Maelezo ya Diwani wa CHADEMA alivyotengenezewa kesi ya Kuteka

Basil Lema

Member
Jan 20, 2013
86
277
MAELEZO YA MHE. DIWANI HILDA WOISO (VITI MAALUM) CHADEMA ALIVYOKAMATWA NA POLISI KWA KOSA LA KUTEKA.

Mimi nilisafiri kuanzia Jumatatu25/3/2013 kwenda kuhubiri injili Simanjiro. Nilikuwa na mkutano wa injili na semina kwa wakristo niliondoka kituo cha Mbuyuni muda wa saa 10. mikutano hii ilipangwa kufanyika kwa siku 6. Nilifika salama na kupokelewa na mwenyeji wangu Mch. Bomba wa FPCT Simanjiro Kijiji cha Ngorika A.

Huduma ilienda hadi siku ya Jumapili tr. 30/3/2013 jioni saa 12.30. Baada ya kufunga mkutano nilienda kulala kwa mama Michael akaaye pale pale Ngorika A.

Tr. 1/4/2013 nilianza safari ya kurudi nyumbani Moshi mjini mtaa wa Mnazi saa 12 asubuhi. Nlifika Mjini eneo la Kiborloni saa 3.30 asubuhi. Nilikuja kwa usafiri wa basi la Sahara ambalo nililipakia Mwanga Mjini.

Nliposhuka kwenye basi nikapokea simu kutoka kwa mume wangu Evans Roman Woiso akaniuliza uko wapi? Nikamjibu niko Kiborloni. Akanimbia kwamba kuna watu wako huku nyumbani ambao wamejitambulisha kuwa ni askari polisi. Wamesema wanakutafuta wewe. Wanasema wewe umeficha pampu za bomba za maji nyumbani kwako. Akaendelea kusema wamekwishapekua nyumba nzima lakini hawakukuta vitu hivyo. Kwa mujibu wa mume wangu upekuzi huo ulikuwa usio makini wa muda usiozidi dakika 10.

Wao wenyewe wakasema hakuna chochote katika hivyo walivyotaja bali wakasema kwa sasa tunataka tu kuonana na Mhe. Diwani Woiso.

Mume wangu akawauliza kwa nini mumekuja kumpekua Mhe. Diwani na kumsingizia maneno ya uongo? Hamuoni kwamba mmemdhalilisha sana Mhe. Diwani ambaye pia ni Mchungaji? Ninyi pia mmejidhalilisha kwa kumsemea uongo.

Wakamwuuliza mkeo yuko wapi? Akawajibu kuwa nilikuwa safarini na sasa nimerudi na nimeshafika Kiborloni. Wakamwomba awape mtoto ambaye ataenda nao hadi hapo Kiborloni mahali nilipokuwepo. Mume wangu akawapa binti yangu atwaye Doreen. ambaye ana umri wa miaka 20 akawaleta nilikokuwa akiwa ndani ya gari ambaye aliitambua kwamba ndiyo inayotumiwa na CID wa Moshi.

Nlipokutanishwa na hao askari polisi walinieleza kwamba wao wananitafuta kutokana na habari walizozipata zilizokuwa zikinituhumu mimi. Lakini baada ya kufika kwako na kukupekuwa tukagundua kuwa hizo habari si za kweli. Kwa kuwa niloipata shaka nikawauliza Je ilikuwaje mkafikia huko? Je mwajua mimi ni nani? Wakanijibu kwa ujasiri kabisa kwa kuniuliza. Tunakujua. Kwani wewe si ni Mchungaji? Na wewe ni Diwani wa CHADEMA. Na ya kwamba umetoka sasa hivi Simanjro kuhubiri injili? Nikawaambia "ndiyo.
Wakaniambia hata hivyo pamoja na kutokukuta lolote, sasa unatakiwa kwa RPC kuna mambo anataka akuulize. Sisi hatuwezi kukuuliza. Wakaniuliza. Au una mashaka? Nikawajibu Ndiyo" wakatoa vitambulishao vyao nikaona kweli wao ni maaskari. Nikawaomba basi nipeleke tu haya mabegi nyumbani. Wakaniambia hapana twende tu mara moja halafu utarudi ukiishajibu hayo maswali. Wakanichukua mimi na binti yangu wakanipeleka ofisi ya Mambo ya Ndani mjini Moshi.

Tulipoingia ndani wakamwambia binti yangu abaki nje. Mmi nikaingizwa ndani na kupandishwa ghorofani. Nikaingizwa ofisi ambayo mlango wake uko opposite na ofisi ya RPC. Nlipoingizwa pale tukasalimiana vizuri na kuanza mazungumzo mazuri tu ya kuheshimiana. Tukijadili kuhusu safari yangu ya injili. Nilikaa ofisini kwake kama dakika 30. Wakanichukua pamoja na wale walionichukua Kiborloni wakanipeleka kwa RPC.
RPC akanikaribisha vizuri, tukasalimiana.... Ndipo aliponiuliza Je unamfahamu SAMWELI. Nkaduwaa. Akaniuliza tena unamfahamu Samweli, nikaduwaa tena. Aaniuliza kwa nini hunijibu. Nikamwambia mimi ninashindwa kukujibu kwa kuwa ninawajua Samweli wengi.
Nikamwambia niulize swali ambalo linafaa kujibiwa. Wakanifokea kwamba "unamjibu hivyo mkuu" na yeye akaanza kunifokea. Na mimi nikamwambia hebu sasa unaiambie umeniita hapa kufanya nini? Akanijibu kwamba ataniambia. Akaanza kwa kusema " kuna askofu mmoja ametekwa. Hadi sasa hajulikani aliko bali yuko kwako na ni wazi kwamba yuko kwako." Nikamjibu si kweli. Na kuendelea kumwambia " simjui na wala sifahamu aliko" akaniuliza ulishawahi kusikia habari za askofu wa Njombe akiwahi kutekwa? Nikamjibu " sijawahi kusikia. Akauliza hujawahi kusikia hata kwenye vyombo vya habari wala magazetini. Nikajibu " hasha" akaniambia "sasa huyu askofu utamleta. Kwa kuwa unasema uongo eti hujui aliko" nikaonyesha hasira. Akaniuliza kwa nini unakasirika?" Nikamjibu nimekasirika kwa kuwa unasema uongo na huwezi kuthibitisha uongo wangu na nina njaa. Akasema mimi ninasema ukweli. "Huyu askofu ulichart naye tarehe 29/3/2013 saa 10 jioni. Akasema hebu lete simu yako, hata hivyo nikakumbuka kwamba siku hiyo nilicharge simu yangu kidogo na kupiga simu nyumbani kwangu. Nilipomaliza kuongea tu na binti yangu ikaingia simu ya mtu nisiyemjua. Akaniita Hallow. Kisha simu ile ikakatika. Na mimi kwa kuwa nilikuwa na shauku ya kujua mambo ya nyumbani nikapiga ile simu na upande wa ,pili akaniuliza je kuna uwezekano wa kupata chumba cha biashara Kiborloni? Kabla sijamjibu ikakatika na charge kwenye simu yangu ikaisha.

RPC akachukua simu yangu akaanza kubonyezabonyeza. Nikakataa kwa kumweleza kuwa asifanye lolote kwenye simu yangu kwani siwezi kubambijkizwa kesi. Wale askari wenzake wakanijia juu wakisema unafikiri mkuu anaweza kukubambikiza kesi?" Nkawaambia kuwa RPC si Mungu aweza kufanya kosa lolote. Hata hivyo aliweka simu yangu mezani na kusema yafuatayo: " sisi tunajua kuwa wewe ni mtu mkubwa. Ni diwani na ni mchungaji. Hatutaki kukuchafulia wala hatutaki kukudhalilisha. Ili tusikuchafue wala kukudhalilisha tuambie ukweli kwamba huyo askofu yuko wapi" nikawaambia sijui aliko wala simfahamu. Na sina lugha nyingine ya kukuelezea ili uamini kwamba ninayosema ni ya kweli, lakini kwa hakika ninayosema ni kweli.

Ndipo ghafla wakaleta karatasi yenye rekodi ya matumizi ya simu yangu kuanzia tarehe 1/3/2013 hadi 30/3/2013. Akatoa pia karatasi nyingine yenye rekodi za matumizi ya huyo askofu ambaye inasemekana kwamba ametekwa kwa siku hizo hizo. Akanionyesha namba yangu na kuniuliza: Je hii ni namba yako? Nkamjibu Ndiyo. Na akanionyesha pia ile ya anayetajwa kuwa ni askofu.

Wakanionyesha namba ile ya yule askofu kwenye chart yangu na kuniuliza Je huoni unatudanganya? Hii namba si imewasiliana na wewe tr. 29? Nkawajibu ni kweli hii namba ilinipigia kuniuliza kama ninaweza kumpa fremu pale kwangu Kiborloni. Nlipomwuuliza huyu mpiga simu kwangu kwamba yeye ni nani alinijibu kwamba nisitake kujua yeye ni nani bali nimjibu kuhusu fremu. Nlipotaka kumjibu simu yangu ikaisha charge. Nkawaambia kwamba huyu si askofu kwani hakujitambulisha kama askofu.

RPC akasema mama tunakwambia kwamba mtu huyu unamjua kwa nini simu yake iko kwako? Ilinishangaza kwamba mawasiliano yake na mimi hayaonyeshi wakati aliponipigia bali pale nilipompigia tu. akaniambia kuwa tutakaa na wewe hapa hadi useme ukweli na umlete huyu askofu. Usifikiri kuwa tumekurupuka" tumekuchunguza siku nyingi. Tumekufuatilia sana. Tunajua mengi kuhusu wewe.

Akawaita wale CID akawaambia wakanichukue maelezo. Wakati huo huo wakahakikisha kuwa simu yangu hawanipi na kuhakikisha kuwa siishiki simu yangu. Na kila simu yangu ilipoita waliikata na kuniuliza huyu apigaye ni nani!

Wakanichukua nikatoe maelezo. Wakaniletea fomu ya maelezo na kuniuliza kama ninataka awepo mtu mwigine ili ahakiki maelezo ninayotoa. Nikawaambia Ndiyo. Nileteeni Mstahiki Meya. Wakaniuliza yuko wapi. Nkawaambia waangalie kwenye simu yangu. Wakatoka nje ili wampigia wakarudi ndani wakasema Jafari hapatikani. Baada ya kumkosa wakasema basi "tunatafuta gari tumfuate nyumbani kwake" nilipoona kwamba wananipotezea muda na hivyo ningeweza kulazwa rumande, nikawaambia ni vyema mnihoji nikiwa peke yangu kwani haina tofauti yoyote?

WKaniuliza " wajua kwa nini uko hapa? Nkajibu Ndiyo. Inaonekana kwamba nimeletwa hapa kwa tuhuma za huyo askofu aliyetekwa. Wakaniuliza pia Je huyu mtu aliyekupigia simu alipata wapi namba yako? Nikawaambia kwamba nimeacha namba pale kwa binti anayeuza pumba na kinyozi hapo hapo ambao wote wamepanga fremu kwenye jengo langu pale Kiborloni. Wakanichukua na kwenda nami hadi Kiborloni kwenye jengo langu kukagua kama kweli niliyosema ni kweli. Waliangalia wakiwa kwenye gari tu na kujihakikishia kuwa yote yalikuwa kweli tupu. Wakageuza gari tukaondoka na kurudi ofisi ya Polisi. Maelezo yakakomea hapo na kuniambia kwamba nitakaa nao hadi uchunguzi utakapokamilika. Tukarudi ofisini mjini na kukaa kama dakika 10 nikawaomba niwapigie nyumbani kuwaeleza kwamba niko huku nimeshikiliwa. Wakakataa wakisem kwamba tukikuruhusu uzungumze na watu wKo utazidi kumpiteza huyo askofu.

Ilipofika saa 10 wakaniingiza kwenye gari na kunipeleka hadi Sango. Halafu wakanirudisha tena mjini. Tukakaa tena kama dakika 10 ndipo wakanichukua tena na kunipeleka kituo cha polisi Himo. Hiyo ilikuwa kama saa 11 jioni. Pale nikaingizwa rumande, nikavuliwa viatu, nikapekuliwa na kuingizwa sero. Wakaondoka hatimaye wakarudi tena muda wa saa 12.30. Wakaniambia hivi. Huyu askofu yuko hewani sasa. Sasa tunataka umpigie uongee naye" nikapiga kweli na yule askofu akapokea simu, askari wakanniambia ongea naye. Nkawauliza niongee naye nini? Wakaniambia ongea naye kuhusu ile fremu. Nikaongea naye ukweli na kumwambia mimi ni yule mchungaji uliyetaka kuongea nami kuhusu fremu. Akanijibu Hallow mama mchungaji ni mimi lakini nimeshapata fremu" nikamwambia hata hivyo mbona mimi fremu -zangu nilikuwa ninapangisha kwa bei nzuri tu? Njoo tupatane bei nzuri. Akaniambia kwamba hapana tayari nimeshapata. Basi nikamwambia hata hivyo mtumishi wa Mungu wewe ni askofu na mimi ni mchungaji, nina matatizo na majaribu mengi nilitaka kuonana na wewe ili unishauri na kuniombea. Yeye akanijibu "" mimi nimeshaondoka Kiborloni na nimeshaenda Arusha siko tena huku. Nikamwambia sio lazima leo niambie tu nitakupataje? Hata kama ni Arusha nije. Simu yake ikakatika na haikupatikana tena.

Nnakumbuka pia kwamba RPC aliniuliza hapo awali kwamba je waweza kuitambua na kufananisha hiyo sauti ya mtu uliyeongea naye kwenye simu? Nlihisi kwamba sauti ile ilishabiiana sana na ya RPC. Nkataka kumwambia hivyo lakini nikaamua kutosema kwa hofu ya kutendwa mabaya.

Baada ya kuzungumza na yule aliyejimbulisha kama askofu nikawaambia. Naomba niwasiliane na nyumbani. Wakakataaa. Nkawaambia kwamba mume wangu ni mgonjwa akisikia ninachopitia ataumia sana na anaweza kupatwa na makubwa.

Wakawa wanafanya mizaha na mimi kwa lugha ya Kiingereza. Baadaye wakaniambia kwamba Mama Mchungaji umetudanganya. Je wewe iliposema wewe ni darasa la saba je hicho Kiingereza umekijulia wapi? Sasa tumeshauliza tukaambiwa kwamba wewe umesoma hadi Form 4 na kaendelea na masomo hadi kupata Diploma ya uongozi kwenye chuo ambacho kina makao makuu Marekani na kina tawi Morogoro.

Wakanirudisha rumande. Wakaenda kuniletea chakula na maji wakaondoka. Walinileta chips mayai na soda na maji. Kwa kuwa pale kulikuwa na harufu mbaya na ni pachafu sikuweza kula. Kinachonisikitisha sana ni kwamba nikiwa pale na baada ya kutambulishwa kwamba mimi nimeletwa kwa agizo la RPC hakuna hata mtu mmoja aliyethubutu kuongea na mimi. Yupo ndugu yangu polisi aliyekuwa pale kituoni kwa namna ilivyotambulishwa hakuthubutu kabisa kunisogelea.

Ndipo nikamwita askari mmoja nikamwuliza Je kwa cheo changu ni halali mimi kuwa mahali kama hapa. Wakanijibu hatujawahi kuona mahabusu akichagua mahali pa kukaa. Nikawaambia kwamba kama mimi niko hapa kama mahabusu basi nipelekwe mahakamani ndani ya saa 24. Vinginevyo kama niko hapa kwa kesi ya kuchunguzwa nipewe chumba tofauti. Ndiyo maana naona mnanizuia kuwasiliana na watu wangu. Hata ndugu zangu wanakatazwa kuniona. Mahabusu waliposikia hivyo wakapiga kelele wakisema "afadhali mhe. Diwani umekuja uone tunavhoteseka. Ukitoka huku ukatutetee uraiani. Nilikuta wapo mahabusu waliokaa rumande siku 10.

Mmoja wa askari akamwita yule niliyekuwa naongea naye na kumwambia " wewe hujui kuwa huyo mama unayeongea naye ameletwa hapa kwa agizo la RPC. Usithubutu kuendelea kumsikiza. Utaingia matatani. Wakaleta chakula usiku. Wakanikaribisha nile. Nikakataa. Wakawapa wale mahabusu wengine na kuwaambia wale. Kile chakula kilikuwa kama share ya watu 2 ambacho walitakiwa watu 10 wakile.

Nikalala rumande usiku ule na hadi kesho yake saa 7 mchana ndo wakanileta Moshi Mjini kwenye ofisi ya RPC. Pale wakaniambia kwamba mama kutokana na tuhuma ulizo nazo hatuwezi kukuachia hivi hivi. Nikawajibu. " mimi ni mtumishi wa wananchi pande mbili. Ninawahudumia kiroho na kama kiongozi wao kimwili/kisiasa. Mnapoendelea kunishikilia hapa mnawanyima huduma /utumishi wangu kwao.

Hata hivyo kwa maelezo uliyotupa tumeona kwamba maelezo yako hayatoshelezi kumpata huyo askofu. Lakini tutakupa dhamana uende nyumbani kwa familia yako.
Nlitoka kituoni nina hali mbaya kiafya. Askari wakaniuliza mbona unaoneka una hali mbaya nikawajibu kwamba ninaumwa shingo, kifua kinabana na kichwa kinauma.

Nikadhaminiwa na kuniagiza niripoti tena kituoni tarehe 3/4/2013. Nlipofika kituoni leo waliniambia kwamba "aliyekuambia uje leo alikosea bali tutakapokuhitaji tutakupigia simu. Basi nikaondoka


My Take:
1. Rekodi haionyeshi mawasiliano ya zaidi ya mara moja. Mawasiliano haya ambayo yameonyesha wazi kwamba huyu mtu aliomba fremu na aliendelea kuzungumzia fremu je utekeji hapo uko wapi.
.
2. Mchungaji mwanamke mwenye ndoa yake ya Kikristo anawezaje kusemwa kwamba amemteka Askofu mwanaume mwenye ndoa yake. Je huku si kunidhalilisha sana?

3. Hakuna askofu so far aliyetekwa!!!

4. Kama polisi walitaka kuonyesha umakini kwa nini hawakuchukua mazungumzo baina ya diwani wetu huyu na huyo askofu.

5. Kwa nini askofu huyo alipozugumza na huyu diwani kwa polisi hawakuagiza kampuni ya simu isionyeshe huyo askofu anaongelea kwenye mnara upi wa simu.

HUJUMA DHIDI YA CHAMA
1. Kwa nini walimzuia diwani kumpata meya asikilize maelezo yake mbele ya polisi.
2. Kuitwa kwa wandishi wa habari kwa RPC mara tu Mhe. Woisso alipoletwa kutoka Himo kwa lengo la kutengenezwa kwa habari chafu dhidi ya CHADEMA.
3. Kum-arrest Mhe. Diwani bila kupeleka taarifa kwa Mstahiki Meya na Viongozi wa chama ni kinyume cha sheria.


Waheshimiwa ninajiridhisha sasa polisi wameamua kuwa idara ya utekelezaji wa propaganda za CCM dhidi ya CHADEMA. Tunaelekea wapi Tanzania?
 
Hivi haiwezekani binadamu akawa ni mwanchama wa chama cha siasa lakini pia akawa muovu? Kwa nini tusifanyie kazi maneno ya naibu katibu mkuu wa CDM kuwa maovu ya mtu mmoja yasitumike kukichafua chama.
 
Hizi ndizo changamoto za kutufanya tuikatae serikali hii na kuibadili ufikapo uchaguzi ujao. Utawala huu unakuwa si wa kisheria tena, bali kulinda watawala kwa kudumaza demokrasia. Ukisoma habari hii unaona kila dalili za serikali kandamizi.
 
Kwa ufupi mama huyo hakutendewa haki hata kidogo.Na RPC pamoja na askari wake hawakumdhalilisha huyo mama tu bali wanawake wote.Swali la msingi kwa nini polisi hawakumuita huyo askofu aliyepotea katika mazingira ya kutatanisha ili naye ahojiwe?Tusitee maovu yanayofanywa na mamlaka tulizowapa majukumu ya kutulinda.Kwa kweli inatia kichefuchefu,mpaka hapo hakuna serikali yetu inatafuta matatizo.
 
"watapigana nanyi lkn hawatawashinda kwa kuwa mimi MUNGU nipo ili niwaokoe"
CDM MUNGU ATAWAVUSHA KAMA MNA DHAMIRA YA KWELI YA KUWAKOMBOA WATANZANIA,LKN KAMA PIA MNAWAADAA WANANCHI VIVYO HIVYO MUNGU ATAWAPIGA,NA PIGO LITAKUWA NI PIGO KUU KWANZIA KWA MKUU WA CHAMA MPK WA MWISHO
 
aisee kama mwanamke kwa haya madudu mliyofanya mnazidi kunishawish nianze siasa ndan ya ukoo wangu kuiunga mkono chadema.totally hata kwa tusiokuwa wapenz wa siasa ccm mnaboa
 
CCM wanaitumia vibaya idara ya Polisi na Usalama wa Taifa, lakini lazima wakumbuke Watanzania wasasa siyo wa miaka ya 80, ipo siku watachoka tu maana hizi hila zipo wazi sana, na siku Watanzania wakichoka ndiyo utakuwa mwisho wa kuiita Tanzania kama kitovu cha amani
 
Mwigulu kwa njama zake za kigaidi ataliangamiza taifa. Kila walichokipanga ccm kupitia vyombo vyake vya dola kitashindwa vibaya. Hii ni kwa sababu Mungu yupo upande wa umma wa watanzania na shetani yupo ni kikundi cha watu wachache waovu wanaojiita serikali. Wanaojitolea kwa hali na mali kuutetea ukweli zidi ya njama za kigaidi ni watu wenye mapenzi mema na nchi hii dhidi ya wachache wachumia tumbo waliokubali kununuliwa kutengeneza uongo kwa nia ya kubambika. Wananchi wa leo sio wale wa 47, na kutumia propaganda za enzi za kale ni kujiweka uchi mwenyewe hadharani. Hilo ndilo wanalofanya ccm kwa maelekezo ya mwigulu. Mkitumia nguvu kubwa kutatua matatizo ya wananchi kama mnavyoitumia kutengeneza propaganda dhidi ya chadema mngelikuwa na nafuu sana na kukubalika angalau kwa wastani. Sii vinginevyo.
.
 
Inasikitisha sana, ila ipo siku huu ukatili wa CCM naserikali yake utafika mwisho.
 
Pole mama kwa udhalilishaji, Mbowe alisema wako wengi waliouawa, kufungwa na kuteswa kwa ajili ya CHADEMA. Haya maCCM hayafai
 
Pole mama kwa udhalilishaji, Mbowe alisema wako wengi waliouawa, kufungwa na kuteswa kwa ajili ya CHADEMA. Haya maCCM hayafai, tutafika tu
 
Ukombozi unakaribia, Ki ukweli safari ni ndefu sana aise! ila TUMESHAFIKA
 
Hapana, hapana, hapana this is too much. Hata hivyo, wanazidi kuthibitisha kile tulichokwishatonywa siku nyingi kwamba kinakuja na bado mengine yanapikwa.
Huwezi kuzuia mabadiliko kwa kutumia polisi any way. Hata walioua enzi za ukoloni hawakuweza, seuse leo.
 
Hakuna njia rahisi kufikia ukombozi kamili, tukaze boot. Tuendsko si mbali
 
police nasema siku zote wanatumiwa
au ni vilaza wa sheria..
huwezi kumtaka mtu kituoni bila kumweleza unamwitia nini
huwezi kuchukua maelezo ya mtu bila kuwa na wakili wake
walichofanya polisi ni kitu cha kijinga kabisa tena RPC
shame upon them
labda wanadhani wako juu ya sheria...
kuna haja kureshufle jeshi zima la polisi.

wanadhani labda wananchi wamelala hawajui haki zao
ukombozi wa misri,tunisia na kwingineko polisi hawakuweza kuzuia nguvu za umma
tena hawa polisi tunaishi nao mitaani ipo siku watajuta kutumiwa kwa maslahi ya wachache
 
Back
Top Bottom