Maandamano yanukia kata ya mavurunza kimara ni kuhusu majina ya watu waliochaguliwa kufanya sensa

mirindimo

JF-Expert Member
Nov 2, 2009
821
1,343
Jana mida ya mchana ofisi za kata ya mavurunza kimara ilitoa majina ya watu waliochaguliwa kufanya zoezi la sensa ya watu na makazi, ni orodha iliyokua ndefu iliyotokana na watu takribani 1200 walioomba kufanya zoezi hilo,

kitu kilichoshangaza raia hawa na kubaki na sintofahamu ni leo asubuhi baada ya orodha ile kutolewa na kubandikwa orodha nyingine ambayo ina majina tofauti na yaliyokuepo katika orodha ya mwanzo na inasemekana asilimia kubwa ya majina hayo hawatoki maeneo ya kimara bali ni orodha ya viongozi waliyokua wameiandaa wao kwa maslahi binafsi...

Hivi sasa raia wanaendelea kusogea katika ofisi hizo za kata huku wengi wao wakiwa ni wale waliotolewa katika orodha ile na wametishia kuandamana ili haki itendeke, wakati huo huo inasemekana ndani ya ofisi hizo za kata ya mavurunza kuna kikao kigumu kinaendelea ndani....tutaendelea kuwajuza yatakayojiri
:director:
 
Back
Top Bottom