Mabanati Yapimeni

Sideeq

JF-Expert Member
Dec 12, 2009
2,422
434
Naasa nisikiani, ya lazima mabanati
Wamekuvisha vimini, hujuwi zao shuruti
Tayari umtihanini , epukeni ma afiriti
Mabanati yapimeni haya yangu mi matamko

Kukwita mi sitochoka , ile njia mustaqima
Nabaki nahuzunika , uendako sio kwema
Na mwenzako walimzika, sio maradhi ya homa
Mabanati yapimeni haya yangu mi matamko

Mary kwa sasa tunaye , amekuwa Mariamu
Kujichuna basi yeye, hijabu haishutumu
Mazurizuri mamboye, hanaye wa kumlaumu
Mabanati yapimeni haya yangu mi matamko

Azisikiza nyingi tepu, za walewale Ansari
Kumuona raha tupu , twajionea ufahari
Karaha ya lapulapu, kutupwa kwenye bahari
Mabanati yapimeni haya yangu mi matamko

Yule Ruth mwamkumbuka?, mmbeja wake Coheni
Nikabu yu ajivika, kitabu kipo mkononi
Cohen kasitirika, tunaye majalisini
Mabanati yapimeni haya yangu mi matamko
 
Ushairi u-mzuri, lughaye nimeipenda
hakika u mhariri, sifazo ninakusunda
misamiati titiri, jibu nimeshindwa unda
mabanati naghairi, mpaka maana kuponda!
 
Mmoja kajitokeza , asiyejuwa kuiunda
Je yupo wa kutueleza, maana bila ya kupinda
Compaq keshatujuza , misamiati imemshinda
Mmoja kajitokeza , asiyejuwa kuiunda
 
Siniseme kwa ubaya, sikupenda kutojua
yani nimepata haya, mabanati kutojua
nawewe bila ya haya, umeshindwa kutatua
mabanati gani haya, nimeshindwa kuyajua!
 
Siniseme kwa ubaya, sikupenda kutojua
yani nimepata haya, mabanati kutojua
nawewe bila ya haya, umeshindwa kutatua
mabanati gani haya, nimeshindwa kuyajua!
Beti gani nilisema, nimeshindwa kutatua
Heri uibaini vyema ,ili tupate ijua
Hapa sasa nasimama, nangoja jibu murua.
Mmoja kajitokeza , asiyejuwa kuiunda
 
Beti gani nilisema, nimeshindwa kutatua
Heri uibaini vyema ,ili tupate ijua
Hapa sasa nasimama, nangoja jibu murua.
Mmoja kajitokeza , asiyejuwa kuiunda

nimetafuta kamusi, ili nipate baini
mabanati nini basi, sijaweka maanani
nijulishe kwa kiasi, beti niweze kughani
naomba ufanye kasi, mabanati kitu gani!!!???
 
nimetafuta kamusi, ili nipate baini
mabanati nini basi, sijaweka maanani
nijulishe kwa kiasi, beti niweze kughani
naomba ufanye kasi, mabanati kitu gani!!!???
Mmoja ndiye binti, walo wengi mabanati
Usizilete hatihati, tughanie bila ya ati
uupambe kwa shuruti, ughani wa mabanati.
Mmoja kajitokeza , asiyejuwa kuiunda
 
Back
Top Bottom