakuwa utawala ni mchakato wa kufanya maamuzi na kuyatekeleza mchanganuo wa utawala hurenga kote na watekelezaji wa utawala wanawezakuwa rasimi au wasiwe rasimi ila wote uhusisha katika maamuzi.

Watekelezaji wa utawala ni Pamoja na Wafanyabaishara wakubwa ,Vyama vya wafanya kazi,Ushirika,Vyama vya wakulima,NGos,Majeshi,Taasisi za fedha,Serikali n.k
Kwa maana hiyo utawala unahusu maamuzi,utekelezaji,usimamizi n.k hivyo ni dhahiri kwamba utawala bora unachangia pakubwa maendeleo ya kijamii kwani kila shughuli ina wasimamizi wake ambao ndio utawala katika shughuli husika.

Kupitia utawala bora tutakuwa na vyama vya ushirika visivyowanyonya wakulima,tutakuwa na Serikali inayosimamia rasimali za umma kwa uwazi na uaminifu,pia tutakuwa na viongozi wanaozingatia masilahi ya umma badala ya kuzingatia masilahi binafsi hivyo italeta hamasa ya kufanya kazi katika jamii na uchumi utakuwa.

Pia kwenye swala la miundombinu ni wazi kwamba inahusika pakubwa kukuza uchumi wa nchi kwani ndio msingi wa shughuli za kiuchumi.

Mfano mzuri ni miundombinu ya barabara ambayo urahisisha shughuli za kibiashara kutoka eneo moja kwenda jingine hivyo kuongeza kazi ya biashara na kurahisisha pia upatikanilaji wa masoko.

2-Changamoto zinazokumba sekta hizi nimeelezea ila kwa ufupi tu na kwa upande wangu naona ni pamoja na Sera,Utawala bora na Uwajibikaji cha kufanya ni kila mmoja kutanguliza, masilahi ya taifa mbele na kutimiza wajibu wake ipasavyo.

Tukiwa wawajibikaji utapunguza changamoto kwa ukubwa.

Tukiwa na sera endelevu tutapunguza changamoto katika sekta tajwa na

Viongozi wetu wakitekeleza wajibu wao kwa kuzingatia utawala bora tumaliza changamoto zote zinazozikabili sekta hizi muhimu.
 
Back
Top Bottom