Madudu mengine ya Mali Asili na Utalii haya hapa; Kagasheki kazi unayo!

pilipilimanga

Member
Aug 10, 2012
5
0
Nimepenyezewa document hii (check attachment) kutoka jengo la ''MPINGO HOUSE'' na mfanyakazi mmoja aliyejiita ''MWENYE HURUMA'' kwamba kunawafanyakazi wenzao wanaofanya kazi WAKALA iliyopo wizarani kumwandikia barua Waziri wa sasa KAGASHEKI mara baada ya kuteuliwa lakini matatizo yao yanawekwa kapuni.

Kwa mujibu wa mtoa taarifa huyo, Wafanyakazi hao wamekuwa na matatizo makubwa na mwajili wao kwa miaka mingi na wamekuwa wakitoa malalamiko kwa barua (zinazoweza kujaza kontena) lakini inaonekana wizarani wanaohusika na wafanyakazi hao wameweka ''SUPA GLUU'' masikioni.

Anadai zilishawahi kuwa kwenye tume mojawapo na alichokiona ni wakubwa wa wizarani KU-IGINOA na HUWEKWA KWENYE DUST BIN ripoti za tume.

MOJA YA MADAI YAO AMBAYO ALIYAONA KAMA MJUMBE WA TUME AMBAYO ILIKUWA NI KILIO CHA WAFANYA KAZI HAO NI KUTOKULIPWA MISHAHARA YA WAKALA NA KUPATA NYONGEZA YA MISHAHARA YA MWAKA NA KUPANDISHWA VYEO. Anadai, tokea aanze kufanya kazi hajawahi kukutana na case za ajabu kama hizo.

Namnukuu ''Wale wafanyakazi ukiwaona nyuso zao ni kama wagonjwa. Yaani they are frustrated. Ajabu Wizara taarifa wanazo juu ya matatizo ya huo Wakala lakini haichukui hatua. Hawawafanyii fair kwa maoni yangu''....mwisho wa kunukuu.

Kama mtu wa ''HURUMA'' alinipenyezea niiweke huku kwa 'GREAT THINKERS'' wamsaidie KAGASHEKI kushauri afanye nini.
 

Attachments

  • malalamiko-maliasili.pdf
    184.1 KB · Views: 348
Huyu ndo hawezi kabisa hii wizara
Huyu anakazi muhimu sana ya kulinda maslahi ya wakubwa waliomuweka pale.

Hilo swala la kushindwa ama kuweza wala sio dili siku hizi ni mwendo wa kupeana ulaji tu! Kwani yule kijana NW wa Nishati na Madini anaweza nini?
 
mbowe kasema watz tuache kulalamika,grab your machete,i grab my rifle..let's kick the thieves outta office
 
Duh inasikitisha sana. Hivi kuna kansa ya kuunda Tume kufuatilia mambo fulani halafu ripoti inaishia kwenye makabati? Imeona ofisi za wakala Lushoto zikizorota siku hadi siku. Kumbe kuna mambo makubwa sana chini ya zulia.
 
Pamoja na mambo mengi tatizo jingine pale TTSA ni la kisera, mashirika mengi ya mbegu za miti kusini mwa Africa yaliyo chini ya serikali yamedorora. Ukienda Zimbabwe, Zambia n.k. hali ni ile ile tu. Ni vizuri kufikiria decentralization of seed and seedling systems!
 
Mimi nauliza swali je mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro ni mali ya ccm? Maana zipo tetesi kwamba kama vile walivyopora viwanja vya mpira pia ngorongoro ni mali yao na ndiyo maana inasimamiwa na makada wa mafisadi kina Msekwa, naomba kujuzwa wakuu.
 
matatizo ya kuwekana au kupeana kazi kishikaji ndio haya. Huyu jamaa ni msanii tosha na ccm yake
 
Mimi nauliza swali je mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro ni mali ya ccm? Maana zipo tetesi kwamba kama vile walivyopora viwanja vya mpira pia ngorongoro ni mali yao na ndiyo maana inasimamiwa na makada wa mafisadi kina Msekwa, naomba kujuzwa wakuu.
kwa hifadhi zote hujui kuwa zinasimamiwa na ccm? hawa jamaa walishatuweka watanzani kama ni wajinga. nilikuwa mbunga ya sellu yaani ukisika ambulance inapita jua wanyama wanapelekwa moro kwa Abood kuuzwa yani ana kiranch pale dakawa watoto wa simba, chui, etc wakikamatwa lazima apelekewe
 
In short inaoneka wizarani wanakula na uongozi. Mtoa taarifa ukitafakari maoni yake utangundua kitu..na tukisoma nakala utaona kuna matatizo pia. Kama kweli Waziri wao kaipata barua na kanyamaza basi labda nae anataka WAGOME maana siku hizi ndo umekuwa mtindo ukitaka haki. Hivi ofisi ikiwa wakala mishahara inabadilikaje?
 
Nilimsikiliza Kagasheki akijibu hoja za Wabunge wakati akihitimisha mjadala wa bajeti kwa wizara yake. Nilisikitika He sounds like any other stupid in the american film.

Yaonekana hakuzoea kusifiwa maana alikuwa naibu waziri kwa muda mrefu kwa umri huo. Sasa anadhani kapewa nafasi ya kuonyesha akili yake.

Barua kama hii alikataa kabisa kwamba eti wabunge wakizipata wamfuate watete na mbunge. Sijui kama anafahamu nini kazi ya mbunge? Bunge lenye wabunge zaidi ya 300 anataka wamfuate. Taarifa mbovu za wizara yake zikiwafikia wabunge eti wamfuate! Tena kwa majivuno kabisa!

Nonsense old man.
 
kwa hifadhi zote hujui kuwa zinasimamiwa na ccm? hawa jamaa walishatuweka watanzani kama ni wajinga. nilikuwa mbunga ya sellu yaani ukisika ambulance inapita jua wanyama wanapelekwa moro kwa Abood kuuzwa yani ana kiranch pale dakawa watoto wa simba, chui, etc wakikamatwa lazima apelekewe

CCM ni tatizo la nchi. CCM inachukuwa pesa kila kona. Nasikia hadi COSTECH. Hawana uwezo wa kuendesha chama kwa kutegemea mgao wa hazina. Kinachotokea ni kupitia taasisi kama hizi na kuchota pesa. Hata halmashauri wanazisumbua kuliko kipimo.

Wanachosahau ni kwamba wakisha muhusisha mkuu wa taasisi kama hapo Ngorongoro, Kinachofuata mkuu huyo naye atachota maana kisha pata sababu. ndo yanayofanyika na it's a chain rule.
 
Kumbe kiongozi wa taasisi inayolalamikiwa amekuwa pale tokea 1992 wakati taasisi ikiwa chini ya DANIDA. Ilipogeuzwa kuwa WAKALA 2001 na tokea hapo amekuwa CE. Katika uongozi wake inasemekana watu wamekuwa wakinyanyaswa utadhani kampuni binafsi. Hataki kukaa na watu vichwa anaona watamchalenge,kwa mujibu wa mtoa taarifa asilimia 80 ya wafanyakazi ni std 7.
 
Jamani,hivi kwa uozo ulioonyeshwa na barua ya hawa wafanyakazi kiongozi wa hivyo anaweza kuomba kuongezewa mda? Sasa ni hivi,jamaa kumbe alishaomba kuongezewa mda tena. Imefahamika anatakiwa kustaafu mwezi mda wowote toka sasa. Hivi atakayehusika na hili jipya ni waziri au ofisi ya utumishi? Balozi kagasheki alisema apelekewe taarifa kama hizi,nadhani anazo hkika. Wakimwongezea mda hao wafanyakazi nadhani watajimeza..
 
Back
Top Bottom