Maendeleo ya CHADEMA Njombe

SG8

JF-Expert Member
Dec 12, 2009
3,955
2,125
Kwa niaba ya M/kiti wa CDM Wilaya ya Njombe (mkoa mpya wa Njombe) napenda kuwafahamisha wapenda mabadiliko wote hasa wapenzi, wanachama, mashabiki wa CDM na wananchi kwa ujumla kwamba tunaendelea vizuri na kazi ya kusambaza moto wa mabadliko kama yalivyoasisiwa na Mh Thomas Nyimbo.
Wale wenye kumbukumbu mtakumbuka kuna siku nilileta hapa mada inayoeleza jinsi Mh. Nyimbo alivyojitolea kwa hali na mali kuwasha moto wa mabadiliko. Kwa hakika tumefanikiwa sana kwa ngazi ya jimbo la Njombe Magharibi na sasa tumeunganisha juhudi na Majimbo mengine ya Njombe kusin na Kaskazini. Kuanzia mwezi wa pili (Februari) tunatarajia kuwasha moto kuelekea LUDEWA na MAKETE kwa msaada mkubwa wa Mh. Nyimbo ili hatimaye mkoa wa Njombe uwe na nguvu kama ile ya Mwanza, Mbeya, Iringa, Arusha na Kilimanjaro.
OMBI MAALUM
Kama yupo mwanaJF anaweza kutusaidia contacts za mtu yeyote wa Makete na Ludewa tunaomba tafadhali sana atusaidie kabla ya Jumapili ya wiki hii ili tuwasiliane naye mapema iwezekanavyo. Tumefikia hatua hii baada ya jitihada zetu kuelekea kukwama. Tafadhali kama unayo namba ya mtu au watu au wewe mwenyewe tujulishe kupitia 0789149165 (M/Kiti CDM Njombe (W) au mgosa81@yahoo.com.
Tunawashukuru sana kwa support yenu

Hakuna kulala.........
Posted by Kiongozi
 
Hongereni Sana wapiganaji. Nasi wa Mbarali Moto unaanza mwezi wa Pili, tukishirikiana na Mh. S**u. Moto utakaowaka CCM hawatakuja sahau maishani mwao. Kilafi anahesabu siku.
 
Jamani huu wito umejaa hekima, busara na utekelezaji wa wazi.. Hizi threads siyo kila mtu anaziona wakati muafaka. Tusaidiane kulibeba hilo jukumu loa kuwaainisha na kuwaarifu wahusika kama unamfahamu mtu wa maeneo hayo ambaye siyo lazima awe mwana JF mpe taarifa muarifu tafadhali.
 
Moto wa mabadiliko ndio nini?

Kama umelala amka, kama uko kwenye chama cha majambazi jiunge na chama cha maslahi ya Taifa. Ni mambo ya kubadilisha upuuzi wa kisiasa kuwa umakini wa kisiasa kwa maslahi ya Taifa.
 
Thanks mdau kwa juhudi mnazofanya kwa mkoa wetu mpya wa njombe. Ninachofahamu mie ni kuwa wilaya hizi zina uongozi kamili ambao kwa hakika contacts zao zipo cdm hq. Mkipata contacts mtaanzia hapo kuendeleza mapambano.
 
Bravo nami katika kuunganisha nguvu hiyo nimebadili upepo hapa jiran kuna kijiwe cha wauza nafaka ya mahindi na mihogo now wote ni chadema nafanya mpango wa kuwapatia bendera
 
Ni kweli nimesikia juhudi za mh. Nyimbo. Wiki kadhaa zimepita tangu tulipoambiwa humuhumu jf kwamba mh Nyimbo amepania kufungua matawi ya cdm vijiji vyote jimbo la Njombe magh, hakika kazi alishaianza na juzi alikuwa ktk kjiji cha Ukomola ambako alipata kuungwa mkono na wanakijiji wengi sana.
 
Moto wa mabadiliko ndio nini?
Huna lolote wewe topical unatafuta tu namna ya kuingiza udini hapo lakini hapaingiliki kwani hayo maeneo yaliyotajwa hapo kumefugwa manguruwe kila kona. Ukileta udini wako hawakusikilizi wala nini na MoU imetunufaisha sana mkoa wa Njombe kiasi tunaanza kusahau nyumba za nyasi.
 
Kazi nzuri sana ya kueneza mabadiliko maeneo hayo. Iliniuma sana Filikunjombe na Makinda kupita bila kupingwa hadi nimeshawishika kuingia ulingoni. 2015 natangaza nia kujitosa katika jimbo jipya la Njombe mjini litakapoundwa.
 
Kazi nzuri sana ya kueneza mabadiliko maeneo hayo. Iliniuma sana Filikunjombe na Makinda kupita bila kupingwa hadi nimeshawishika kuingia ulingoni. 2015 natangaza nia kujitosa katika jimbo jipya la Njombe mjini litakapoundwa.
Hongera kwa maamuzi magumu hivi hamna kijana makini wa kumvaa makinda maana mimi nitachangia kampeni za kumpoteza huyu mama 2015. Hatutaki kumwona tena bungeni. Naamini hataweza kusimama mbele ya vijana makini wa chadema. Kampeni zianze sasa hivi hakuna kulalal.
 
Njombe keep up, kuna vijamaa baba zao wametutesa kwa kutuibia sasa vinajifanya kuwalaani ili tuone vyenyewe vimekuja kutukomboa. HATUDANGANYIKIIIIIIIIII
 
Bravo,

Mtangulizeni Mungu kazi ya ukombozi siyo lelemama. Elimu ndio ukombozi kwa wananchi wengi wa vijijini.

May God bless you all.
 
Good news yule waliyempa kwa nguvu kwa kudhulumu kura za nyimbo ni ndugu yake K/MKi. (Mzee FR), CCM lahana tupu
 
Hongereni sana wapiganaji kwa kuwapa wananchi fikra mpya za ukombozi. Najua eneo lote hilo nyimbo za ccm zilikuwa zimegandisha ufahamu wa wananchi kujitambua. Narudia tena, hongereni sana.
 
Back
Top Bottom