Maandamano ya Amani Nchi Nzima

Nakuakikishia KIKWETE atatawala kwa taabu sana awamu hii ya miaka mitano! Maana hari si hari tena! Mambo yanaanza hivi; Msukumo kutoka kwa wafanyakazi wa serikali bado ni ngoma nzito, kwani wengi wamejenga chuki kubwa kwa serikali tangu jamaa alivyoasema hana shida na kura za wafanyakazi! nina imani ata mei mosi ya 2011 hawatamualika.

Msukomo wa pili ni wanafunzi wa vyuo vikuu waliopevuka ambao kwa sasa serikali wanaiona kama sokomoko. Hasira za wananchi wengi juu ya maumivu yatokanayo na ugumu wa maisha unaosababishwa na Wezi wa rasilimali za nchi wakishirikiana na wakubwa Serikalini.

Vyama vya kiraia, Na changamoto ya Bunge lenye watu wachache makini! HIVYO MAANDAMANO YAPO! WEWE SUBIRI TU UTAJIUNGA YATAKAPOTOKEA! MAANA WATANZANIA WENYE UFAHAMU HAWATAKI KUFANYWA WAPUMBAVU TENA!
 
Kwenye list umewasahau wakurugenzi wa halmashauri Aibu, huko kuna mapigo mwenyewe utachoka. Cheki na ripoti ya CAG kujiridhisha. Elimu na afya bure vinawezekana kwa viongozi makini lakini sio hawa wa ccm. Lakini pia hawa wzaee wa ccm wananichefua kabisa sijui haya maumivu wenzetu hawayasikii au ndo unduminakuwili, hebu wape hiyo list mwanawane!
 
Saa ya ukombozi?

Embu tuendeleeeni maneno ya kilokole kwa jambo la nchi?

Ukombozi kwa yesu ok?
 
Greatthinkers;
Nadhani wakati ni huu, isiwe kanda ya ziwa tuu bali iwe inchi nzima.
Wananchi wamebakia yatima, tumaini pekee ni CDM.

Mwanza Ilizizima,

Musoma Ikaunguruma,

Shinyanga imerindima.

Freedom is coming tommorow

Peoples..............power.:A S 13:
 
GrEaTthinkers,

Think kiasi gani tumepoteza kama taifa,
Kwa nini jasho letu linatumika vibaya hivi!

  • TICTS
  • RADAR
  • NDEGE YA RAIS
  • SAFARI ZA NJE YA NCHI-UTADHANI YEYE NI WAZIRI WA MAMBO YA NJE
  • TWIN TOWERS BOT
  • MIKATABA ISIYO NA TIJA KWA NCHI(Madini)
  • KAGODA(EPA)
  • MEREMETA
  • RICHMOND/DOWANS
  • WAKUU WA MIKOA na WILAYA(Hao ni Watumishi wa CCM)
  • IPTL
  • KIWIRA COAL MINES
  • NETGROUP SOLUTIONS
  • MISAMAHA YA KODI(Nchi inakosa mapato)
  • ALEX STEWART
  • BEI YA BIDHAA ie. UMEME (watanzania ndiyo wanaofidia misamaha ya kodi)
  • RITES
  • ALLIANCE AIR
  • KUJENGA BARABARA KUPITIA MBUGA YA SERENGETI(Matumizi mabaya ya kodi zetu)
  • LOLIONDO
  • BARABARA YA KILWA NA MANDELA KAZI KURUDIWA(Matumizi mabaya ya kodi zetu

Nasema hawa si wa kuchekea wanaiumiza Nchi,

Kwa Asili ni sisi ni matajiri, tunafilisiwa na wapuuuzi

Haiwezekani madudu yote hayo, hakuna hata mwenye hatia ukitoa Liyumba.

Ukinunua soda ya 500Tsh umetoa 90Tsh. kama kodi.

Amkeni, Toeni sauti, Nchi inakwisha.:target:

....huyu jamaa alitakiwa awekewe vikwazo vya kusafiri! polisi wa mkamate na kumshtaki kwa kosa la uzururaji wa ovyo!!!! manake yupoyupo tu wakati nchi inaenda kombo!!!!!
 
Maandamano tayari Chadema wameanzisha tuwaunge mkono kuyaboresha hadi yafikie Mapinduzi halisi ya nguvu ya umma, kama Misri tu
 
GreatThinkers&Frontliners;

Tengenezeni Mabango yanayoonesha mikataba mibovu yote kama nilivyoainisha.

Taalifuni wananchi namna gani inavyowazuru wengi na kuwaneemesha wachache.

Peoples................Power!
 
Nakuakikishia KIKWETE atatawala kwa taabu sana awamu hii ya miaka mitano! Maana hari si hari tena! Mambo yanaanza hivi; Msukumo kutoka kwa wafanyakazi wa serikali bado ni ngoma nzito, kwani wengi wamejenga chuki kubwa kwa serikali tangu jamaa alivyoasema hana shida na kura za wafanyakazi.

Nina imani ata mei mosi ya 2011 hawatamualika! Msukomo wa pili ni wanafunzi wa vyuo vikuu waliopevuka ambao kwa sasa serikali wanaiona kama sokomoko! Hasira za wananchi wengi juu ya maumivu yatokanayo na ugumu wa maisha unaosababishwa na Wezi wa rasilimali za nchi wakishirikiana na wakubwa Serikalini! vyama vya kiraia.

Na changamoto ya Bunge lenye watu wachache makini! HIVYO MAANDAMANO YAPO! WEWE SUBIRI TU UTAJIUNGA YATAKAPOTOKEA! MAANA WATANZANIA WENYE UFAHAMU HAWATAKI KUFANYWA WAPUMBAVU TENA!

babu wafanyakaz wamemwalika mei mosi kimakusudi il wasikilize pumba zake ndio watoe tamko.
 
GreatThinkers,

Mimi nina akili timamu na sijanywa maji bendera, Hivi ni nani kawaloga, 2011 watoto wenu form four ni 11% tu ndio waliopata div. 1-4 , katika hiyo mjue 9% ni private schools, wengine wote zero halafu mnanung'unika waziri mhusika yupo.

Hivi nani kawaloga, wizara ya nishati na madini imeshindwa kazi na waziri mhusika yupo anachekewa, Tena ni huyu huyu waziri alisababisha jana gari langu libaki Mwenge kituo cha mafuta kisa mafuta hayauzwi. Nimelala giza pia nyumbani.

Hivi nani kawaloga, kwa nini tusifanye maandamano ya amani kuonesha kukerwa na hii hali? Nani asiyejua kama mabwawa ya Mtera na sehemu zingine yamejaa tope na si kweli kwamba mvua hazitoshi?

Mbona kwa wenzetu pale Jinja Owen Falls inapiga mzigo bila tatizo? Amkeni jamani, hii nchi imeisha, pigeni kelele.

i Si Em basi Inatosha
 
wewe umesahau moja (NSSF)hili ndio chaka kuu la kutuibia fedha za jasho la watumishi na kuzipeleka kwenye miradi yao,na mwanachama anapotaka malipo yake inakuwa mizunguko maana fedha inakuwa imetumika kusikotakiwa na wánasubiri michango mipya ndo walipe wanachama. je huu si ufisadi??,
 
GreatThinkers,
Ni kweli NSSF ilitakiwa watoe hisa kwa wanachama ili kila faida inayopatikana kwa kila uwekezaji umfaidishe mwananchama.
Saivi tunatunisha matumbo yao, milion kumi unayoichukua baaada ya miaka kumi ni sawa na laki na nusu ya sasa kwa muda huo.

Roho ya ushetani na ufisadi imewajaa
 
Maandamano yanaendelea, ngoja tutoke arusha kesho utaona. Mbona bado hujaelewa, sasa hivi mpaka kieleweke. Kwanza unajua hata issue ya madini haijashughulikiwa na bunge?
 
ndugu zangu ujasiri ni asili, hapa wa2 wanajifanya majasiri kwa kuwa eti hawajulikani. pengine!

angalia kastro,
kwa mara ya kwanza aliingia library ya rais ya cuba wa wakati huo na kutafuta sana kitabu. alipoulizwa ww unatafuta kitabu gani akasema hii library ni bure kabisa, siku izo akiwa primary school. castro alimjib! kitabu cha kupindua serikali. mhudumu aliguna na baadhi ya wakubwa walimdharua kwa kuwa walimwona ni mtoto mdogo.
baada ya muda alimwandikia barua rais wa marekani wa siku izo jinsi walivokuwa wanachukizwa na raisi wa cuba wa wakati huo, raisi huyo wa marekani pamoja na rais wa cuba walidharua sana barua yake, ....ndipo catro akiwa mtu mzima alifanya mambo karne yoote yanakumbwa. na record zake zinajulikana kote duniani.

Unamfunza nini mwanao???WOGA???
 
labda tunasubiri kijana mmoja mwenye hasira na mzalendo kama yule wa Tunisia then hapo maandamano yanaweza kuanza...tuandae mhutasari ukielezea lini maandamano yaanze napendekeza viwanja vyote vya mipira kila mkoa viwe tahiriri..tusijali kupoteza mda kwa maslahi ya Taifa...
 
kabla ya maandamano napendekeza kutengenezwe kajarida kanakotoa mutahsari wa madudu yote hayo na kasambazwe nchi nzima hasa huko vijijini

naunga mkono hoja, tuwaeleze walioko vijijini kwa nini maisha ni magumu. Mafuta ya taa ni ghali mno kwa mtu wa kijijini.

Pia wapo watu huku mjini wasiojua kwa nini maisha ni magumu.hata huku mjini umeme haupatikani na mafuta taa ni tegemeo pia.

Wanasema tu fanya kazi kwa bidii, lakini hawajui uhusiano kati ya ufisadi wa ccm na maisha magumu.

Nipo tayari kuchangia gharama za uchapishaji na usambazaji.

Uwekwe mkakati sasa hivi wa kuchapisha na kusambaza ili usihujumiwe.

Nitachangia pesa na nitaingia barabarani pia kikamilifu
 
Back
Top Bottom