Madiwani wapya msikubali ujinga uwazoee katika mabaraza yenu

Mwl wa akiba

Member
Nov 12, 2020
66
66
MADIWANI WAPYA MSIKUBALI UPUMBAVU UWAZOEE KATIKA MABARAZA YENU.

Naandika Mwl wa akiba

📌Madiwani wapya ambao wengi wameapa katika kipindi hiki lazima watambue kuwa kuna vikundi vya watu wachache katika halamshauri zetu ambao wanatabia ya kuhujumu fedha za umma kiujanja ujanja tu.

📌 Madiwani wetu wasione aibu kuomba ushauri wa kitaalamu katika maeneo ambayo hawana ubobezi kuliko kupitisha mambo ambayo hayaleti tija katika jamii kwa upambavu tu wakutokuuliza ili wapate ufafanuzi mzuri.

📌Madiwani lazima watambue hivyo vikundi vya watu wachache wasioitakia mema wananchi huwa wanatumia lugha za kitaalamu katika kuiba na kuwadanya madiwani wetu hivyo kama madiwani wasipokuwa makini basi lazima wananchi wataendelea kuibiwa tu.

📌Madiwani tumieni wataalumu wetu bila kujali tofauti za itikadi zetu za kisiasa katika kutafuta ufafanuzi na uchambuaji wa mambo ili kukabiliana na vikundi vichache vyenye roho za kishetani katika halmashauri zetu .

📌 Nimpongeze Mh. Msukuma na madiwani kwa kusimama kidete katika kuhakikisha fedha za wananchi wa halmashauri ya Geita zinatumika kiuweledi .👏🏿👏🏿👏🏿👏🏿👏🏿👏🏿👏🏿👏🏿

NB: ZAMA ZIMEBADILIKA SIO KILA HOMA NI MALARIA

Ndugu yenu.


Mwl, wa Akiba
 
Madiwani gani unawapa ushauri huu? Hawa wasiojua hata kusoma?

 
Hao madiwani wenyewe wamepata udiwani kwa kura za wizi na utoaji rushwa, watapata wapinzani uwezo wa kuhoji wizi?
 
Madiwani wawapi unaowapa ushauri wa CCM au Lahaula! Unapoteza muda CCM ya sasa hivi haishauriki unajisumbua bure tu Babu.
 
Wewe naona huelewi Serikali za Mitaa vizuri. Wenye matumizi mabaya ni madiwani. Wanaowajibika kwenye matumizi na mapato ni watendaji, wanaojibu audit query ni watendaji.

Watendaji ndiyo wahangaika na maendeleo ya wilaya siyo DC wala madiwani.

DC anasimamia interest za Serikali iliyoko madarakani.

Diwani anawakilisha interest za wananchi na kufuatilizia utekelezaji na wanahudhuria vikao vya Baraza na kamati kupitia maazimio na yatokanayo husika, Madiwani hawatakiwi kuingilia shughuli za utendaji, kama kutoa maagizo nje ya vikao halali vya Halimashauri, vilevile DC na RC. DC RC ni assistant Proper officer na Proper respectively. Wakusanyaji fedha za miradi ya Halimashauri na uendeshaji ni watendaji.

Hivyo watendaji wasionewe na kudhalilishwa na wanasiasa, hivyo waachwe wafanye kazi zao kea mujibubwa sheria na taratibu za Serikali za Mitaa. Wan taratibu zao kuadhibiana.

Madiwani mara nyingi ndiyo wafugaji wa taratibu za Halimashauri, ndiyo wanatosa watendaji ambao kwa bahati mbaya hawajui vizuri taratibu za uendeshaji wa Halimashauri.

Dawani anahudumu kwa miaka mitano lakini mtendaji yuko pale kwa muda wake wa utendaji.
 
Hela zitaliwa tuu na hao hao madiwani kama upepo haujakupitia chuna tu.
 
Back
Top Bottom