SoC03 Madhara ya utoaji wa mimba kwa vijana na jamii kwa ujumla

Stories of Change - 2023 Competition
Jul 12, 2023
3
1
Utangulizi.
Matharani kundi kubwa la vijana wa kike ndilo linaongoza kwa utoaji wa mimba katika jamii nyingi za kiafrika.
πš„πšπš˜πšŠπš“πš’ 𝚠𝚊 πš–πš’πš–πš‹πšŠ,Hiki nikitendo cha kutoa kijusi,uteute unao wezesha kuumbika kwa mtoto katika tumbo la uzazi.

Hivyo ni vyema kama jamii kuandaa mpango kazi wa kuhakikisha kwamba tunakomesha kabisa kitendo cha utoaji wa mimba.

Kutokana na tafiti mbalimbali nilizo soma kuhusu maendeleo ya vijana ,nimefanikiwa kugundua kwamba vijana wengi huingia kwenye mahusiano kwa lengo la kufanya ngono na kuachana.

Sababu za utoaji wa mimba.
Kunasababu kedekede ambazo kwa namna yake huchochea katika swala zima la utoaji wa mimba.
π™ΌπšŠπšπšŠπšπš’πš£πš˜ 𝚒𝚊 πš”πš’πšŠπšπš’πšŠ,Ni moja kati ya sababu ambayo kwa namna ya kipekee huwa inapelekea utoaji wa mimba kwa wanawake wengi sana,hii hutokana na ridhaa ya kisayansi kupitishwa kwa lengo la kuokoa maisha ya mtolewaji wa mimba.

πš„πš”πš˜πšœπšŽπšπšž 𝚠𝚊 πšŽπš•πš’πš–πšž 𝚒𝚊 𝚊𝚏𝚒𝚊 𝚒𝚊 πšžπš£πšŠπš£πš’,Hali hii hupelekea kuibuka kwa matatizo ya kutopangilia uzazi kwa kutoacha muda wa kutosha ili kuzaa mtoto mwingine hupelekea kutolewa kwa mimba ili kulinda ukuaji wa mtoto aliye tangulia kabla ya mimba.

πš‚πš πšŠπš•πšŠ πš•πšŠ πšžπš–πšŠπšœπš”πš’πš—πš’,Umaskini ni hali ya kutokuwa na uwezo wa kupata mahitaj ya msingi kama vile,chakula, mavazi na makazi kutokana na hali hii wanawake na mabinti wengi huwa wakipata mimba hukimbilia kuzitoa.

π™Όπš–πš˜πš–πš˜πš—πš’πš˜πš”πš˜ 𝚠𝚊 πš–πšŠπšŠπšπš’πš•πš’,Kuporomoka kwa maadili mema katika jamii hupelekea kukua kwa vitendo viovu mfano, ubakaji,ukahaba pamoja na Uzinzi vitendo hivi kama matikeo ya mmomonyoko wa maadili husababisha mimba na hpelekea utoaji wa mimba.

Madhara ya utoaji wa mimba kwa vijana na jamii kwa ujumla.

Kitendo cha utoaji wa mimba huwa kina madhara kwa mtoji mwenyewe na jamii kwa ujumla huwa ina athirika.
π™·πšžπš™πšŽπš•πšŽπš”πšŽπšŠ πš”πš’πšπš˜ πš”πš πšŠ πš–πšπš˜πšŠπš“πš’ πš–πš πšŽπš—πš’πšŽπš πšŽ,Hali hii inaweza kusababishwa na kutoka kwa damu nyingi wakati wa utoaji wa mimba pamoj na michubuko inayo sababishwa na kukatwa kwa maungio ya mtoto tumboni.

π™·πšžπš™πšžπš—πšπšžπš£πšŠ πš—πšπšžπšŸπšž πš”πšŠπš£πš’ 𝚒𝚊 πšπšŠπš’πšπšŠ,Hali ya mtu aliyetoa mimba huwa ni mtu mwenye uchovu mwingi pamoja na mwili kukosa nguvu,akili yake huwa inamawazo mengi kutokana na mvurugiko wa saikorojia kwa kitendo cha utoaji mimba hivyo huchukua muda ili kurudia hali yake ya kawaida katika utendaji kazi wake,pamoja na kiumbe kilicho potea huenda kingekuwa na mchango katika taifa.

π™·πšžπš™πšŽπš•πšŽπš”πšŽπšŠ πš–πšŠπšπšŠπšπš’πš£πš˜ πš”πšŠπšπš’πš”πšŠ πš–πšπšžπš–πš˜ 𝚠𝚊 πšžπš£πšŠπš£πš’,Ni hali ambayo hutokea pale ambapo mwanamke ametoa mimba mara moja au zaidi kwani kwa kawaida mishipa inayo zunguka uke ndani na nje huwa inadhurika hivyo hupelekea kukosa uwezo wa kubeba mimba.

Je! nini kifanyike ili kuhakikisha kwamba tunazuia utoaji wa mimba katika jamii.

π™ΊπšžπšŽπš•πš’πš–πš’πšœπš‘πšŠ πš“πšŠπš–πš’πš’ πš“πšžπšž 𝚒𝚊 πš–πšŠπšπš‘πšŠπš›πšŠ πš’πšŠπšžπšπš˜πšŠπš“πš’ 𝚠𝚊 πš–πš’πš–πš‹πšŠ, Elimu hii inalenga kutoa uelewa wa kuzuia mimba zisizo tarajiwa katika mahusiano ya kimapenzi kwa vijana na anandoa pia.

π™Ίπšžπš πšŽπš™πš˜ πš”πš πšŠ πš—πš“πš’πšŠ πš—πš£πšžπš›πš’ 𝚒𝚊 πš–πšŠπš•πšŽπš£πš’ πš”πš πšŠ πšŸπš’πš“πšŠπš—πšŠ πš—πšŠ 𝚠𝚊𝚝𝚘𝚝𝚘,Malezi mazuri huwaweka watoto na vijana wakue kwenye maadili mema pamoja na kuwajengea uwezo wa kupinga vishawishi ambavyo vinapelekea kuingia kwenye ngono zembe pamoja na utoaji wa mimba.

π™Ίπšžπšπš˜πšŠ πšŽπš•πš’πš–πšž πš”πš πšŠ πš“πšŠπš–πš’πš’ πš“πšžπšž 𝚒𝚊 πšžπš£πšŠπš£πš’ 𝚠𝚊 πš–πš™πšŠπš—πšπš˜,Elimu hii ya uzazi wa mpango huwafanya wanajamii waweze kuishi kwenye maisha bora zaidi kwa kuzuia mimba zisizo tarajika kwa kutumia njia bora za kuzuia mimba ili kuepukana na wimbi la utoaji wa mimba.

π™Ίπšžπšπš˜πš•πšŽπš πšŠ πš”πš πšŠ πšŽπš•πš’πš–πšž 𝚒𝚊 πšœπšπšŠπšπš’ 𝚣𝚊 πš–πšŠπš’πšœπš‘πšŠ,Elimu ya stadi za maisha huwa inafundisha ujuzi mbali mbali hivyo humfanya kijana awe na ubunifu ambapo ataweza kufanya kazi kwa bidii na kujitengenezea uchumi mzurii,hivyo ataweza kujihudumia wakati wa ujauzito na baada ya kujifungua itasaidia kupunguza utoaji wa mimba.

πš„πšœπš‘πšŠπšžπš›πš’ πš“πšžπšž 𝚒𝚊 πš”πšžπš™πšžπš—πšπšžπš£πšŠ πšœπš πšŠπš•πšŠ πš•πšŠ πšžπšπš˜πšŠπš“πš’ 𝚠𝚊 πš–πš’πš–πš‹πšŠ πš”πš πšŠ πšŸπš’πš“πšŠπš—πšŠ πš—πšŠ πš“πšŠπš–πš’πš’ πš”πš πšŠ πšžπš“πšžπš–πš•πšŠ.
π™Ίπšžπšπš˜πš”πšŠπš—πšŠ πš—πšŠ πš–πš πš˜πš—πšŽπš”πšŠπš—πš˜ 𝚠𝚊 πšŸπš’πš“πšŠπš—πšŠ πš πšŽπš—πšπš’ πš”πšžπš πšŠ πš πšŠπš—πšŠπš’πš—πšπš’πšŠ πš”πš πšŽπš—πš’πšŽ πš–πšŠπš‘πšžπšœπš’πšŠπš—πš˜ 𝚒𝚊 πš”πš’πš–πšŠπš™πšŽπš—πš£πš’ πš”πš πšŠ πš•πšŽπš—πšπš˜ πš•πšŠ πš”πšžπšπšŠπš—πš’πšŠ πš—πšπš˜πš—πš˜ πš—πšŠ πš‹πšŠπšŠπšπšŠπšŽ πš”πšžπšŠπšŒπš‘πšŠπš—πšŠ πš™πšŠπšœπš’πš™πš˜ πš—πšŠ πšœπšŠπš‹πšŠπš‹πšž 𝚒𝚊 πš–πšœπš’πš—πšπš’ πš—πšπš’πš™πš˜ πšπšžπš—πšŠπš˜πš—πšŠ πš–πšŠπšπš˜πš”πšŽπš˜ πš”πšŠπš–πšŠ πšŸπš’πš•πšŽ πšžπšπš˜πš“πš’ 𝚠𝚊 πš–πš’πš–πš‹πšŠ,πš˜πš—πšπšŽπš£πšŽπš”πš˜ πš•πšŠ πšπšŠπš–πš’πš•πš’πšŠ πš’πšŽπš—πš’πšŽ πš–πš£πšŠπš£πš’ πš–πš–πš˜πš“πšŠ πš™πšŠπš–πš˜πš“πšŠ πš—πšŠ 𝚠𝚊𝚝𝚘𝚝𝚘 𝚠𝚊 πš–πšπšŠπšŠπš—πš’.

π™·πš’πšŸπš’πš˜ πš‹πšŠπšœπš’ πš—πš’ πšŸπš’πšŽπš–πšŠ πš£πšŠπš’πšπš’ πš”πšŠπš–πšŠ πšŸπš’πš“πšŠπš—πšŠ πš πšŠπš”πš’πš™πšŠπšπšŠ πšŽπš•πš’πš–πšž 𝚒𝚊 πšžπš£πšŠπš£πš’ 𝚠𝚊 πš–πš™πšŠπš—πšπš˜ πš”πšŠπš‹πš•πšŠ 𝚒𝚊 πš”πšžπš“πšŽπš—πšπšŠ πš–πšŠπš‘πšžπšœπš’πšŠπš—πš˜ 𝚒𝚊 πš”πš’πš–πšŠπš™πšŽπš—πš£πš’,πš”πš πšŠ πš—πšŠπš–πš—πšŠ 𝚒𝚊 πš”πš’πš™πšŽπš”πšŽπšŽ πš πšŠπš—πšπšŽπš πšŽπš£πšŠ πš”πšžπš πšŠ πš—πšŠ πšπšŠπš–πš’πš•πš’πšŠ πš—πš£πšžπš›πš’ πš—πšŠ πš’πšŽπš—πš’πšŽ 𝚊𝚏𝚒𝚊.
 
Back
Top Bottom