Maelezo namna ya kutatua migogoro ya muungano kwa kuwa na serikali 2 au 3

FRELIMO

Member
Apr 12, 2014
42
4
Kama mtanzania ninapata shida kutambua migogoro ya muungano iliyopo na utatuzi wake lakini niliamini wajumbe wangenipatia majibu ya maswali yangu kupitia wale wa hoja ya serikali 3 na wale wa serikali 2 lakini imekuwa kinyume zaidi nachopata ni serikali 2 ndio mwarobaini wa muungano na utatuzi wa kero zake ila hawaelezi jinsi gani watatatua kero hizo na kwanini walishindwa kutatua toka mwanzo mpaka kufikia miaka 50 ya muungano.

Wale wa serikali 3 nao hawaelezi bayana kero ni zipi na zitatatukaje na kuwa hii serikali ya 3 itapata wapi mapato ya kuiendesha na vp hatma ya watanganyika walio ZNZ na wazanzibar walioko Tanganyika,majeshi yataendeshwaje.

TAFADHALI NAOMBA NIFAHAMISHWE KERO ZINATATUKAJE KWA WAUMINI WA PANDE ZOTE.badala ya kusema mi nataka serikali 2 au 3 bila kueleza faida na jinsi ya utatuzi wa changamoto zilizopo na zitakazojitokeza.AM OUT!
 
Soma ripoti ya Warioba pamoja na randama yake. Humo imeelezwa bayana jinsi kero zilizopo zitatatuliwa na uwepo wa serikali 3
 
Back
Top Bottom