Mabadiliko ni muhimu na ni ya lazima ili kwa nafuu

milimo

Member
Nov 29, 2012
61
32
TAHADHARI; NIMAKALA NDEFU KIDOGO,LAKINI NAOMBA USOMA HADI MWISHO

( samahani Ilitolewa vibaya na kwa kichwa tofauti, sasa nimerekibisha kidogo kimwonekano ili isomeke vizuri)

Umeme:
Ni janga la nchi kwa siku za nyuma, sasa na siku zijazo kwasababu hatujawekeza vya kutosha
na hakuna juhudi zinzofanyika ili kuwekeza.

Mimisijabahatika kupewa kipawa cha unabii au utabiri, kama ninavyo basisijavitambua bado. Ninachongolea sasa sio utabiri wala unabii ila ni mtazamo tu.

Watanzania tumesambaratika, hatuwezi tena kutambua mbichi na mbivu. Kwa mtazamo wangu wala
sio utabiri, viongozi wa juu wa sasa wa wizara ya nishati na madini ni kati ya watanzania wachache wenye uzalendo (ni kweli nao wanayo mapungufukama binadamu wengine).

Mara nyingi tumewabeza kwa kejeli mpaka wanaelekea kukatishwa tamaa (hawapewi ushirikiano wa kutosha).

Kwa wale wanaojua wizaraile na tasisi zake zilivyokuwa zemegubikwa na madudu yasiyoelezeka watanielewa.
Hawa watu walianza vizuri sana lakini wamelipwa kejeli tu.

Watanzania tutajuta sana kama hawa watu wenye uzalendo ( kwa mazingira ya sasa ya nchi yetu) wataondoka bila kuwatumia vizuri. Mh. Rais awape
ushirikiano mzuri hawa watu, Bunge liwape ushirikiano, wafanyakazi wa wizara na tasisi zake wawape
ushirikiano, wananchipia tuwape ushirikiano na wao pia wasikate tamaa maana kazi ya kutumikia umma si
nyepesi wala kutaka kusifiwa.

Serikali itafute fedha na kuwekeza kwenyeumeme wakati watu hawa bado wapo wizarani.

Ushauri
Imefikia hatua kila ushauri mzuri unaotolewa na baadhi yawatu ambao wanao ufahamu mkubwa na uzoevu wa uongozi unabezwa.

Watanzaniatujitahidi sana kuwa wavumilivu na wasikivu kabla ya kutoa kejeli. Kwa mfano, Mh. Samwel Sita amekua mtu wa kusema ukweli mara nyingi (sio kwa asilimia mia)hata kufikia hatua ya kuisema serikali ambayo na yeye pia ni mmoja wao, hichosio kitu rahisi kama tunavyofikiria kwa mazingira ya sasa ya nchi yetu. Inawezekanakweli anafanya hivyo kwa maslahi fulani, lakini je nani ambaye hana maslahikatika lile analolisema au kutenda? Huyu mtu amesaidia sana kuondoa uwoga watanzania
wa kusema ukweli kwa maslahi ya umma hata kama kikundi unachokitumikia kitathirika kwa namna moja.

Ukweli wa hata asilimia hamsini tu ndio utakaotuvusha hapa tulipo. Nitoe mfano mmoja ambao unalingana
na hili; kuna rafikiyangu wa karibu sana ambaye ni daktari wa Phd mweledi wa mambo ya marketingand Entrepreneurship,
alikua kwenya timu ya kwenda wilayani Njombe (wakatihaijawa mkoa) kutoa ushauri kwa wafanyabiashara namna ya kukuza mitaji.

Baadaya semina waliruhusu maswali kutoka kwa wafanyabiashara. Wakaulizwa; tumesikia kwa makini
ushauri wenu na ni mzuri sana, lakini nyinyi je mumefanyia vipi hicho mlichotueleza ili na sisi tuige (wakinga ni wabishi na ni tomaso), rafikiyangu akaniambia lilikua swali gumi sana kwake kwa sababu hajawahi kufanya biasharayoyote hata kuwa na genge tu.

Lakini wale wafanyabiashara waliochukulia ushauriwao vizuri walienda tasisi za fedha kukopa na
wakakuza mitaji yao na sasa wanashukuru kwa ushauri waliopewa maana biashara zao zimekua kwa kiasi kikubwa sana.

Kwaufupi ni kuwa, usimchumchunguze sana bata utashindwa kula nyama yake na kufa nanjaa.

Mabadiliko ya kifikraya siasa kwa vijana wa vyama mbadala:
Kuna kitu kimoja kinakatisha tamaa watu wengi wenye ueledi namawazo mazuri, kushindwa kuunga
mkono moja kwa moja vyama mbadala mfano Chadema. Tatizo ni hili, ukiwangalia vijana wengi (sio wote)
wa Chadema wenyeushawishi/uongozi ndani ya chama wameanza kutembea mabega yakiwa juu
kamawanamajipu kwapani (Mh. Mandela aliwahi kusema unachukia jinsi Bush Jr. na Tonwalivyokua
wanaona dunia ni ya kwao kwa kutembea mabega juu kama wana majipu kwapani), wamefikia hatua hata
ya kuona wao tu ndio wenye kustahili kuongea mambo ya mabadilko ya kisiasa ya nchi hii, naomba viongozi
wa vyama mbadala wawe karibu sana na hawa vijana na kuwashauri kuwa na low profile.

Jeuri,majivuno, majigambo vitaua vuguvugu la mabadiliko. Ndio maana wakifukuzwa kwasababu ya aidha utovu wa nidhamu au kuonewa wanaanza kupayuka ovyo ovyo kwasababu walijihakikishia uwaziri au ukubwa fulani serikalini
endepo chama kikishinda.

Watazuia watu wengine kuingia kwenya vyama mbadala. Ngoja niwambie vijana wangu kwamba kila mtu ana jukumu la kufanya, inawezekana wewe jukumulako lilikua kukifikisha chama kuwa na
vuguvugu la kitaifa (ukishia hapo utakumbukwa tu), na ili ufanisi uendelee inawezeka kuna mtu mwingine anatakiwa achukue kiti kwenda mbele.

Ndio maana hata Muumba huwa anapanga majukumu kwamuda fulani
na kwa mtu fulani, hivi Mwenyezi Mungu alishindwa kuzuia kifo cha Yesu Kristo mpaka afe akiwa kijana mbichi
kabisa, ni kwamba kazi aliyotumwa ilishakamilika hapa duniani kimwili.

Hili si tatizo ila changamoto inayotakiwa kufuatiliwa kwa karibu sana na viongozi wa vyama, na vijana walioko ndani na nje ya vyama tusikate tamaa na hulka za jeuri, kiburi nk. za baadhi ya vijana Ili tusonge mbele, kwa mtanzania mwenye nia njema, busara na akili timamu anajua mabadiliko ni lazima.

Tatizo lililopo ni woga wa mabadiliko tu ambacho ni kitu cha kawaida kwa binadamu wengi (mara nyingi binadamu hukinzana na mabadiliko), kinachotakiwa ni elimu. Kila mtu kwa nafasi yake awe chachu yamabadiliko ya kisiasa maana Tanzania sasa kila kitu ni siasa. Tuweke ubinafsi pembeni wa kudharauriana miongoni mwetu (nilifurahishwa sana na wabunge wa upinzani kuunga mkono kwa nguvu zote hoja ya Mh. Mbatia ya mfumo wa elimu bilakujali tofauti za itikadi za vyama vyao).

Kitakachonifanyanimkumbuke President Hon. Dr. J. M Kikwete baada ya kustaafu:
Mheshimiwa raisi wangu mpendwa, najua wewe huna makuu kwahulka yako, huna uroho mkubwa wa
mali, ni mtu wa watu, mpenda amani nk. Naombazawadi moja tu kutoka kwako ambayo itatufanya tukukumbuke siku zote.

Ukitupawatanzania hiyo zawadi tutafurahi sana na kukuombea wewe na kizazi chako wakatiwote,
ukitoa hiyo zawadi mimi mwenyewe nitakutetea mahali popote nitakapokuwahadi tone la mwisho la jasho langu bila woga.

Zawadi yenyewe ni kusaidiakuiondoa CCM madarakani wakati huu watanzania tukiwa bado na umoja.
I am veryserious Hon. President more than you can imagine. Hon. President tusema ukwelijinsi wenzetu wakenya
wanavyo fanya vizuri baada ya Mh. Arap Moi kuwapa zawadiya mabadiliko. Wakenya hawawezi kumsahau Moi
hata kama kuna mambo mengi mabayaaliwafanyia, na wakimbeza watakua hawajajua umuhimu wake (historia itamkumbuka tu mzee Moi).

Ni kazi ngumu, tena ngumu kweli kweli lakini Mwenyezi Mungu atakulinda na sisi wenyewe tutakuombea.

Ujue kwamba kazi ngumu kama hii ndio inajenga historia ya binadamu. Unayo nafasi ya kutoa hiyo zawadi kwa sababu mazingira yanaruhusu na itumie vizuri mheshimiwa.

Asilimia kubwa ya wana CCM wanajua
wata ipenda hiyo zawadi (tatizo ni uwoga wa mabadiliko tu) achilia wale wachache wachumia tumbo ambao wanasema CCM italeta mabadiliko wakati wanajua haiwezekani.

Maana kila kitu hai kinazaliwa, kinakua na kufa. CCM ilizaliwa,ikakua na sasa iko kwenye hatua ya kufa labda kama haina uhai (usidanganywe na idadi kubwa ya watu kwenye mikutano yenu).

Kila mtu anajua hotuba zako za mwanzo zilivyokua na mashiko, na tunajua ulichokua unakisema ulimaanisha ila tatizo ni hilo dudu kubwa linaitwa CCM.

Mimi mwenyewe nakumbuka ile hatuba yako ya kwanza kwa bunge ulipopata uraisi awamu ya kwanza (a marvelous speech ever),ni hatuba iliyojenga matumaini mapya kwa watanzania Nakuomba upate muda kidogo ujaribu kuisoma tena mwenyewe ile hotuba utanielewa vizuri, najua ulikua na nia njema kabisa lakini hili dudu ccm?????

Uhai unaweza kuendelea kukifanyika rejuvenation nje ya system. Hivi Hon. President huona hata hao wazungu wanaotutawala kwa mbali vyama vyao vinapojisahau huwekwa pembeni na baadaye vinarudi upya baada ya ku-rejuvinate. Hutakua mtu wa kwanza kufanya kazihiyo mpendwa Ho.President (Moi alifanya, Gorbachev wa urusi ya zamani alifanyaetc).

Mwisho niseme ukweli toka moyoni kwamba kwa hili niko serious, am real very serious. Siwezi kukudhihaki kwa sababu najua fika Madaraka/mamlaka yako yalivyo na mimi ni kama sisimizi hata ukitaka kufanya lolote atanikanya kwa muda wa sekunde tu na wala watu wasijue nini kimetokea achilia mbali nchini hata kijin ikwangu hapa nilipo. Kama utanielewa vibaya, NAOMBA UNISAMEHE BURE TU ila najua baadaye utakuja kufahamu nilikuwa namaanisha nini
.
MWENYEZI MUNGU AKULINDE HON. PRESIDENT, AKUPE AFYA NJEMA NA MAISHA MAREFU NA HEKIMA ILI UTUPE HIYO ZAWADI WAKATI HUU.

MUNGU IBARIKI TANZANIA ILI TUWE WAMOJA KWA USTAWI WA WOTE.
 
Back
Top Bottom