Mabalozi wa Tanzania ughaibuni

R

raisi

Guest
Naomba kuuliza swali,kwanini mabalozi wa Tanzania walio wengi ,katika nchi za waarabu au zenye asili ya kiarabu,ndani na nje ya Africa ni waislamu tuu?

Nawasilisha.
 
Hata kama ni kweli, nchi ulizotaja ni za kiislam hivyo ni vizuri mabalozi wakawa ni watu wanaofuata utamaduni huo.
 
Kwa hiyo nchi za ulaya na america,lazima wawatafute waislamu kuwakilisha nchi zao.hilo halina msingi.hapo kuna kupendeana.
 
Kazi za Balozi kwa lugha rahisi, ni kudumisha urafiki na nchi husika. Ndani ya urafiki huo ndipo huweza kutokea uhusiano au ushirikiano wa kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Kufuatia lengo hilo, ni busara kumpeleka balozi Muislamu nchi za Kiislamu kama tunavyompeleka balozi Mkiristu ubalozi wetu wa Italy ambaye pia anatuwakilisha Vatican ambayo ni nchi ya Kikristo.

The formular is simple logic na sio udini.
 
define nchi ya Kiislam kwanza then tutajua kama kuna mjadala hapa au la

Naomba kuuliza swali,kwanini mabalozi wa Tanzania walio wengi ,katika nchi za waarabu au zenye asili ya kiarabu,ndani na nje ya Africa ni waislamu tuu?

Nawasilisha.

Hakuzungumzia nchi ya kiislamu bali nchi za waarabu au wenye asili ya kiarabu. Kwani uarabu ni uislamu?

Amandla.....
 
Udini ni swala la kifikra zaidi kuliko uhalisia wa maisha yetu, nimekuwa nikijiuliza laiti mi ningeitwa rajabu baada ya kuzaliwa Yemen will it be bad? religion is a nonparticipatory first sight childhood upbringing ideology, it is a bit suprising no room is even given to question the parents or care takers/guardian.

with formal education if at all we have had families splited into traditionalists,christians,moslems, with such a scenario if it happen you priotize issues would value blood relations or religious affiiliation?
 
The way forward: deep insights should be sought up before such chaotic political and governance enzymes if not catalysts are worth registered in this diverse targeted populace platform. we should not force our intuitive opinions into potential facts.
 
Kuna maneno yamesemwa nami nauliza kule Paris hivi balozi wetu ni ndugu nani ? UK Je ? Kule Ujerumani sijui .Hebu nisaidieni.Mtu ukisema Arab world measn islam na si zaidi .
 
Kuna maneno yamesemwa nami nauliza kule Paris hivi balozi wetu ni ndugu nani ? UK Je ? Kule Ujerumani sijui .Hebu nisaidieni.Mtu ukisema Arab world measn islam na si zaidi .

Unamaanisha nchi zote za kiarabu ni za kiislamu au zina waislamu wengi?

Kwa mtazamo huu nchi za Albania, Iran,Turkey, Pakistan, Bangladesh, Malaysia, Indonesia n.k tunaziweka wapi?

Amandla.....
 
Kazi za Balozi kwa lugha rahisi, ni kudumisha urafiki na nchi husika. Ndani ya urafiki huo ndipo huweza kutokea uhusiano au ushirikiano wa kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Kufuatia lengo hilo, ni busara kumpeleka balozi Muislamu nchi za Kiislamu kama tunavyompeleka balozi Mkiristu ubalozi wetu wa Italy ambaye pia anatuwakilisha Vatican ambayo ni nchi ya Kikristo.

The formular is simple logic na sio udini.

Huo ndiyo ukweli ila inategemea na nchi zenyewe zina msimamo gani au tolerant kiasi gani.
Balozi wetu huko Italy kwenye miaka ya mwanzo ya 90 Mzee Sykes ( was it Abbas or Ally?) alikuwa ni Muislam na haikuwa na ubaya wala tatizo lolote.
 
Na ninavyoelewa, balozi wetu Italy ndiye anaetuwakilisha Vatican!
 
Hata kama ni kweli, nchi ulizotaja ni za kiislam hivyo ni vizuri mabalozi wakawa ni watu wanaofuata utamaduni huo.

kwa hiyo na nchi za ki kristu mabalozi wawe wa kristu?????
balozi anawakilisha TZ na sio dini
 
Hali ndiyo hiyo.

Udini mtupu.

Wote twajua Malkia ni top leader wa kanisa la Anglican Uk.

Jiulize Uk wamsusie maajar kisa muislamu itakuwaje?
 
Hali ndiyo hiyo.

Udini mtupu.

Wote twajua Malkia ni top leader wa kanisa la Anglican Uk.

Jiulize Uk wamsusie maajar kisa muislamu itakuwaje?

Mambo ya kidiplomasia hayaendi hivyo Mkuu.Diplomasia kama siasa ni mchezo wa aina yake.
UK hawawezi kususia TZ kwa vile balozi Mwanaidi Maajar ni mwislam.Na kabla alikuwepo balozi Ally Mchumo and all was ok.Kadhalika sidhani kama Tanzania ikiamua kumpeleka Balozi mkristo nchi za kiislam watamsusia... ila kama alivyosema PASCO hapo juu, ni suala la kuona huo ushirikiano wenu utapata faida gani endapo mtapeleka balozi anayeweza "kukubalika all round" - nadhani nimeeleweka.
 
Sahihisho. Ubalozi wa Tanzania nchini Ujeremani ndiyo unawakilisha Vatican, siyo Ubalozi wa Tanzania nchini Italia.
 
Back
Top Bottom