Maaskovu Vs. Makamba na mgongano wa Arusha

Ni kweli Makamba natumia Biblia kwa ufinyu sana. Ukisoma Biblia utakuta Manabii wengi sana walikuwa wakitumia muda mwingi kuwakosoa watawala wa Israel/Yuda na wengi wao walipata misukosuko sana. Nabii Elisha, Nabii Isaya na Yeremia ni mifano mojawapo. Ilifikia Nabii Yeremia akatumbukizwa kwenye kisima kwa kumkosoa na kumkemea Mfalme. Kazi wa watu wa dini ni pamoja na kukosoa watawala.
 
Kwani Wakiristo ndio kina nani? Slaa yumo? Mbowe yumo?

Na wapi kwenye Bibilia iliposema "hiki ni kitabu cha wakiristo"?

Ukishindwa kujibu, kaa kimya! SHUT UP.

Kama ulijua hayo yote mbona ukauliza, wewe ndio ulitakia kukaa kimya
 
Ila na maaskofu kwa makusudi au vinginevyo wana selective memory. ... Mbona hawakumkemea Kilaini wakati alipotoa ufunuo fake kuwa JK ni chaguo la Mungu? Au Mungu kabadili mawazo sasa anamtaka Slaa? Na huyo Mungu kaamua ku-overlook "fornication" ya PHD (Cannon Law). Looks like that god is troubled these days!
Sijui ni kwanini askofu Kilaini alisema Kikwete ni chaguo la Mungu, lakini haimaanishi kuwa hata kama ni kweli chaguo la Mungu, hawezi kukosea na Mungu hawezi kumkataa baadae kama ameacha misingi ya haki. Kitabu cha Wafalme kinaeleza habari za Sauli, mfalme wa Israeli aliyechaguliwa na Mungu lakini alipopotoka, Mungu alimwacha na kumteua Daudi mchunga kondoo kuwa mfalme mpya badala yake.

Si lengo langu kusema kuwa Kikwete alikuwa chaguo la Mungu au la au kuwa Mungu amemwacha au la (hayo ni mambo ya imani, kila mtu moyoni mwake na kwakuwa tuna imani tofauti, hiyo italeta shida), isipokuwa hiyo kejeli ya kusema "looks like that god is troubled.." ndio imenifanya nitoe mfano huo.

Halafu, hivi Dr.Slaa anahusika vipi na kauli hiyo ya maaskofu hadi umhusishe hapa?Au ni bahati mbaya kwake kujikuta ni muumini wa dini ya Kikristo na kuwa na historia ya upadre n.k? wapi maaskofu walisema "Kikwete si chaguo la Mungu kwa 2010, Dr.Slaa sasa ndiye!"?? Isitoshe, Kilaini yuleyule aliyesema Kikwete ni chaguo la Mungu, hajawahi kukanusha, na hata 2010 alirudia kauli hiyo ya Kikwete kuchaguliwa na Mungu, what is Dr.Slaa to do with that?

If you ask me, i think we're doomed!Suala la udini limepata manabii wa kulishabikia(wakristo kwa waislamu) na hawatachoka hadi waone wakristo na waislamu hatupikiki tena chungu kimoja! God (not the troubled one) help us!!
 
makamba ni wa kumpuuza kabisa, anapotosha sana maandiko matakatifu kwa manufaa yake ili awez ku capture majority interest. anaongea ujinga kam mamlaka zote zimewekwa na Mungu, huu ni upotoshaji wa hali ya juu, kasahau kuna serikali na dola za kishetani kama yaYezebeli, Balamu. anataka kusema hata Bagbo wa Ivory nae kawekwa na Mungu au kajiweka mwenyewe. huna nidhamu kwa Mungu mzee
 
Sasa Chadema kinazidi kujidhihiisha kuwa na chama cha kidini na hasa Ukatoliki ambao kasomea Slaa, walikuwa wapi kulaani kwa nguvu watu wa Pemba walipouwa kipindi wanaandamana? sio hawa walithubutu kusema kuwa CUF inapaswa kulaumiwa kwa kukataa kutii amri ya Polis? na huyu Kikwete walisema ni chaguo la Mungu, iweje leo awe chaguo la shetani? au kwa sababu kaondoa memorandum of understanding?

Kalaga baho na ubozi wako myago Hata mmbwa akitangaza wanacho kibainisha CDM mimi nitamfuata Bila kujali masika au kiangazi Kengele au Azana Ima Dogoli au Wegu!
DAWA DAWA Ni kwa ccm ifanye kweli tena kwa nguvu na dhamira ya kweli kuindoa nchi kwenye UJINGA,UMASKINI,NA UFISADI Hapo CDM Itakufa kifo cha me mende bila hivyo roho ya CDM Haitakufa daima.
HABARI NDIO HIYO
 
Hivi katika CCM yooote..hakuna mwenye akili zaidi ya Makamba mpaka waongozwe na mtu mjinga kama yule? Yaani CCM ni chama so low intellectually kiasi hicho?
 
Nchi inaongozwa na katiba sio Biblia, ila kwa kuwa Makamba hana elimu hana uwezo wa kunukuu katiba, kwanza inahitaji uelewa wa kisheria angeongea nini mbumbumbu yule!
 
Hivi katika CCM yooote..hakuna mwenye akili zaidi ya Makamba mpaka waongozwe na mtu mjinga kama yule? Yaani CCM ni chama so low intellectually kiasi hicho?

Tabwe Hiza - Mtambo mwingine wa CCM.
 
Tunaelewa msimamo wa Maaskofu wenye maadili! huwezi kuwalinganisha na viongozi wengine wa dini zisizokuwa na msimamo! zinazopendelea mtu wao! na zinazojaribu kupenyeza hoja za kijinga wakati watu wao wapo kwenye system!
Ni Hivi, maovu hayana mipaka! iwe katika jamii, siasa na sehemu nyingine yoyote! watu makini kama viongozi wa dini ni kuwaongoza watu kuepuka maovu na kutenda mema. Hii ni kwa ajiri ya faida kwa jamii nzima. Utakuwa mpumbavu sana kiasi cha kudharaulika kama ukifanya maovu katika siasa harafu useme viongozi wa dini wasizungumze! Mauaji na Wizi unaofanywa na Watanzania wenzetu waliopewa dhamana ya kuongoza na wananchi kwa kushirikiana na watu wengine wa nje ni uovu unaostahiri kukemewa na kulaaniwa na watu wote wenye ufahamu. Makamba na chama chake kwa sasa ni sehemu ya waouvu, na ndio maana Maaskofu wanakemea! Ni vema sasa Watanzania wananyosha mikono, wanasema inatosha, wanaamua kufa kwa faida ya kizazi kijacho! hii itaendelea hadi pale haki itakapotendeka!
 
Sasa Chadema kinazidi kujidhihiisha kuwa na chama cha kidini na hasa Ukatoliki ambao kasomea Slaa, walikuwa wapi kulaani kwa nguvu watu wa Pemba walipouwa kipindi wanaandamana? sio hawa walithubutu kusema kuwa CUF inapaswa kulaumiwa kwa kukataa kutii amri ya Polis? na huyu Kikwete walisema ni chaguo la Mungu, iweje leo awe chaguo la shetani? au kwa sababu kaondoa memorandum of understanding?

Wakati ule CUF ndio wenye nguvu, Chadema hakikuwa na nguvu. Mbona huulizi vyma vingine?
 
Askofu Kilaini kusema Kikwete ni chaguo la Mungu si tatizo! kwani hata Rusfel alikuwa malaika lakini unaona kazi yake ya kishetani mpaka wamezaliwa rusfel wengi akiwemo Makamba! watu wengi walikuwa na Tegemeo na kikwete lakini bahati mbaya sisi siyo malaika wa kumjua mtu upande wa pili na haya ndio yametupata! watanzania hawana tena matumaini ya maisha bora! mbele ni giza!
 
Ukiwaona the so called great thinkers, hawaoni tatizo la viongozi wa dini kuingilia mambo ya siasa na kutugawa watanzania basi ujue tunakokwenda siko. Yaani GT can not think beyond udini....Hawa viongozi wa dini wameshakosea mara ngapi ? Sasa wakiambiwa ukweli wafuasi mnakua wakali, ndio maana waliwaambia Kikwete ni chaguo la mungu...

Asante Mkuu,

Nawatahadharisha tu HAO MAASKOFU PAKICHAFUKA TUSHIRIKIANE SIO WAO WANAKIMBILIA UBALOZI WA VATICAN KUOMBA HIFADHI MAANA WAO NDIO CHANZO!!!!
 
Unajua maaskofu na mapadre vile vile wana TAALUMA kwani wengine ni Madokta(MD), wamesomea sheria(sio sharia), political sc, saikolojia, etc, kwa hiyo kinapotokea Tatizo linalohusu taaluma yake ikipindishwa ama yeye kuwa na upeo hii inafanya mtu aweze kutetea na kuwa mkali ili nafsi isije kumsuta

Hivi nikuulize nini tofauti ya PhD ya divinity na PhD ya islamic sharia maana wako masheikh dar wanazo hizo ila waislamu hawapendi kuitwa Dr maana wana jina lao maalum nalo ni Sheikh. tuondosheeni ujinga wenu hapa
 
Safi saaaana, makamba nazani AMEISHIWA.

Makamba nampa ushauri, Hajue kizazi hiki na Nyakati hizi sio zile za kipinde kile kwamba Woteeee ni CCM wa kila kitu NDIO, uongo NDIO, zambi NDIOO....Hapana, Nyakati hizi watu WAMEFUNULIWA, si wajinga na wapumbavu kama zamani, Watu WAMEFUNULIWA Uchafu na UOVU wao, HAWATAKI TENA KUWA NCHINI ya DHULUMA, UJINGA, UPUMBAVU na UONGO.

Hakuna tena mtu wa kumdrive, labda home kwake......

HAKUNA TENA KWA WATANZANIA, tena namshauri kuwa AJUEA WATU WASHAMCHOKA, na hana kabisa CREDIT katika Jamii hivi sasa, NI BORA AJITUBIE na ATUBU zambi zake AJITULIE.
 
That guy known as makamba is useless in thiscountry.he is neither intelligent nor wise.he is a disaster to this nation
 
Hivi nikuulize nini tofauti ya PhD ya divinity na PhD ya islamic sharia maana wako masheikh dar wanazo hizo ila waislamu hawapendi kuitwa Dr maana wana jina lao maalum nalo ni Sheikh. tuondosheeni ujinga wenu hapa
kama sheikh yupi? acha uongo mtaje mwenye PHD in sharia law hapa Tanzania
 
kama sheikh yupi? acha uongo mtaje mwenye PHD in sharia law hapa Tanzania

Nakupa mmoja ukamtafute yupo msikiti opposite na Chuo cha biashara (CBE) anavaa miwani mikubwa na anasalisha hapo ni imam pale ana PhD ya sharia laws ameipa Al-Azhar University. Hajiiti Dr kama Madr wenu wa Divinity na ukimwita hivyo hapendi ila watu hutoka pembe mbali mbali za dunia kumfata kwa ushauri.
 
Sasa Chadema kinazidi kujidhihiisha kuwa na chama cha kidini na hasa Ukatoliki ambao kasomea Slaa, walikuwa wapi kulaani kwa nguvu watu wa Pemba walipouwa kipindi wanaandamana? sio hawa walithubutu kusema kuwa CUF inapaswa kulaumiwa kwa kukataa kutii amri ya Polis?

CHADEMA kujidhihirisha kuwa chama cha Kikristo, kwa lipi? Mbona sioni uhusiano ktk hoja yako? Kwamba CHADEMA ni chama cha kidini kwa vile kiliandamana kupinga uchaguzi holela wa meya, na kisha kupigwa mabomu ya machozi na risasi za moto hata watu kuuawa, na CHADEMA wakapinga uonevu huo. Sasa udini uko wapi?

Kwa kuhusisha kwako na yaliyowapata CUF, inanipa picha kuwa wewe umeumizwa na yaliyoisibu CUF hata kupoteza ushawishi wake Tz Bara. Lakini hasira zako inabidi uzipeleke CCM na si CHADEMA, kwani wao ndo walioamuru polisi kuua raia wasio na silaha mwaka 2001 huko Znzbr. Isitoshe ni CCM haohao waliohubiri kuwa CUF ni chama cha kidini, sasa naona wewe na wenzako mna falsafa ya "tukose wote" kwa kutaka na mzimu uliowatafuna ninyi uitafune na CHADEMA.

Lakini mimi naamini hii ni changamoto nzuri kwa CHADEMA. Kwakuwa hizi ni siasa, wao kama kweli ni makini kama wanavyosema, watapaswa kuithibitishia jamii kuwa hizo shutuma si za kweli, na hiyo itadhihirisha ukomavu wao na itazidisha maradufu imani ya wananchi kwao. Personally I think this is the ultimate test, against all the odds CHADEMA coming out clean of all exclusion speculations, and that my friends is the only thing standing between CHADEMA and the state house!
 
Back
Top Bottom