JACADUOGO2.
JF-Expert Member
- Dec 13, 2010
- 930
- 217
Wananchi wote wa Rorya hasa maeneo ya Shirati bila kujali Itikadi, Dini, Kabila wala Rangi tutafanya maandamano makubwa Alhamisi tarehe 17.11.2011 kuanzia saa 2:00 asubuhi. Maandamano hayo yataanzia maeneo ya Sota na kuishia Shirati - Obwere ambapo yatapokelewa na wananchi wenye hasira kali na wenye uchungu na nchi yao. Malengo ya maandamano hayo ni:
1. Kudai katiba mpya ya Tanzania
2. Kudai maji na mamlaka ya mji mdogo wa Shirati tuliyoahidiwa na waziri mkuu (Pinda) lakini baada ya CCM kushindwa na CHADEMA kwenye uchaguzi mdogo wa Udiwani kata ya Mkoma uliyofanyika 2/10/2011, CCM walikaa kikao cha kamati ya siasa na maadili na kuamua kuwa zoezi la kupeleka mamlaka ya mji mdogo na maji Shirati lisitishwe hadi baada ya 2015 kama CCM watashinda udiwani kwenye kata hii Mkoma na kwamba wakipeleka maji na mji mdogo Shirati itaonekana kuwa CHADEMA ndiyo wamefanya hayo yote na CHADEMA itaimarika ndani ya Rorya!
Kikao hicho kilihudhuriwa na mkuu wa wilaya ya Rorya, M/kiti wa CCM wilaya, Katibu wa CCM wilaya na wajumbe wengine wawili na tuna nakala ya hicho kikao na hayo maamuzi ya kipumbavu na ya kijinga!
Wote mliokaribu tunawakaribisha ili mtuunge mkono kwa mafanikio makubwa zaidi.