Maandalizi ya mkutano wa UKAWA/CHADEMA uwanja wa Jangwani

Status
Not open for further replies.
Sasa kama atashindwa kusimama hata dakika 30 kuhutubia ataweza ktk mikutano mikubwa ya kimataifa.?? Hoja ni kwamba tuangalie uwezo wa mgombea wetu, uhodari wa kuzungumza na watu, ushirikiano kati ya mwili na matamshi yake.

kwenda uko mikutano ya nje ya nchi watu wanatucheka mpaka mda huu rais kuimba mashairi mwanzo mwisho? Lowasa njo ufanye kazi
 
Mgombea wa urais kwa
tiketi ya CCM, Dk John Magufuli
amewashauri Watanzania
kutoharakisha kutaka mabadiliko na
mapinduzi yasiyo na mipango kwa
kuwa baadhi ya nchi zilizofanya hivyo,
sasa zinajutia uamuzi wao.
Mgombea huyo jana alitumia sehemu
kubwa ya mikutano yake kuwaeleza
wananchi kuwa anao uwezo wa
kukidhi kiu yao ya mabadiliko
wanayoitaka, hivyo hakuna haja ya
kuhadaiwa na watu wanaolazimisha
ukombozi na mabadiliko bila kufanya
tathmini ya kina.
Akiwahutubia wakazi wa Mbalizi,
Mbeya Vijijini, Dk Magufuli alisema
mabadiliko bora yanaweza kuja hata
bila kubadilisha chama kwenye
uongozi. Akisema hiyo ilitokea kwa
Chama cha Kikomunisti cha China
ambacho kilifanikiwa kuifanya nchi
hiyo ikue kwa kasi kiuchumi duniani
kiasi cha kuishinda Marekani.
Alisema nchi kama Libya, Tunisia, Iraq
na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
(DRC), wananchi wake walilazimisha
mabadiliko lakini leo wanajuta.
“Msitoe hukumu ya jumla, zipo nchi
zilifanya hivyo zinajuta. Libya ya
(Hayati Muammar) Gadaffi ulikuwa
ukioa unapewa nyumba, unatafutiwa
mtaji, maji, elimu na umeme bure
lakini wananchi walichoka raha,”
alisema.
“Wakasema anaondoka lakini leo hii
hakuna raha na wale vijana waliotaka
ukombozi wa haraka ndiyo wa kwanza
kuvuka Bahari ya Mediterranean
kwenda Ulaya.”
Aliwaomba Watanzania wamwamini
na kumpigia kura kwa kuwa akiingia
Ikulu hatakuwa na deni la kulipa kwa
sababu hakupata nafasi ya kugombea
urais kwa kuwalipa watu ili wamteue.
Alisema mchakato wa uteuzi aliufanya
kwa mwongozo wa Mungu ndiyo
maana hata fomu za uteuzi wa
mgombea urais ndani ya CCM
alichukua na kurudisha kimyakimya.
“Wapo watu wengine walitumia pesa
ili wachaguliwe, lakini walipoona mimi
nimechaguliwa wameanza kukimbia
wenyewe,” alisema Dk Magufuli.
Alisema wapo baadhi ya watu
wanamchukia kutokana na misimamo
yake ya kiutendaji na kukemea rushwa
ndiyo maana alipoteuliwa baadhi yao
ndani ya CCM walikimbia mapema.
Mgombea huyo ambaye ameendelea na
kampeni zake katika mkoa mpya wa
Songwe, alisema akiingia madarakani
atakomesha ujangili wa wanyamapori
kwa kuboresha masilahi ya askari wa
wanyama hao.
Alisema ni jambo la kushangaza kuona
tembo wanauawa kila siku na meno
yao kushikwa nje ya nchi, licha ya
kuwapo askari wenye bunduki za SMG
wakati Wamasai wanachunga ng’ombe
wao kila siku bila kuibiwa.
“Hivi kwani hakuna uwezekano wa
kuwapanga maofisa kutokana na
makundi ya tembo? Unampa tembo 30
kila askari halafu unamwambia nikute
hata jino moja limeng’oka wewe na
mimi na unampa mshahara mzuri,”
alisema Dk Magufuli akiwa Mkwajuni
wilayani Songwe huku akishangiliwa.
Alisema kuna watendaji wachache
wanaofanya wananchi waichukie
Serikali kwa kuiba fedha za maendeleo
za halmashauri na kwamba akiingia
wakurugenzi wote wa Manispaa na
halmashauri ambao ni wazembe
watakiona.
Waziri huyo wa Ujenzi, kila
alikohutubia aliahidi kujenga barabara
za lami na kumwagiza Meneja wa
Wakala wa Barabara (Tanroads) Mkoa
wa Mbeya kutangaza zabuni za ujenzi
wa barabara hizo haraka
iwezekanavyo.
Akiwa Mbalizi, aliahidi kujenga
kilomita moja ya barabara ya lami
wakati Mkwajuni na Makongorosi
aliahidi kujenga kilomita nne za ndani
na kumalizia ujenzi wa Barabara ya
Mbalizi – Chunya kwa lami kwa kuwa
Songwe imeshakuwa wilaya. Katika
siku yake ya tano ya kampeni, Dk
Magufuli aliahidi kuanzisha mfuko
maalumu wa fedha za kutoa pensheni
kwa wazee ili waweze kuishi vizuri na
kutoa ushauri kwa vijana.

Kusiharakishe kivipi? Inamaana miaka 54 bado haiwatoshi kuwepo madarakani? Kwaio tumewavumilia kwa miaka yote hiyo tumeona sasa basi tunafanya changes 2015. Pipooooz.!
 
idawa mi mwenyewe ni follower wa Dr SLaa ila kwa huu uj!nga unaoendeleza wa kusapoti magamba itoshe sasa, kumbuka ni sisi tuliowananga walioondoka na zzk na tukaponda siasa za kufuata mtu. Niliudhika na nimeudhika na chama kumpuza Dr Slaa ila nikilichukulia kwa hasira itakuwa faida kwa ccm. Now nipo kundini ccm ing'oke mengine tuulizane baadae. Dr mwenyewe anataka ccm iondoke ndio maana hataki kuzungumza kupinga chama japo hajaridhika

Dr slaa hakupuzwa bali alinunuliwa na ccm akawa anajishutukia mwenyewe, nguvu za umma zilimtisha kuhamia ccm moja kwa moja, Membe alimpatia Dola million 2 toka kwenye mapesa ya marehemu Gadafi.
 
Last edited by a moderator:
kwenda uko mikutano ya nje ya nchi watu wanatucheka mpaka mda huu rais kuimba mashairi mwanzo mwisho? Lowasa njo ufanye kazi

Lowasa hana maneno mengi yeye ni maneno machache yenye ujumbe mahususi, watu wamechoka na maneno mengi sasa ni wakati wa vitendo tu.
 
ccm huu si wakati wenu wa kutoa ahadi tunataka majibu kwa nini mmeshindwa kuondoa ujinga,umasikini na maradhi kwa miaka 54?
 
ccm huu si wakati wenu wa kutoa ahadi tunataka majibu kwa nini mmeshindwa kuondoa ujinga,umasikini na maradhi kwa miaka 54?

Wajinga ndio wamesha toka maradhi ndio yanawatesa. On to the next one
 
Mgombea wa urais kwa
tiketi ya CCM, Dk John Magufuli
amewashauri Watanzania
kutoharakisha kutaka mabadiliko na
mapinduzi yasiyo na mipango kwa
kuwa baadhi ya nchi zilizofanya hivyo,
sasa zinajutia uamuzi wao.
Mgombea huyo jana alitumia sehemu
kubwa ya mikutano yake kuwaeleza
wananchi kuwa anao uwezo wa
kukidhi kiu yao ya mabadiliko
wanayoitaka, hivyo hakuna haja ya
kuhadaiwa na watu wanaolazimisha
ukombozi na mabadiliko bila kufanya
tathmini ya kina.
Akiwahutubia wakazi wa Mbalizi,
Mbeya Vijijini, Dk Magufuli alisema
mabadiliko bora yanaweza kuja hata
bila kubadilisha chama kwenye
uongozi. Akisema hiyo ilitokea kwa
Chama cha Kikomunisti cha China
ambacho kilifanikiwa kuifanya nchi
hiyo ikue kwa kasi kiuchumi duniani
kiasi cha kuishinda Marekani.
Alisema nchi kama Libya, Tunisia, Iraq
na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
(DRC), wananchi wake walilazimisha
mabadiliko lakini leo wanajuta.
“Msitoe hukumu ya jumla, zipo nchi
zilifanya hivyo zinajuta. Libya ya
(Hayati Muammar) Gadaffi ulikuwa
ukioa unapewa nyumba, unatafutiwa
mtaji, maji, elimu na umeme bure
lakini wananchi walichoka raha,”
alisema.
“Wakasema anaondoka lakini leo hii
hakuna raha na wale vijana waliotaka
ukombozi wa haraka ndiyo wa kwanza
kuvuka Bahari ya Mediterranean
kwenda Ulaya.”
Aliwaomba Watanzania wamwamini
na kumpigia kura kwa kuwa akiingia
Ikulu hatakuwa na deni la kulipa kwa
sababu hakupata nafasi ya kugombea
urais kwa kuwalipa watu ili wamteue.
Alisema mchakato wa uteuzi aliufanya
kwa mwongozo wa Mungu ndiyo
maana hata fomu za uteuzi wa
mgombea urais ndani ya CCM
alichukua na kurudisha kimyakimya.
“Wapo watu wengine walitumia pesa
ili wachaguliwe, lakini walipoona mimi
nimechaguliwa wameanza kukimbia
wenyewe,” alisema Dk Magufuli.
Alisema wapo baadhi ya watu
wanamchukia kutokana na misimamo
yake ya kiutendaji na kukemea rushwa
ndiyo maana alipoteuliwa baadhi yao
ndani ya CCM walikimbia mapema.
Mgombea huyo ambaye ameendelea na
kampeni zake katika mkoa mpya wa
Songwe, alisema akiingia madarakani
atakomesha ujangili wa wanyamapori
kwa kuboresha masilahi ya askari wa
wanyama hao.
Alisema ni jambo la kushangaza kuona
tembo wanauawa kila siku na meno
yao kushikwa nje ya nchi, licha ya
kuwapo askari wenye bunduki za SMG
wakati Wamasai wanachunga ng’ombe
wao kila siku bila kuibiwa.
“Hivi kwani hakuna uwezekano wa
kuwapanga maofisa kutokana na
makundi ya tembo? Unampa tembo 30
kila askari halafu unamwambia nikute
hata jino moja limeng’oka wewe na
mimi na unampa mshahara mzuri,”
alisema Dk Magufuli akiwa Mkwajuni
wilayani Songwe huku akishangiliwa.
Alisema kuna watendaji wachache
wanaofanya wananchi waichukie
Serikali kwa kuiba fedha za maendeleo
za halmashauri na kwamba akiingia
wakurugenzi wote wa Manispaa na
halmashauri ambao ni wazembe
watakiona.
Waziri huyo wa Ujenzi, kila
alikohutubia aliahidi kujenga barabara
za lami na kumwagiza Meneja wa
Wakala wa Barabara (Tanroads) Mkoa
wa Mbeya kutangaza zabuni za ujenzi
wa barabara hizo haraka
iwezekanavyo.
Akiwa Mbalizi, aliahidi kujenga
kilomita moja ya barabara ya lami
wakati Mkwajuni na Makongorosi
aliahidi kujenga kilomita nne za ndani
na kumalizia ujenzi wa Barabara ya
Mbalizi – Chunya kwa lami kwa kuwa
Songwe imeshakuwa wilaya. Katika
siku yake ya tano ya kampeni, Dk
Magufuli aliahidi kuanzisha mfuko
maalumu wa fedha za kutoa pensheni
kwa wazee ili waweze kuishi vizuri na
kutoa ushauri kwa vijana.

anzisha thread yako a cha upumbavu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom