Mutensa
JF-Expert Member
- Feb 20, 2009
- 421
- 90
Wapendwa,
si vibaya kushirikishana mambo ya maanjumati kutokana na uzoefu.
leo nimeamua kuwasaidia mabachela ili waache kula vyakulahafifu kwenye mama ntilie wajitengenezee misosi home haraka.
Basi tenga muda kwenye weekend nunua vitunguu vya kutosha, vitunguu swaumu, pilipili hoho, nyanya kiasi na vinginevyo vinavyokufaa kutokana na "taste".
Sasa utamenya nyanya nyingi tu, kata kata vitunguu kama vinne hivi na hoho za kutosha.
pima mafuta ya kutosha kupika nyanya hizi.
-- Kaanga vitunguu kama dk 2 halafu tia pilipili hoho
-- kaanga kwa dk nyingine 3-5
-- sasa mwaga nyanya zilizokatwakatwa
-- usiweke maji, endelea kuchemsha.
-- weka chumvu (na pilipili kama ni mpenzi).
chemsha mchanganyiko huu kwa kama dk 15 na baada ya hapo sauce itakuwa tayari. Ipua, subiri ipoe, halafu iweke kwenye chupa au bakuli lenye mfuniko.
Tunza kwenye fridge tayari kwa matumizi ya wiki nzima.
Namna ya kutumia mchanganyiko huu:
Mpaka hapo mchanganyiko hu utakusaidia kupika kwaharaka - iwe nyama, kuku, maharage, samaki au mboga yoyote - hauhitaji kukaangiza tena. Chukua kiasi cha huu mchanganyiko, weka kwenye mboga yoyote na chemsha. Utapata msosi wako mzuri sana fasta.
Kama una ipad yako, ingia jikoni - weka music au endelea kusurf mama yule jamaa wa zantel wakati huo msosi unajipa.
Kila la heri.
Hii sio shule ya kitabuni, its real life experience.