Maendeleo Tanzania - kutofadhiliwa kwa wasomi

Chapakazi

JF-Expert Member
Apr 19, 2009
2,874
310
Sina uhakika kama kuna thread hii tayari, lakini nilikuwa nawaza; Kwa nini Tanzania tunashindwa kupiga hatua za maendeleo?

Moja ya jibu nililoweza kupata ni serikali kutofadhili wasomi. Mara nyingi katika nchi zilizoendelea, serikali zinatoa pesa kwa vyuo kwa kusudi la research. Mifano hai hii hapa: Stanford, Princeton, Cambridge, nk.

Research hii inasaidia kuangalia matatizo na hata kutafuta solution ya hayo matatizo yanayokumba jamii na nchi kwa ujumla.
Tatizo ninaloliona Tanzania (kwa maoni yangu) ni watu wengi kuenda nje ya nchi kwa ajili ya research. Tatizo la mtindo huu ni hizo research kutokuwa 'targetted' katika maendeleo ya nchi yetu.

Kwa nini serikali zisingeboresha hili jambo? Kama huu ufadhili upo, je unapatikanaje? Ni open process au ndo ile ya kibongo kwa rushwa na upendeleo?
Pia publication ya hizo research inafanyika na kwa uwazi kiasi gani? Au ndio zinakusanya vumbi tu? Nadhani siasi zimekithili sana nchi zetu kuliko utendaji.

Wanajamii mnaonaje hilo?
 
Kiongozi Mtoto,
ulichoandika ni kweli kabisa, hata hivyo sababu ya kwanza kabisa ya umasikini Tanzania ni gonjwa la Malaria na namba mbili ni utawala mbovu.
Research ni muhimu lakini kwa jinsi dunia ilivyo sio kila research lazima tufanye kama watanzania. Matokeo ya research yapo na matumizi yake kama technolojia tunaweza kuinunua.Nchi masikini kama Tanzania ikiingiza kwenye gharama kubwa za sophisticated research itaingia kwenye umasikini zaidi.
 
Kiongozi Mtoto,
labda nikuulize swali tu. Unadhani kuna tatizo gani la Tanzania ambalo halijafanyiwa research ya kutosha/ ambalo utatuzi wake haujagunduliwa?
 
Mkuu, heshima mbele
Matatizo tunayoya-face ni mengi. Na research sio kwenye technologia peke yake. Kuna research kwenye system ya utawala....mambo ya sociology na power administraion, kuna ya kilimo, hasa katika mikoa, kuna ya madini, nk. Kwa mfano, mtu anaweza kuangalia kama kweli kuwa na mikoa 26 ina faida, pesa wabunge wanazopata zinatumikaje. Yani mkuu, hakuna limit kwenye research. Point ya research ni kukusanya data, and that is lacking. Sitaki tuende kushinda na university kama Princeton inapewa $200mil na serikali ya US, lakini tuanze jamani. There is no one to help us, but ourself. Bila kujichunguza wenyewe, hatutafika popote. Pia kungekuwa na publication ya hizi research nchini, ingekuwa fresh sana. nadhani zipo, lakini ni kwa low level. Sina uhakika na upatikanaji wake.

Pia mkuu, umeongelea malaria. Sasa ivi pale KCMC kuna research iko funded na Gates. Lakini tungekuwa serious, tungeweza wenyewe. Misaada mingine bwana, ndo maana wazungu wanatudharau. Yani tuna vichwa sana nchini, sema tunashindwa kuwatumia. Kumekuwa na to much politicalisation ya system nzima. Badala ya kuwapa wasomi kipaumbele, kitu ambacho nchi zilizoendelea ziliweza kufanya.

Tatu mkuu, sawa system ya utawala mbovu, but we can't be discussing that everyday. Am just opening a discussion on a different angel. Au sio?
 
Wala usiseme mbali huko US, angalia India inavyopiga hatua ktk maendeleo!! Wao zamani nao walizembea kidogo ktk issue ya elimu na kujali wasomi. Lakini ktk miaka ya 80 walianza kuwekeza ktk wasomi wao, hivi sasa India wanacho fanya ni kuwapa wasomi pesa na wasomi wanaandika vitabu ambavyo vinatumika ndani ya nchi yao tu. Japokuwa kama kawaida ya Watanzania, huwa tunadharau vitabu vya wahindi lakini ndo hivyo wanatuacha kimaendeleo kwa kutumia vitabu hivyo hivyo tunavyo vidharau...

Kuna mengi ya kusema kuhusu jinsi serikali zote za Tanzania zilivyo telekeza wasomi lakini muda hautoshi. Ukienda kwenye vyuo vyetu ukauliza budget ya academic departments ni aibu kwa sababu pesa inayotengwa kwa ajiri ya breakfast ya mkuu wa chuo inazidi mara tano ya budget ya idara. sasa fikiria......twafa tukwirola...
 
Mkuu yani hapo umelenga topic kabisa. Angalia nchi kama Japan, na China, South Korea, wamejenga nchi kutokana na usomi wao na research zao. Walituma wachache kwenda ulaya kujifunza. Wale waliporudi, waka-adopt system ya ulaya katika ufanyaji wao kazi.
Wazungu watakunyonya siku zote. Kwa nini aje kukusaidia yeye na asijisaidie yeye kwanza? Nyie wadhani kugawa computer mashule ni bure? wanajenga future market hapo. Wanajua huyu akianza kwa kujifunza kutumia microsoft, ndo tumemdaka maisha yake yote. Na wanajuaje hilo?...through research. Yani research ni kitu muhimu sana. Inakufundisha mengi mno. Sema ndo hivyo tena, tunazembea wenyewe. Kila siku humu JF ni kuongelea serikali na ubovu wake. I am hoping to expand on that, tuongelee vitu vingine. Maana kuitoa CCM pale, sijui! Maybe we should try to correct them na kuwasaidia.
 
Mkuu, heshima mbele
Matatizo tunayoya-face ni mengi. Na research sio kwenye technologia peke yake. Kuna research kwenye system ya utawala....mambo ya sociology na power administraion, kuna ya kilimo, hasa katika mikoa, kuna ya madini, nk. Kwa mfano, mtu anaweza kuangalia kama kweli kuwa na mikoa 26 ina faida, pesa wabunge wanazopata zinatumikaje. Yani mkuu, hakuna limit kwenye research. Point ya research ni kukusanya data, and that is lacking. Sitaki tuende kushinda na university kama Princeton inapewa $200mil na serikali ya US, lakini tuanze jamani. There is no one to help us, but ourself. Bila kujichunguza wenyewe, hatutafika popote. Pia kungekuwa na publication ya hizi research nchini, ingekuwa fresh sana. nadhani zipo, lakini ni kwa low level. Sina uhakika na upatikanaji wake.

Pia mkuu, umeongelea malaria. Sasa ivi pale KCMC kuna research iko funded na Gates. Lakini tungekuwa serious, tungeweza wenyewe. Misaada mingine bwana, ndo maana wazungu wanatudharau. Yani tuna vichwa sana nchini, sema tunashindwa kuwatumia. Kumekuwa na to much politicalisation ya system nzima. Badala ya kuwapa wasomi kipaumbele, kitu ambacho nchi zilizoendelea ziliweza kufanya.

Tatu mkuu, sawa system ya utawala mbovu, but we can't be discussing that everyday. Am just opening a discussion on a different angel. Au sio?

Kiongozi,
nadhani Tanzania tatizo letu sio kufanya research. Research zinafanywa nyingi sana, hasa katika hizo nyanja unazozitaja. Gharama ya research kwa ujumla ni kubwa sana. Ulaya kwa mfano inaendelea kwa parasitism- wanatumia sanasana findings za wengine, Ulaya haitoi kipaumbele kwa research. Marekani ndio wanathamini zaidi research, lakini sasa angalia maendeleo ya Ulaya na Marekani hamna tofauti yoyote. kwa mfano pesa ambayo Ulaya inatumia kwenye research zote za medical field haifikii pesa ambayo Marekani inaingiza kwenye NASA pekee!
Sisemi kuwa research siyo muhimu, ninachosema ni kwamba research sio lazima ufanye mwenyewe.
Umetoa mfano wa Gates Foundation funded project ya KCMC, ni rahisi kusema tungetaka tungefund wenyewe lakini ukweli ni tofauti. Gates anafund research za malaria vaccine, sasa sisi watu ambao hata vyandarua hatujavitumia ipasavyo tuna uwezo wa kuanza kufanya tafiti za vaccine?Kwa sasa swala la research haliwezi kuwa priority Tanzania, kwa sababu its very expensive and it is 'gambling'.
Katika hiyohiyo malaria, nilikutana na kiongozi wa taasisi ya utafiti wa afya mwezi uliopita. Katika mazungumzo akasema Tanzania ina data nyingi sana za malaria ambazo hazijafanyiwa kazi! Lakini cha ajabu ni kwamba kila siku research mpya zinaanzishwa, who is going to analyse the collected data? Wanasayansi wetu nao ni maslahi mbele.Mtu akipata pesa tu basi research ndio mwisho.
Narudi tena kwenye malaria, hivi kweli dunia inahitaji research mpya ya jinsi ya kupigana na malaria? Ugonjwa ambao mataifa mengine yameweza kuupiga vita nusu karne iliyopita! Yaani njia walizotumia wao kuupiga vita tunashindwa vipi kuzitumia kuangamiza malaria? Malaria mpaka sasa ipo na inaendelea kuua watu kwa sababu ya selfishness ya policy makers. Sio kwa sababu hatujui jinsi ya kuangamiza mbu, sio kwa sababu hakuna vaccine na wala sio kwa sababu hakuna dawa.
 
Okay mkuu...point well taken. Umetumia malaria ku-defend argument yako vizuri. I take your word for it kwamba umezungumza na huyo kiongozi wa taasisi ya afya, na kakueleza jinsi data zilivyo nyingi. Mimi nilikuwa sina uhakika na amount ya research inayofanyika au data tulizonazo. Nilidhani tatizo ni kutokuwa na data. Sasa umeonyesha tatizo ni utumiaji wa hizi data.
So next question ni uchapishaji wa hizi data ukoje? Nikitaka kuzipata ni rahisi, au ndo nenda urudi kesho?
 
Wataalamu wanatakiwa kuboreshewa maslahi yao,wanaumuhimu sana katika kuendeleza nchi lakini wanavyopuuzwa ndio maana wengi wanahama nchi na kwenda kutumikia nchi zingine hiyo ni brain drain,unasomesha kwa gharama kubwa wataalamu halafu huwajali hasara mara kumi
 
Kuna Umuhimu mkubwa sana wa Tanzania kujali wasomi wake. Kutokana na kutojali wasomi ndio maana unakuta Prof and Dr wako kwenye siasa badala ya kuwa kwenye Academic/Research institutions. Tanzania inaweza kwa kiasi kikubwa tu kutoa funds kwa ajili ya Reseach mbali mbali ambazo zinaweza kutuletea maendeleo. Serikali inatumia pesa nyingi sana kwenye Political Issues.
 
Sina uhakika kama kuna thread hii tayari, lakini nilikuwa nawaza; Kwa nini Tanzania tunashindwa kupiga hatua za maendeleo?

Moja ya jibu nililoweza kupata ni serikali kutofadhili wasomi. Mara nyingi katika nchi zilizoendelea, serikali zinatoa pesa kwa vyuo kwa kusudi la research. Mifano hai hii hapa: Stanford, Princeton, Cambridge, nk.

Research hii inasaidia kuangalia matatizo na hata kutafuta solution ya hayo matatizo yanayokumba jamii na nchi kwa ujumla.
Tatizo ninaloliona Tanzania (kwa maoni yangu) ni watu wengi kuenda nje ya nchi kwa ajili ya research. Tatizo la mtindo huu ni hizo research kutokuwa 'targetted' katika maendeleo ya nchi yetu.

Kwa nini serikali zisingeboresha hili jambo? Kama huu ufadhili upo, je unapatikanaje? Ni open process au ndo ile ya kibongo kwa rushwa na upendeleo?
Pia publication ya hizo research inafanyika na kwa uwazi kiasi gani? Au ndio zinakusanya vumbi tu? Nadhani siasi zimekithili sana nchi zetu kuliko utendaji.

Wanajamii mnaonaje hilo?
ni jambo zuri kufadhili utafiti kwa ajili ya maendeleo endelevu ya nchi.

tatizo lililopoo hata hizo zilizifadhiliwa uwasilishi wake na utekelezajiii bado ni tatizoooo kubwaa.

tuna taasisi zinaziheshimika kwa utafiti kama UDSM, ESRF, NIMR, REPOA, muchs, nk ila sijaona role ikoje katika cordination yake???

COSTECH vipi wao ni centre for cordination of research au kwa kuwa ni taasisi ya umma kama nyingine ni KICHAKA CHA UBABAISHAJI????
 
Kuna Umuhimu mkubwa sana wa Tanzania kujali wasomi wake. Kutokana na kutojali wasomi ndio maana unakuta Prof and Dr wako kwenye siasa badala ya kuwa kwenye Academic/Research institutions. Tanzania inaweza kwa kiasi kikubwa tu kutoa funds kwa ajili ya Reseach mbali mbali ambazo zinaweza kutuletea maendeleo. Serikali inatumia pesa nyingi sana kwenye Political Issues.

Si ndo hilo hata mimi naliona. Wewe angalia hela mmbunge anayopata, alafu angalia na hela inayowekwa katika elimu. Yani tumerudi nyuma sana kutokana na hili. Watu wengi sana wenye uwezo, wanakuwa frustrated na system nzima bongo. Yani mtu ukitoka nje kuja Tz, unaweza kuacha kazi kabisa. Maana kama umezoea uwazi, kwa mfano upatikanaji wa data na hata utumiaji wake, basi bongo hilo ni sifuri. Vitu vinaendeshwa na siasi badala ya wasomi wenyewe. UJINGA wa kwanza ndo huo! Na hili ni Nyerere ndo alilikuza. Hakutaka watu wenye akili waje kum-challenge. Akaleta ofisi ya chama kweli kila organisation. Hapo ndo aliiua nchi kabisa. At one point...we have to speak the truth! Baba yetu wa Taifa hakuwa tunavyosema alikuwa!
 
Back
Top Bottom