Mabasi ya mwendo kasi Mbezi na Kimara yameleta machungu kuliko neema?

Peter Agostino

Senior Member
Sep 23, 2016
105
226
Mabasi yaendayo kasi maarufu kama mwendo kasi jijini Dar es salaam yalipoanza rasmi mwezi may mwaka huu kila mtu hususani wakazi wa maeneo ya Kimara na Mbezi alishangilia. Walifahamu sasa shida ya usafiri bye bye. Lakini kadiri siku zinavyozidi kwenda na serikali kutimiza azma yake ya kuziondoa daladala zingine zote ndogo ndivyo shida ya usafiri Mbezi na maeneo ya karibu nayo inavyozidi kuongezeka.

Shida hii inaonekana kuwaathiri zaidi wananchi wa kipato cha chini ambao inakuwa vigumu kuunganisha magari mawili kutokana na nauli kuwa kubwa. Watu walizoea kupanda basi moja kutoka Mbezi mpaka maeneo mengine ya katikati ya jiji ijapokuwa wakati mwingine kwa kusukumana na kusubiri muda mrefu stendi, lakini hilo wala haliwezi kumsumbua mwananchi wa kawaida ambaye kipato chake hakizidi dola 2 kwa siku. Ni bora achelewe kuliko kuteketeza fedha kidogo aliyokuwa nayo mfukoni kwa nauli.

Tatizo linalolalamikiwa na watu wengi wa maeneo haya ni kwamba, asubuhi mtu uwapo tuseme maeneo kama mbezi mwisho, kibanda cha mkaa, Kwa msuguri, Temboni na hata Kimara Suka, huwezi kupata gari kirahisi linalokwenda maeneo ya katikati ya jiji, badala yake unalazimika kupanda daladala ziendazo Kimara mwisho ndipo tena ukachukue Mwendokasi kwa shilingi 650. Bora basi ungepanda hata daladala la kawaida sh 300 mpaka Kimara mwisho, hivi karibuni tena hata hizo daladala hazionekani, unapanda mwendokasi linalotokea Mbezi, unalipa 400 na kisha wanakushusha Mbezi Mwisho unakata tena tikiti ya sh. 650 ili uende unakokwenda.

Watu wengi wanalilia angalao Serikali ingeliona hili na kuamua kati ya mambo haya 3, Magari hayo yasiishie Kimara Mwisho bali yaende mpaka Mbezi mwisho kwa nauli hiyohiyo moja au wapunguze nauli kidogo angalao mtu unapokwenda mjini usitoe zaidiya 1000 kwa safari ya kwenda tu peke yake, na tatu, ikiwezekana daladala za kawaida ziachwe chache ziendelee kufanya kazi kwa ajili ya watu wa hali za chini.

Mama mmoja anayefanya biashara ya kuuza mahindi ya kuchoma alikuwa akilalamika kwa masikitiko akielezea jinsi ambavyo faida yake ya mahindi inavyoishia njiani tofauti na siku za nyuma alipokuwa akipanda daladala za kawaida.

Anasema mahindi huyafuata Tandale akitokea Kimara Matosa na anapofika kituoni Kibanda cha mkaa husimama muda mrefu bila kuona gari mpaka anapoamua kupanda mwendokasi kwa sh.400 hadi Kimara, halafu hapo huchukua tena mwendokasi lingine kwa sh. 650. Anasema kwa siku mpaka anafika Matosa hutumia zaidi ya sh.3,000 pamoja na bajaji kutoka stendi kibanda cha mkaa mpaka anapofanyia biashara yake.


Mwandishi wa makala hii ni Mwanzilishi wa Blogu ya Jifunzeujasiriamali na mwandishi wa vitabu vya Self Help Books Tanzania

Karibu pia kwenye Darasa la kujifunza Michanganuo ya biashara liitwalo, (Tanzania Online School of Business Planning(TOSBP))
 
Hayo nagari wenye uelewa walishaachana nayo ni kero tu sio huko tu Kila sehemu,
Kuna uwezekano na wao wanaisoma namba
 
Ni kwl aisee, alaf magar hayafiki vituon kwa wakati , magar machache , mnashindiliwa kama mkaa wenye viroba, dada zetu wenye presha kila kukicha wanadondoka kwa kukosa hewa ya kutosha ,

Yan sielewi nn hatma ya huu mrad
 
Mimi nimeshakata tamaa.Nauli inaumiza sana.Kwakweli usafiri huu bado haujakaa sawa.Unakuta abiria mmejazana kituoni lakini magari machache.Gari likifika inakuwa ni balaa...ni kugombania tu.Juzi nimeibiwa elfu 50 pale Gerezani wakati tukigombania kuingia kwenye gari.Roho iliniuma sana,sikuona hata mtu wa kumlalamikia.Sijaona hata sanduku la kutolea maoni.Serikali inabidi iutazame upya huu usafiri vinginevyo tutazidi kuumia.Mbaya zaidi hata vyombo vya habari kwa sasa havifuatilii sana usafiri huu kama wakati usafiri huu ulipokuwa unaanza.
 
Walipokuwa wanataka kuweka kiwango cha nauli kwa safari moja Tsh1,600/= wanasiasa walipata kick kwa kujifanya kuingilia kati kwamba ni kiwango kikubwa sana ila hawakumaanisha ilikuwa siasa tu...ungetegemea ktk hili yule yule wa mwanzo atoe tamko kukataza ila yupo kimya,sitaki kuamini kwamba hajui kuna wananchi duni wanapata shida kutokana na mipango mibovu ya wasimamizi wa jiji.aseme neno watu wanateseka.
 
Ukiwa na kadi Mbezi-Gerezani-Kivukoni ni sh 800 kama huna kadi ni sh 1050 kadi inauzwa 2000 unabakiwa na sh 1500
 
ninacho kiona serikali ina nia nzuri haswa kupunguza foleni lakini bdo haijajipanga vyema.matokeo yake ni shida tupu.mbaya zaidi kwa wanaotokea kibaha na bagamoyo.unaweza jikuta mshahara wote umeishia kwenye nauli duh
 
Hakuna haja ya kuzuia daladala kufanya safari zake hata kama gari za mwendokasi zipo, kuzuia daladala ni kuwalazimisha abiria kutumia mwendokasi kilazima lazima.
 
waambie wanunu kadi kama wansafiri mara kwa mara itasaidia nauli ni 800 ukiunganisha
 
waambie wanunu kadi kama wansafiri mara kwa mara itasaidia nauli ni 800 ukiunganisha
Bado nikubwa Sana kwa mtu wa kipato cha chini kwasababu kutoka mbezi mpaka kivukoni kwa daladala ni sh 600 na kutoka mbezi mpqka kariakoo n 500 wakati kwa mwendokasi ni 800 wacha daladala ziende huko posta , kivukoni na kariakoo ili wengine wasevu hela. Na sio kuwalazimisha kupanda hayo mabasi kwa tetesi kwamba hawapati faida ndo mana wamefungia hizo daladala kwenda huko. Wacheni free trade ikamate mkondo wake
 
Bado nikubwa Sana kwa mtu wa kipato cha chini kwasababu kutoka mbezi mpaka kivukoni kwa daladala ni sh 600 na kutoka mbezi mpqka kariakoo n 500 wakati kwa mwendokasi ni 800 wacha daladala ziende huko posta , kivukoni na kariakoo ili wengine wasevu hela. Na sio kuwalazimisha kupanda hayo mabasi kwa tetesi kwamba hawapati faida ndo mana wamefungia hizo daladala kwenda huko. Wacheni free trade ikamate mkondo wake
sio wamezifunga kwa tetesi kuwa hawapati faida ndio mkataba unavotaka kuwa zikiisha t.l.b waondoke barabarani
 
1478809983805.jpg
36b572c75f1871fba46b8d5655db97c4.jpg
View attachment 432285View attachment 432286View attachment 432287View attachment 432288
Mimi nimeshakata tamaa.Nauli inaumiza sana.Kwakweli usafiri huu bado haujakaa sawa.Unakuta abiria mmejazana kituoni lakini magari machache.Gari likifika inakuwa ni balaa...ni kugombania tu.Juzi nimeibiwa elfu 50 pale Gerezani wakati tukigombania kuingia kwenye gari.Roho iliniuma sana,sikuona hata mtu wa kumlalamikia.Sijaona hata sanduku la kutolea maoni.Serikali inabidi iutazame upya huu usafiri vinginevyo tutazidi kuumia.Mbaya zaidi hata vyombo vya habari kwa sasa havifuatilii sana usafiri huu kama wakati usafiri huu ulipokuwa unaanza.
 
Unajua tatizo jingine ni elimu kwa watumiaji mabasi haya, ni watu wengi hata hawaelewi kama kuna huo utaratibu wa kadi, wanapowaona wale waliokuwa na kadi hudhania penginee ni watu spesho au wafanyakazi wa serikali na mashirika makubwa kumbe hata wao wangeweza tu kuwa nazo. Mimi naona kikubwa hapa juhudi nazo zingeongezwa na mamlaka ya mradi huo kuwaeleimisha wananchi na siyo kuangalia faida wanayoipata tu. Mbona sioni kampeni kubwa kwenye vyombo vya habari kuwajulisha abiria maswala mbalimbali yahusuyo mradi kama ilivyoonekana wakati wanauzindua?
 
Back
Top Bottom