Madiwani wa Ileje wamsurubu mkurugenzi kidokozi wa kura za mgombea wa CHADEMA Sumbawanga

Ndyali

JF-Expert Member
Nov 24, 2011
1,661
948
Wana- JF mtakumbuka mama yule aliyekuwa Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Sumbawanga Mjini, alihusika sana kupora haki ya watu wa jimbo la Sumbawanga mjini kuwakilishwa na mtu waliyemtaka Mwalimu Yamsebo. Mama Siliwa, alidokoa Kura za Mzee Yamsebo wa CHADEMA na kumjazia Aeshi wa CCM.

Mara tu baada ya kutangaza matokeo ya dhuruma mama Siliwa ghafla alihamishwa Sumbawanga, kwenda kuwa mkurugenzi wa halimashauri ya Ileje.

Lakini juzi laana ya watu wa Sumbawanga ilimfuata hukohuko Ileje ambapo kwenye kikao cha madiwani waliokuwa wakimsurubu kwa udokozi wa fedha za umma wa Ileje, alisikika akitamka aonewe huruma mara tisa hata hivyo, madiwani waligoma na kumpiga kalam.:A S-baby::A S-baby:
 
Awajibike asisubiri kutimuliwa!!

WAKAZI wa Wilaya ya Ileje mkoani hapa, wameutaka uongozi wa mkoa huo kuwawajibisha watendaji wa wilaya hiyo kwa kusababisha ukosefu wa huduma za afya.
Kauli ya wakazi hao imekuja siku chache baada ya Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo kumsimamisha kazi Mkurugenzi wake, Silvia Siriwa kwa tuhuma za ubadhirifu.
Wakizungumza kwenye mdahalo ulioandaliwa na asasi za kiraia za Wilaya ya Ileje (ILENGONET) kwa kushirikiana na mashirika ya kiraia Mkoa wa Mbeya (MBENGONET) uliofanyika jana, walidai kuwa uzembe wa viongozi hao unawalazimisha baadhi ya wananchi kukosa matibabu katika hospitali ya wilaya.
Baadhi ya huduma za matibabu wanazokosa wakazi hao ni X-ray na upasuaji hali inayowalazimu wenye uwezo kifedha kwenda Wilaya ya Chipata nchini Malawi umbali wa kilomita 35.
“Tunashangaa kuona Wilaya ya Ileje ambayo ni sehemu ya Tanzania wananchi wake wanakosa matibabu na kulazimika kukimbilia nchi jirani na kwa waganga wa kienyeji, hivyo ni lazima viongozi tuliowachagua kama madiwani wawajibishe wote waliozembea,” alisema Michael Nelson mkazi wa Itumba.
Kutokana na malalamiko ya wananchi hao Mwenyekiti wa Halmashauri ya Ileje, Mohamed Mwala aliyehudhuria mdahalo huo, aliwataka wananchi kuwa wavumilivu kwa sababu madiwani wamechukua hatua dhidi ya watendaji wabadhirifu katika halmashauri hiyo

Source: Tanzania daima 31/05/12.
 
Mimi nilimuonea huruma juzi Kumbe mwizi fukuza kabisaa hilo jimama

Hii Mikada ya ccm inapenda sana kuonewa huruma wakati mioyoni mwao imejikinai kufanya unyama kana kwamba peke yao ndo wenye haki katika nchi hii.:sleepy::sleepy:
 
Awajibike asisubiri kutimuliwa!!

Huyu mama analindwa sana na mtoto wa Mkulima, hapa Mbeya akiwa afisa maendeleo ya jamii aliwahi kuwashiwa moto na madiwani wa jiji la Mbeya kwa nyodo zake, lakini tukashanga anapaishwa kuwa kuwa Mkurugenzi wa halimashauri ya Sumbawanga.
 
safi sana na bado huyo mama atakomaa h!yo laana haimuachi itamtafuna mpaka ashangae, kilo cha masikin wapiga kura kimemfikia mola anawalipia na ni somo kwa wez wote wa kula na wanaojihusisha na vitendo vinyokiuka maadil ya u2mish
 
Hata hivyo ni mbabe sana huyu mama! Amekuwa akihamishwa hamishwa katika mikoa hiyo miwili kwa zaidi ya miaka 10 sasa
 
Fukuzeni kabisa, lakini yalivyo yaa jabu utasikia anapelekwa lindi vijijini
 
hahaa kuna yule naibu waziri anayekagua BOQ na vitasa vya UNION? hajui hili kweli?
 
Kumbe huyu mama ndiye aliyekuwa Sumbawanga. Lo! Mvisheni Sanda Nyeusi Akafie huko, Gamba mkubwa
 
Back
Top Bottom