Maaskofu wa DECI ni WACHUNAJI -MTIKILA

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,148
Wakati huohuo, Mchungaji Mtikila amewacharukia wachungaji na maaskofu wanaodaiwa kupanda mbegu kwenye taasisi ya Deci na kwenda kuzivuna kinyemela baada ya serikali kuizuia kufanya kazi, akidai hao si wachungaji wa watu bali ni wachunaji.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika juzi Jumamosi kwenye viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam uliokutanisha wapandaji na kamati ya dharura ya wanachama hao, Mtikila alisema habari za kuwapo watu wakubwa kung’oa fedha zao ni za kusikitisha.

"Nimepigiwa simu na baadhi ya watu wakinieleza wazi kuwa kuna baadhi ya maaskofu na wachungaji waliokuwa wamepanda mbegu zao Deci eti wameng'oa mbegu hizo kinyemela, hizi ni habari mbaya kuona mchungaji anayetakiwa kuchunga kondoo anamshawishi kondoo wake kuweka fedha Deci na baadaye anakwenda kuchukua kimya kimya na kumuacha kondoo huyo akihangaika, huyu si mchungaji wa kweli bali ni mchunaji," alisema.

Mtikila alisema kitendo cha watumishi hao wa Mungu kuchukua fedha zao kimya kimya na kuwaacha waumini wao wakihangaika, kinampa mashaka juu ya ushiriki wao katika taasisi hiyo.

Katika hatua nyingine mwenyekiti wa kamati ya dharura ya wanachama wa Deci, Mchungaji Isaack Kalenge ameeleza kufurahishwa na uamuzi wa serikali kuzuia Deci kutoa fedha kwa wanachama waliotakiwa kuanza juzi, akisema utoaji fedha hizo ungesababisha watu kupoteza haki zao.

Alisema yeye kama mtetezi wa wanachama anapingana na kitendo cha uongozi wa Deci kinachodai watu watakaolipwa ni wale ambao hawajawahi kuvuna, akisema kufanya hivyo ni kuonea wanyonge.

Kalenge alisema yeye na kamati yake wameamua kujitolea kushughulikia suala la wanachama wa Deci hadi wanahakikisha wanapata haki zao ili kusiwe hata na mmoja anayedhulumiwa.

Wakati huohuo leo katika ofisi za Deci zoezi la kuorodhesha majina ya wanachama kwa ajili ya kuja kung’oa mbegu zao linaendelea baada ya mapumziko ya siku ya Jumapili.

Kwa mjibu wa ratiba iliyotolewa na uongozi wa Deci zoezi hilo litaanza saa za kawaida za kazi na utaratibu wa kawaida wa kuorodhesha majina kwa kutumia namba unaendelea kutumika.

Katika hatua nyingine Fidelis Butahe anaripoti kuwa wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wameibuka na kuitupia lawama serikali kwa kuifungia taasisi ya Deci.

Mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Nathaniel Mlaki alisema uamuzi huo wa serikali unaonyesha ni jinsi gani isivyojali maendeleo ya wananchi.

"Tangu uhuru mpaka hivi leo hakuna chombo chochote kilichowekwa na serikali kwa ajili ya kusaidia wananchi wenye kipato cha chini, lakini Deci ilifanya hivyo na hakuna mtu aliyelalamika kutapeliwa na taasisi hii sasa kwa nini ifungiwe.

"Wastaafu tumedai fedha zetu tumeishia kufunguliwa kesi, washiriki wa Deci ambao wengi ni walalahoi wamepanda mbegu, lakini sasa taasisi hiyo imefungiwa. Kwa nini kila mwananchi wa kipato cha chini anapokuwa katika utaratibu wa kujikwamua, serikali inaingilia kati; hivi hiyo ndio demokrasia?"
 
Tufike wakati tuache kulalamika na kila mtu awajibike kwa matendo yake.
Katika hili swala la DECI wahusika kwa maana ya wanachama inabidi wawe responsible for their decisions and actions.
 
He mbona MUSA wetu amebadilika tena??
si alisema haya ni maono ya MUNGU haya??
He hii kali
 
Mtikila naye haeleweki , sasa kam wachungaji walipanda mbegu zao waaache kwenda kuchukua, pamoja na kwamba ni wachungaji lakini ni binadamu pia wana mahitaji na wana mapungufu yao. Na wachungaji wengi wa makanisa ya kiroho ambayo hayajakua kihuduma waumini huwa ni wachache na wao wanategemea sadaka,kwa hiyo lazima walishtuka mapema ndo wakaenda kuchukua hela zao.
 
Tumwelewe MCH>.MTIKILA, anachosisitiza ni kiongozi kuwa mfano kwani si vyema kufanya kimya kimya pasipokuwataadhirisha na unaowaongoza....!
To be honest I support the clergyman for this......! Wachungaji na maaskofu wawe mifano katoka hili
 
sasa hawa watz wamekuwa kondoo.

mtikila na wenzako kama munataka kuwa wachungaji kawasaidieni wamassai huku kuchunga ngòmbe,mbuzi na kondoo sio mugeuze watu kondoo.

ka hao kondoo nyie nani (wachungaji)?

umepata kuona wapi kondoo akamchuka kondoo mwenzake?
 
Kwenye hii issue ya DECI inaonyesha wazi Kanisa limekosa direction, wameamua ku-ignore bible wanayo dai ni neno la Mungu, Bible clearly imekataza RIBA lakini watu wa dini hii wakiongelea swala hili hakuna hata mmoja anaeligusia, wanakariri maneno ya Pinda kua Deci iko established illegaly, hakuna reference kutoka kwenye bible, sasa bible haina value kwao

Inabidi ndugu zetu hawa warudi kwenye kitabu chao au watakua kondoo waliopotea
 
Nasikia imendikwa kuwa "...walionacho wataongezewa na wale wenye kidogo watanyang'anywa."

Ndio hivi tunayaona...! Na ndio wasomi wetu hao...! Wanakulana wenyewe kwa wenyewe lol!
 
hehehe.....jamani poleni maana ukisikia "mtu anapanda mbegu afu inakuja mvua na kuharibu mashamba ndo huku" wazungu husema....there is no royal way to success
 
Huo ni utapeli ambao umeshatokea majuu ila hapa bongo ulichelewa kufika , sema ndio bongo naona safari hii wamezidiwa kete kwa ujumla.
 
Huo ni utapeli ambao umeshatokea majuu ila hapa bongo ulichelewa kufika , sema ndio bongo naona safari hii wamezidiwa kete kwa ujumla.

MKUU MWIBA BONGO ULISHAFIKA SIKU NYNGI WATU WABISHI
UNAKUMBUKA FAIDIKA...,UNAKUMBUKA ILE YA MAMA RUPIA....BADO TUNANGANGANA
 
Hivi hawa jamaa wataendelea kudanganywa mpaka lini!?
Wakati mwingine tunashindwa hata jinsi ya kuwahurumia! Si kazi waliambia kuwa DECi imebarikiwa...!
 
Wabongo ni wabishi sana.... hawasikii na wanapenda sana mambo ya bure bure..... sasa kuna nyigine ipo mitaani inaitwa PUFDIA..
 
Mtikila naye haeleweki , sasa kam wachungaji walipanda mbegu zao waaache kwenda kuchukua, pamoja na kwamba ni wachungaji lakini ni binadamu pia wana mahitaji na wana mapungufu yao. Na wachungaji wengi wa makanisa ya kiroho ambayo hayajakua kihuduma waumini huwa ni wachache na wao wanategemea sadaka,kwa hiyo lazima walishtuka mapema ndo wakaenda kuchukua hela zao.

Mbado tu haukujua kuwa huyu jamaa ni msanii na opportunisit anatafuta tu pa kutokea ili aendelee kubaki live
 
Back
Top Bottom