Madenti Vs Mwalimu

Mohammed Hamad

JF-Expert Member
Jan 17, 2011
3,988
1,304
Madenti 5 chuo kikuu kimoja hapa nchini walikuwa wanatakiwa wafanye mtihani siku inayofuata. Bahati mbaya wakanywa pombe mpaka mida mibaya na hivyo wasingeweza kufanya mtihani kesho yake. Wakatunga uongo wa kwenda kumdanganya mwalimu wa somo husika kwamba walikuwa kwenye harusi na wakati wanarudi gari yao ikapata pancha na wakavamiwa na vibaka na kuibiwa pamoja na kupigwa. Yule Lecture alikubali na akawapa siku tatu za kujiweka sawa na kujiandaa na special exam. Siku ya mtihani wa Special yule Lecture aliwapa mtihani na aliwasimamia mwenyewe.

Mwongozo wa mtihani ulikuwa kama ifuatavyo:
1. Mtihani huu ni kwa wanafunzi watano.
2. Majibu yao lazima yawe sawa na yakiwa tofauti wote wanapata ziro na wanafeli.
3. Mtihani huu una maswali matano na yote lazima yajibiwe.

Maswali ya mtihani yalikuwa hivi:
1. Harusi ilifanyika katika ukumbi gani?
2. Gari mliomtumia mpaka mkapata pancha inaitwaje?
3. Ajali imetokea eneo gani? 4.Nani alikuwa dereva?
5. Tairi ipi ilipata pancha,ya mbele au ya nyuma?

NAWATAKIA MTIHANI MWEMA!Mwalim
 
hapa si Korogwe.Nenda Willy Gk au Baclays Ukawape huo oungo.Mpe Hi Scud
 
Back
Top Bottom