Mzito Kabwela
JF-Expert Member
- Nov 28, 2009
- 18,857
- 7,617
Na waandishi wetu Fredy Azzah na Fidelis Butahe
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ambaye jana aliruhusiwa kutoka katika Hospitali ya Aga Khan ya jijini Dar es Salaam alikolazwa kwa matibabu ya tumbo amedai kuwa matatizo hayo aliyapata baada ya kula chakula chenye sumu.Namshukuru Mungu naendelea vizuri na nimesharuhusiwa kutoka hospitali, madaktari wameniambia ilikuwa food poisoning (chakula chenye sumu), alisema Zitto.
Zitto ambaye hakuweza kueleza chakula hicho alikuwa wapi na kina sumu ya aina gani, alisema kuwa baada ya kugundua tatizo hilo, madaktari walimtaka kuwa makini na vyakula anavyokula.
Sumu gani nimekula na ni wapi, mimi nadhani sio story (habari). Cha msingi kwa sasa naendelea vizuri na nimetakiwa kuwa makini na vyakula ninavyokula, alisema Zitto.
Hata hivyo, kauli hiyo ya Zitto inapingana na madaktari wake waliosema kuwa mbunge huyo kupitia tiketi ya Chadema, alikuwa anasumbuliwa na mchafuko wa kawaida wa tumbo.
Alikuwa anasumbuliwa na Gastro enteritis (mchafuko wa tumbo), tatizo hili linaweza kusababishwa na bacteria, virusi katika chakula, au kama chakula hakijapikwa vizuri, alisema Dk Mustafa Bapumia.
Zitto alilazwa hospitalini hapo tangu Disemba 9 mwaka huu saa 3:00 usiku, baada ya kutoka kwenye mkutano wa ndani wa chama chake uliofanyika Bagamoyo mkoani Pwani ambako alivuliwa cheo cha Naibu Kiongozi wa Kambi ya upinzani bungeni.
Kuhusu hatua ya chama hicho kumvua Zitto wadhifa wake wa unaibu kiongozi wa upinzani bungeni, alisema kwa sasa bado hawezi kuzungumzia suala hilo kwa sababu hajapata taarifa rasmi kutoka chama chake mbali na kusoma suala hilo kwenye vyombo vya habari.
Hata hivyo, alieleza hakuwahi kuomba kupewa wadhifa huo, kwa hiyo endapo watu waliomwona anafaa kufanya kazi na kumpa wadhifa huo, wakiamua kumnyanganya siyo tatizo kubwa kwake.
Kwa sasa nadhani suala la afya yangu ndiyo muhimu zaidi. Ngoja kwanza nitoke hapa na afya yangu iimarike na kama kutakuwa kuna sababu ya mimi kuzungumza nitazungumza, alisema Zitto:
Lakini ikumbukwe kuwa mimi sikuwahi kuomba wadhifa huu , kwa hiyo kama watu walionipa wameamua kunibadilishia, mimi sidhani kama kuna tatizo.
Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe aliupolizwa na Mwananchi Jumapili juu ya Zitto kuvuliwa uongozi bungeni alisema kuwa chama kitatoa taarifa baadaye.
Source : Mwananchi
Mijitu mingine bana! Jitu lina kipindupindu linasema sumu!