MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba, Mohamed Abdallah Machupa, amesema klabu hiyo imemdhalilisha vya kutosha, hivyo hafikirii kuichezea tena klabu hiyo.
Akizungumza leo jioni, Machupa, ambaye kwa sasa yupo Tanzania akikamilisha taratibu za kujiunga na klabu yake mpya ya Aalborg BK 1885 ya Denmark, inayoshiriki ligi kuu ya nchi hiyo, alisema kuwa Simba isahau kufikiria kumwita katika kikosi chake kutokana na vitendo alivyofanyiwa wakati anaichezea.
Klabu ya Aalborg BK 1885 inashiriki katika michuano ya UEFA baada ya kushika nafasi ya tatu kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya katika kundi lililohusisha timu za Manchester United na Villareal, ambazo zilishika nafasi mbili za juu katika kundi hilo.
Source : NIFAHAMISHE Tanzania news portal