Mabilioni yaliyotumika katika uboreshaji wa utumishi wa umma ni kama yameteketea

Byendangwero

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
871
56
Kwa karibu miongo miwili na nusu sasa, serikali imekuwa ikitekeleza mpango wa uboreshaji wa utendaji kazi katika utumishi wa umma. Mpango huo, unahusisha serikali kuu na serikali za mitaa. Jambo la kushangaza ni kuona kwamba katika kipindi hicho cha utekelezaji wa mpango huo, nchi yetu imeshuhudia mmomonyoko mkubwa wa maadili kwenye utumishi wa umma ambao haukuwahi kushuhudiwa; kwa mfano, uuzaji holela na kwa bei ya kutupwa wa mali za umma, mikataba mibovu, uchotaji wa wazii wazi wa fedha za umma kupitia EPA na makampuni hewa kibao n.k. Swali langu, kuna haja ngani kwa serikali na wafadhili kuendelea kuteketeza fedha nyingi katika utekelezaji wa mpango huo, ambao dhahiri umeliingizia taifa hasara kubwa?
 
Back
Top Bottom